👉🏿Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuianza siku hii ukiwa na hamasa ya kutosha katika kuendeleza bidii ya kuboresha maisha yako kupitia ushindi mdogo mdogo wa kila siku.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha zawadi ya kipekee ambayo mwanadamu amependelewa ukilinganisha na viumbe wengine. Baada ya kuumba ulimwengu na vitu vyote vilivyopo, kipekee Mwenyezi Mungu alisema na sasa tuumbe mtu kwa sura na mfano wetu. Kupitia maandiko matakatifu tunaona namna mwanadamu alivyoumbwa na kupuliziwa pumzi ya uzima na hatimaye kupewa mamlaka ya kutawala vitu vyote vilivyo chini na juu ya ardhi.
✍🏾Jambo la kwanza na kubwa la kujifunza kutoka kwenye maneno hayo katika maandiko matakatifu ni kwamba mwanadamu yoyote ambaye umeumbwa na kuishi katika Dunia hii umepewa mamlaka ya kutawala vitu vyote vilivyopo katika mazingira yanayokuzunguka. Kwa tafsiri hii kila mwanadamu ambaye anaishi katika Dunia hii ana mamlaka ya kutawala vitu vinavyomzunguka kwa faida yake na jamii inayomzunguka.
✍🏾Jambo la pili la kujifunza kutoka kwenye maandiko hayo matakatifu ni: mwanadamu umeumbwa na kupewa zawadi ya kipekee ambayo ni AKILI. Kupitia zawadi hii tunaona kuwa mwanadamu anaweza kutofautishwa na viumbe wengine waliopo Duniani.
✍🏾Akili ni nyenzo muhimu ambayo imemuwezesha mwanadamu kuwa na utashi wa maamuzi katika maisha yake ya kila siku. Unaweza kuamua kufanya au kutofanya jambo kutokana na maamuzi yako. Hicho kinachokusuma kufanya au kutokufanya ni akili ambayo kila mwanadamu amepewa tangu enzi za kuumbwa kwake.
✍🏾Hata hivyo, matumizi ya zawadi hii yanatofautiana kutoka binadamu mmoja hadi mwingine. Akili ambayo mwanadamu amepewa inauwezo wa kufanya kitu chochote kile hapa Duniani endapo itatumiwa kwa asilimia mia moja. Kutokana na viwango tofauti vya matumizi ya zawadi hii muhimu ndipo tunaanza kuona matabaka wa watu katika jamii.
✍🏾Matabaka haya yanajumuisha kundi la kwanza ambalo lina watu waliofanikiwa zaidi (wanatumia zawadi ya akili kwa kiwango cha juu sana). Kundi hili limeboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi kutokana na kazi za vichwa vyao. Fikiria kuhusu gunduzi mbalimbali ambazo zimefanikisha uwepo wa huduma kama vile usafiri, mawasiliano, afya na malazi.
✍🏾Kundi la pili linajumuisha tabaka la watu wenye mafanikio ya kawaida. Kundi hili linategemea kundi la kwanza na linatumia sehemu ya gunduzi za watu katika kuendelea kuiboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi.
✍🏾Kundi la tatu, linajumuisha watu ambao hawajafanikisha lolote katika maisha yao. Watu katika kundi hili hawasumbui vichwa vyao kwenye ni jinsi wanaweza kuboresha zaidi Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Kwa maana nyingine wamepewa talanta (akili) na kuificha chini ya ardhi hadi pale mwenye nayo atakapohitaji talanta yake.
✍🏾Mwisho, kutokana na neno la tafakari ya leo jiulize ni kwa namna gani unatumia zawadi ya kipekee ambayo umepewa na Muumba wako. Lenga kuwa kati ya watu wenye mafanikio makubwa ambao kupitia matumizi ya akili zao wamefanikisha kuendelea kuifanya Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw