NENO LA LEO (FEBRUARI 13, 2020): FAHAMU NAMNA AMBAVYO UMEKUWA UKIJIDHURUMU MWENYEWE KWA KUSHINDWA KUSEMA HAPANA

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kundeleza bidii za kuboresha maisha yako katika siku hii ya leo. Kumbuka kuwa kadri unavyoweka jitihada kila siku ndivyo unafanikisha ushindi mdogo mdogo ambao kwa pamoja unakamilisha lengo lako kuu.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kukumbusha kwenye moja ya muhimili wa nidhamu binafsi katika kufanikisha kusudi la maisha yako. Kupitia neno la tafakari ya leo tutaona nguvu iliyopo kwenye neno HAPANA katika kuendeleza kasi ya mafanikio.

✍🏾Matumizi ya maneno HAPANA au NDIYO ni moja ya matumizi ya sheria za asili za uwili kinzani. Kupitia sheria hii ya uwili kindhani inafanya kazi kwa kuzingatia kuwa kati ya vitu viwili vilivyopo kuna nafasi ya kitu kimoja kupata nafasi ya kujidhihirisha na kitu kingine kutopewa nafasi. Tafsiri rahisi ni kwamba katika vitu viwili una nafasi ya kuchagua kitu kimoja na kuachana na kitu kingine.

✍🏾Hivyo mara unaposema NDIYO kwenye tukio ambalo siyo la muhimu katika maisha yako unakuwa umesema HAPANA kwa tukio la muhimu katika maisha yako. Watu NDIYO kwenye kila tukio huwa maisha yao yanaishia kuwa ya kawaida, kwa maana hawafanikishi chochote chenye thamani katika maisha.

✍🏾Kuna thamani kubwa ya kusema HAPANA kwa marafiki ambao wanabeza mipango yako; sema HAPANA kwa marafiki ambao wanapenda kuongelea maisha ya watu kuliko maisha yao wenyewe; sema HAPANA kwa rafiki au mfanyakazi mwenzako ambaye mara zote anawaza maisha katika upande hasi kuliko upande chanya; sema HAPANA kwa rafiki au ndugu ambaye anacheka ndoto ulizonazo na anakuona kama vile hauwezi kufanikisha lolote katika maisha au sema HAPANA kwa tukio lolote la kijamii ambalo linaenda kinyume na kanuni zako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia namna ambavyo tumekuwa tukipoteza fursa nyingi kutokana na kusema NDIYO kwenye matukio yasiyo na tija katika maisha yetu. Hata hivyo, ili ufakiwe kusema HAPANA kwa watu wanaokuzunguka ni lazima uwe na vipaumbele vya maisha yako. Ni lazima uwe na malengo ya maisha yako au utambue kusudi la maisha yako. Kwa ufupi ni kwamba ni lazima ujitambue wewe ni nani na unataka kufanikisha nini katika maisha yako yajayo.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(