👉🏾Habari ya leo mwanafamilia wa FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwaumeamka salama na upo tayari kukabiliana na majukumu yako ya siku hii ya leo ambayo yanalenga kukufikisha kwenye kusudi la maisha yako.
KUMBUKA UNAWEZA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA NA KUNDI LA WHATSAPP
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linatukumbusha umuhimu wa kulipa gharama kwa ajili ya kufikia kusudi la maisha yako. Kila mwanadamu ameumbwa na kuweka hapa Duniani ili akamilishe kusudi maalum. Wengi wameshindwa kufikia kusudi la maisha yao kwa kuwa hawakujibidisha kuweka malengo yanayolenga kuendeleza kila sekta ya maisha yao.
✍🏾Kipekee neno la leo linatukumbusha kuwa chochote unachotamani kufanikisha katika maisha yako ni lazima ujiulize ni gharama zipi ambazo unatakiwa kulipia. Na hapa namaanisha kulipa gharama katika mfumo wa rasilimali fedha. Ili utimize malengo yanayokuwezesha kufikia kusudi la maisha yako unatahitaji kujiuliza ni gharama zipi unatakiwa kulipia katika kila hatua unayopiga kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.
✍🏾Wengi huwa wanashindwa kulipia gharama kwa kudhani kuwa kufanya hivyo wanapoteza lakini ukweli ni kwamba katika kila lengo ulilonalo ni lazima ujiulize ni gharama zipi unatakiwa kulipia ili kufikia lengo hilo.
✍🏾Kuna gharama unatakiwa kulipia kwa ajili ya kuwekeza kwenye elimu ya mafanikio, mfano, unahitaji kusoma vitabu mbalimbali, unahitaji kusoma makala, unahitaji kulipia semina mbalimbali, unahitaji kulipia ushauri wa kifedha au kujifunza kozi maalum kuhusiana na uwekezaji au uendeshaji wa biashara. Zote hizo ni gharama ambazo zinalenga kukuendeleza katika kupanua maarifa yako kwenye hatua mbalimbali za kufikia kusudi la maisha yako.
✍🏾Hata hivyo, katika kila gharama unayolipia kabla ya kufanya hivyo ni lazima ujiridhishe kuwa utapata thamani halisi kwenye kile unacholipia. Maisha yanaendeshwa kwa mfumo wa kubadilishana thamani ya kitu kimoja na kingine. Enzi za zamani ilikuwa ni kubadilishana bidhaa kwa bidhaa lakini katika karne ya sasa biashara inaendeshwa kwa kubadilishana thamani ya fedha na thamani ya bidhaa/huduma.
✍🏾Mwisho namalizia kwa kukumbusha kuwa unapolipa gharama kwa ajili ya huduma au bidhaa husione kuwa umepoteza bali tambua kuwa ni sehemu ya wajibu wako katika kufikia kusudi kuu la maisha yako. Pia, kumbuka kuwa kipimo cha maendeleo ya mwanadamu kinaanzia kwenye maendeleo ya ubongo wake. Hivyo, kubali kuboresha ubongo wako ili ufikie kusudi la maisha yako.
👐🏾Nakutakia kila la kheri katika siku hii ya leo.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Kupata mafundisho haya kila siku jiunge kwenye kundi langu la Wahtsapp kupitia link hapa chini.
Karibu kwenye kundi la Fikra za Kitajiri upate elimu ya mafanikio kwenye kila sekta ya maisha yako.