👉🏾Hongera rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI kwa asubuhi hii ya leo ambapo tunauanza mwezi wa pili kati ya miezi 12 ya mwaka 2020.
👉🏿Tunapoingia mwezi wa pili ni kiashiria kuwa mwaka unasogea na sio mwaka mpya tena. Ni kiashiria kuwa kama umeweka malengo mwanzoni mwa mwaka huu sasa ni muda wa kujiuliza spidi yako katika kufikia malengo hayo iko vipi.
👉🏿Mategemeo yangu ni kwamba Mungu ni mwema kiasi amnacho amekuwezesha kuamka salama na upo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kubadilisha maisha yako ili hakika 2020 iwe ya tofauti.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo linakuta uweke ahadi ndani ya nafsi yako kuwa mwezi Februari, 2020 utakuwa mwezi wa mabadiliko kwako kiasi ambacho hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu utakuwa umebadilika kifikra, kimawazo na kitabia. Mabadiliko hayo yanatakiwa yapimwe kwa vitendo vinavyolenga kuelekea kwenye hitaji la maisha yako. Mfano, kama una kiu kubwa ya kuwa na uhuru wa kifedha hakikisha mwishoni mwa mwezi huu uwe umeweka misingi ya kuboresha kipato chako.
✍🏾Misingi ya kundi hili ni kuwa na fikra ambazo zinapelekea kwenye utajiri wa kila sekta ya maisha yetu. Hivyo, ahadi ya kwanza ambayo nataka uanze nayo ni kuhakikisha mwishoni mwa mwezi Februari, 2020 uwe umejenga nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa. Siri kubwa ambayo inatofautisha tajiri na masikini ni namna ambavyo watu hawa kila mmoja anatumia pesa zake.
✍🏾Tajiri kabla ya kutumia anawekeza kwa kujilipa kwanza wakati masikini anatumia kiasi chote anachopata na kuongeza madeni juu. Katika kipindi hiki cha mwezi Februari, 2020 ninataka nione unachukua hatua maalum za kuhakikisha kila shilingi inayoingia mkononi mwako utenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kujilipa kwanza. Baada ya kujilipa ndipo ugawe kiasi kilichobakia kwenye matumizi mengine. Mfano, ukiamua kujilipa kwanza kila siku shilingi 1,000/= mwisho wa mwezi utakuwa na jumla ya elfu 29,000/. Kama utaendelea kujilipa kiasi hicho mwishoni mwa 2020 utakuwa una jumla ya 330,000/. Anza sasa kujilipa maana bado haujachelewa.
✍🏾Kupitia nidhamu ya pesa ya kujilipa kwanza utaweza kutenga kiasi cha fedha ambacho utakitumia kama mtaji kwa ajili ya kuanzisha au kukuza biashara ya ndoto yako. Hakika kama kila pesa unayopata unatumia yote bila kutenga kiasi chochote kwa ajili ya maendeleo maisha yako yataendelea kwenye uchumi wa wasiwasi au kifupi utaendelea kuwa masikini.
✍🏾Unapojilipa kwanza inakuwezesha kuwa na fedha ya akiba ambayo ikitokea fursa yoyote ya kiuwekezaji utatumia akiba hiyo kuipata fursa husika. Nimekuwa nikifanya hivyo toka mwaka 2017 na nimefanikisha kupata fursa nyingi ambazo kama nisingekuwa na akiba kwa ajili ya uwekezaji ningekosa fursa hizo. Mfano, mwaka 2018 nilipata viwanja 2 kwa bei ya kutupa ya milioni 3. Leo hii nikisema niuze kiwanja kimoja ni zaida ya milioni 5. Hayo ndio maajabu ya uwekezaji.
✍🏾Nasema maajabu kwa kuwa pesa inayowekezwa huwa inaongezeka thamani. Buku unayoiona leo ndogo ikikisanywa ndani ya muda maalum kwa nidhamu ya hali ya juu hakika haitakuwa buku tena bali yatakuwa ni maelfu. Hakikisha mwezi huu unaanza kuzikusanya buku kwa kujinyima kutoka kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
✍🏾Mwisho pata nafasi ya kutafakari juu ya kiwango cha pesa unachopata na namna unavyotumia pesa hizo. Gundua ni matumizi yapi ya pesa ambayo siyo ya lazima. Kokotoa thamani ya kila tumizi na pata jumla ya pesa yote ambayo unaweza kuitenga kila unapopata pesa kwa ajili ya kujilipa kwanza.
👉🏿Narudia tena, hakikisha umeweka ahadi dhidi ya nafsi yako kuwa mwezi Februari, 2020 ni mwezi wa mabadiliko kwako.
👐🏾Nakutakia kila la kheri katika siku hii leo.
Kupata nakala za uchambuzi wa vitabu mbalimbali BONYEZA HAPA
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias