NENO LA LEO (FEBRUARI 12, 2020): HIVI NDIVYO UMEKUWA UKIJICHELEWESHA MWENYEWE?

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongerakwa siku hii ya leo ambapo naamini ni siku muhimu kwako katika kuendeleza moto wa kufikia uhuri wa kifedha unaoutamani katika maisha yako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linaendelea kukufunulia misingi muhimu katika kufanikisha maisha ya utajiri wa ndoto zako. Kupitia neno la leo tutaangalia namna ambavyo umekuwa ukisita kuchukua hatua kwa kusubilia ukamilifu wa asilimia zote ambao hata hivyo huwa hautokei katika maisha ya mwanadamu wa kawaida.

✍🏾Kuna ugonjwa unaitwa KUAIRISHA kwa lugha ya wenzetu ni PROCRASTINATION. Ugonjwa huu ni hatari na ndio unasababisha watu wengi kuendelea na maisha yao ya kawaida kwa maana wanashindwa kupiga hatua kila mara. Dalili za ugonjwa huu ni muhusika muda wote kuona hajajikamilisha kuchukua hatua kwenye malengo anayojiwekea. Ugonjwa huu unamfanya muhusika aone kuwa kuna nyakati bora huko mbeleni na nyakati hizo zikifika ndipo atachukua hatua.

✍🏾 Huu ugonjwa umewazuia maelfu ya watu kubadilisha maisha yao na pengine hata wewe unayesoma makala hii ni mmoja wao bila ya kujijua kuwa unakabiliwa na adui huyo wa maendeleo. Kutaka kujua kama na wewe ni mmoja wa waathirika wa ugonjwa huu jiulize mwaka huu ulilenga kukamilisha nini na hadi sasa umetekeleza nini. Naamini wengi bado wanaona kuwa ni mapema mno kuanza kutekeleza malengo ya mwaka huu kwa kuzingatia mwezi Januari huwa unaambatana na mambo mengi yanayohitaji fedha. Hivyo, wengi wanaamini kuwa miezi ijayo itakuwa bora kuliko sasa. Hii dalili moja wapo ya ugonjwa huu.

✍🏾Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni kusubilia kujipanga na kujikamilisha kwa asilimia mia ndipo uchukue hatua. Hii ni hatari kwa kuwa kanuni ni kwamba ni lazima uwe tayari kuchukua hatua kuanzia kwenye asilimia ndogo uliyonayo. Ukipata asilimia 50 ya mahitaji muhimu inatosha kuchukua hatua. Watu wengi waliofanikiwa wanaamini kuwa hakuna wakati ulio bora zaidi ya sasa. Kutokana na imani hiyo wanajibidisha kuchukua hatua bila kujali mapungufu waliyonayo kwa wakati huo.

✍🏾Kadri wanavyochukua hatua wanajifunza na kutokana na changamoto na hatimaye wanaendelea kuboresha kile wanachofanya. Kumbe, unachotakiwa kufanya ni kuanza sasa. Achana na tabia ya kusogeza mambo na badala yake anza kuchukua hatua sasa. HAKUNA KESHO ILIYO BORA ZAIDI YA SASA.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limekufunulia namna ambavyo umekuwa ukisita kuchukua hatua kusubiria nyakati zilizo bora zaida ya sasa. Kuanzia jenga imani mpya ya kuwa unaweza kuanza kidogo huku ukiwa na fikra pana ya kule unakotaka kufikia.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155 au 0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(