NENO LA LEO (FEBRUARI 21, 2020): HAUWEZI KUCHAGUA UZALIWE KATIKA HALI GANI HILA UNAWEZA KUCHAGUA UFE KATIKA HALI FLANI

👉🏾Habari ya asubuhi hii ya leo rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii katika malengo uliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
👉🏾Kumbuka husisahau kutengeneza ushindi mdogo mdogo kila siku kwani kupitia ushindi huo unazidi kupiga hatua kuelekea kwenye kutimiza malengo makuu uliyojiwekea katika kila sekta ya maisha yako.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha kuwa maisha ya hapa Duniani ni mafupi na hakuna anayejua mwisho wake ni lini. Kutokana na fumbo hilo lilipo katika maisha yetu ndipo tunatakiwa kuchagua hatima ya maisha yetu iwe katika hali gani pindi mauti yatakapotufikia.

✍🏾Ni moja ya sheria ya asili ya uwili kinzani (Natural law of polarity) ambayo inatukumbusha kuwa kama kuna kuzaliwa pia kuna kufa. Kila mwanadamu anayeishi katika Dunia hii siku ikifika ni lazima aonje mauti. Pamoja na kwamba kifo kinaogepesha kwa kiumbe chochote chenye uhai lakini hakuna namna maisha yana mwisho wake.

✍🏾Hauwezi kuchagua uzaliwe katika hali gani kwani kama ingekuwa hivyo kila mtu angechagua kuzaliwa kwenye familia tajiri. Jambo moja ambalo una uwezo nalo katika maisha yako ni kuchagua hatima ya maisha yako iwe katika hali ipi ili hata mauti yakapowadia kwako uacha alama kwa kipindi ambacho umezawadiwa kuishi.

✍🏾Unawezaje kuacha alama jina lako? Mwandishi Robin Shama katika kitabu chake cha “The Greatness Guide” anatufundisha kuwa tunatakiwa kufa kila siku! Ndiyo, husiogope unatakiwa kufa kila siku. Tafsiri ya fundisho hili, mwandishi anatushirikisha kuwa kila siku unatakiwa kujiuliza swali moja “kama leo ingekuwa ni mwisho wa maisha yangu ni mambo yapi ambayo jamii ninayoiacha ingejivunia kwa kipindi kifupi cha maisha yangu”?.

✍🏾Swali hili linaambatana na tafakari ya kujiuliza maswali haya kila asubuhi: “kama siku ya leo ingekuwa ndiyo mwisho wa maisha yangu ni kipi ambacho ningefanya kukamilisha kusudi la maisha yangu hapa Duniani?, Kama ningepata nafasi ya kuishi siku zaidi ni mambo yapi ambayo ningefanya kwa ajili ya kuepuka maisha niliyofanya hapo awali? Je ni watu gani ambao ningepata muda wa kuishi zaidi ningependa wawe karibu yangu? Je ni watu wapi katika jamii inayonizunguka ningependa kupata muda kidogo kwa ajili ya kuomba msamaha makosa niliyowakosea?

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa maisha yetu hapa Duniani yana mwisho. Jambo linalowezekana leo hakikisha linafanyika leo badala ya kusema nitafanya kesho. Neno hili ilikuwa niandike mwanzoni mwa mwezi huu hila kila ilipokuwa inafika muda wa kuandika nilikuwa nalisogeza mbele. Hali hii ilitokana na ukweli kwamba kila mtu anaogopa kifo. Hila jana bahati mbaya nimeondokewa na rafiki yangu ambaye nilipopata taarifa za kifo chake sikuamini kabisa. Masikitiko hayo ndo yamenisukuma niwashirikishe neno hili kwa ajili ya kila mmoja wetu kuishi akitambua kuwa maisha yana mwisho hivyo husipende kuahirisha mambo.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(