NENO LA LEO (FEBRUARI 18, 2020): HAPA NDIPO UNATAKIWA KUIANZIA SAFARI YAKO YA UTAJIRI.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kuendeleza jitihada za kuboresha maisha yako. Safari hii ambayo umeianzisha inahitaji nidhamu, bidii na ubunifu katika kila siku ya unayojaliwa kuishi pasipo kukata tamaa. Wengi wameanza safari hii nakujikuta wanakata tamaa njiani.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha sehemu ambayo unatakiwa kuanza kuwekeza kwa nguvu za kutosha kabla ya kuianza safari yako. Sehemu hii si nyingine bali ni kuwekeza kwenye chakula cha ubongo wako. Kama ulivyo mwili wako kwa ujumla jinsi unavyohitaji chakula kwa ajili ya kupata nguvu, ubungo wako unahitaji maarifa sahihi kila mara kwa ajili ya kujiendeleza katika kila sekta ya maisha yako.

✍🏾Mwandishi Yuval Noah Harari katika kitabu chake cha “A Brief History of Humankind” anaelezea jinsi mwanadamu aliyoendelea kutoka kwenye kipindi cha kuyategemea mazingira hadi kufikia kipindi cha kujitegemea mwenyewe. Katika kipindi cha kutegemea mazingira binadamu aliishi sawa na wanyama wengine akiyategemea mazingira pasipo yeye kujishughulisha.

✍🏾Kadri nyakati zilivyopita ndivyo ubongo wa mwanadamu uliboreshwa kupitia vinasaba na hivyo kulithisha jeni (genes) zilizoboresha kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Vizazi vipya viliendelea kulithi jeni zenye tabia bora na hatimaye kufanikisha maisha ya mwanadamu yenye ubunifu unaoendana uboreshaji wa mazingira anayoishi.

✍🏾Ni historia hii fupi ya maendeleo ya mwanadamu tunaona jinsi ambavyo mwanadamu aliweza kuwekeza kwenye ubongo kiasi ambacho amefanikiwa kuachana na kutegemea mazingira na badala yake ameweza kutawala mazingira hayo kwa kuyaboresha kizazi hadi kizazi.

✍🏾Kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa kama hauwekezi kwenye ubongo akili yako itaendelea kuwa ile ile siku nenda rudi. Matokeo yake ni kwamba akili goi goi italithishwa ndani ya kizazi chako. Mwisho wako ndipo tunaanza kusikia kauli kama vile ukoo wetu huwa hatuwezi kuwa matajiri. Utajiri ni kwa familia chache zilizobahatika n.k.

✍🏾“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” – Ni kauli ambayo tunaipata kutoka kwenye maandiko matakatifu ambayo inaonesha umuhimu wa kuwekeza kwenye ubongo kwa ajili ya kuyatawala mazingira yanayokuzunguka kwa faida yako na kizazi chako.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nakukumbusha umuhimu wa kuwekeza kwenye kutafuta maarifa sahihi yanayolenga kuboresha kila sekta ya maisha yako. Unahitaji kusoma vitabu, unahitaji kushiriki semina mbambali, unahitaji kuwa kwenye makundi maalum ya kijamii ambayo yanalenga kukuza maarifa yako. Hakika Elimu, Elimu, Elimu, Elimu, Elimu ndio mkombozi wako wa kifikra na kiakili.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN - DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(