NENO LA LEO (FEBRUARI 24, 2020): KUBALI KUWA KILICHOFANYIKA KIMEFANYIKA – SONGA MBELE NA YALIYOPO

👉🏾Habari rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kuianza vyema siku ya kwanza katika wiki ya mwisho wa mwezi Februari, 2020. Ni wiki ambayo unatakiwa kufanya tathimini juu ya hatua unazopiga katika kutimiza malengo uliyojiwekea kwenye kipindi hiki cha mwaka 2020. Ni wiki ya kuweka mikakati ili unapouanza mwezi Marchi husirudie makosa ambayo umegundu umefanya katika kipindi hiki cha miezi miwili iliyoisha.


HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linaendelea kutukumbusha wajibu wa kutopoteza muda kutokana na matendo yako yaliyopita. Kuna nyakati ambazo unajikuta katika hali ya kutopendezwa na matokeo ya maamuzi ambayo yamepelekea kutenda jambo ambalo lipo kinyume na matarajio yako.

✍🏾Zipo nyakati ambazo utajikuta unasikitika kwa kupoteza fedha zako kwenye uwekezaji ambao haujazalisha faida kama ulivyotarajia. Pengine mradi uliokusudia kuwa utatengeneza faida kubwa umekuwa sehemu ya kupoteza fedha zako ambazo umekusanya kwa kipindi kirefu au umekopa sehemu.

✍🏾Zipo nyakati ambazo utajikuta upo kwenye huzuni kubwa kutokana na matukio ambayo yapo nje ya uwezo wako. Pengine umepoteza fedha zako kutokana na kuibiwa au rasilimali zako kupotea kutokana na majanga ya kimazingira kama vile mafuriko, wadudu waharibifu au ukame.

✍🏾Zipo nyakati ambazo huzuni na hofu kubwa itatawala kutokana na matukio kama vile magonjwa, vifo vya wapendwa wako au kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki kutokana na matakwa yao wenyewe kutokana na kuishi kwako misingi na kanuni za mafanikio zinazoenda kinyume na mahitaji yao.

✍🏾Neno la tafakari ya leo linakukumbusha kuwa katika nyakati kama hizo unatakiwa kusimama imara na kurudisha nguvu kubwa ambayo itakuwezesha kukusukuma kusonga mbele. Husikubali kusimama na pengine kurudi katika maisha yako ya awali ambayo ulishajiwekea mikakati ya kuachana nayo na kuishi maisha mapya yenye misingi na kanuni za mafanikio.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunakumbushwa umuhimu wa kutopoteza muda pamoja na dira kuu ya maendeleo ya maisha yetu hata kama tutayumbishwa na mawimbi ya Dunia hii. Neno hili linatukumbusha kuwa sio kila mara tutapata matokeo yanayoendana na matarajio yetu. Kama kuna nyakati za kupanda tunatakiwa kutarajia pia kuwa nyakati za kushuka zipo.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(