NENO LA LEO (FEBRUARI 26, 2020): Roho inataka lakini Mwili ni dhahifu.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Siku hii ni kati ya zawadi za kipekee ambazo unaendelea kuzawadiwa kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kuyaishi maisha ya ndoto zako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo naendelea kukushirikisha umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kufikia kilele cha malengo yako. Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia nguvu ya roho ikilinganishwa na nguvu ya mwili. Kila mwanadamu ambaye ameumbwa amepewa vitu hivi viwili (roho na mwili).

✍🏾Pamoja na kwamba kila mwanadamu amepewa roho na mwili, vitu hivi vinafanya kazi kwa kutofautiana. Mara zote roho ipo upande wa mema kwa mhusika, roho inataka ukamilifu vitu kwa asilimia zote. Roho inataka kila kinachofanyika kifanyike kwa mafanikio makubwa sana. Roho inataka uwajibikaji na utekelezaji wa shughuli kwa viwango vya hali ya juu. Roho inataka kuepuka dhambi zote na kuwa upande wa matendo mema kwa jamii.

✍🏾Hata hivyo, pamoja na kwamba roho ipo upande wa mema haiwezi kukamilisha mambo yote yaliyopo ndani ya matamanio yake bila kushirikisha mwili. Kwa ufupi ni kwamba roho inatamani lakini haiwezi kufanya kazi bila ya mwili kuhusika. Mwili ndo unatakiwa kupokea maagizo kutoka kwa roho na kuyabadilisha kutoka kwenye matamanio au ndoto kuja kwenye uhalisia wake. Kumbe, Mwili kwa mwanadamu ndio unahusika na utekelezaji wa matamanio ya roho na bila kuwa na utayari mhusika ataendelea kuwa na ndoto au matamanio ambayo hayatekelezeki.

✍🏾Tunajifunza nini katika neno hili kuhusu roho na mwili wako? Somo kubwa la kujifunza ni kwamba katika maisha ya kila siku, mwili huwa unapenda kustarehe kwa maana haupendi maumivu au mateso ya aina yoyote ile. Unapenda kupumzika na sikujihusisha na kazi; unapenda kunywa/kula vitu vizuri; unapenda kuepukana na kazi ngumu; unapenda kulala kwa ajili ya kupata joto na kuepukana na baridi ya asubuhi; unapenda kukimbilia dhambi za kuliko matendo mema na mengine mengi. Haya ndio madhaifu ya mwili ambayo yanadumuza watu wengi kuchukua hatua dhidi ya matamanio ya roho zao.

✍🏾Mwisho kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa kama unahitaji kupata matokeo makubwa dhidi ya matamanio au ndoto za maisha yako ni lazima roho na mwili wako vifanye kazi kama timu moja. Roho inatakiwa kutoa maagizo kwa mwili ili mwili uitikie maagizo hayo na kuyafanyia kazi. Hakuna namna nyingine au njia ya mkato zaidi ya nguvu hizi mbili kusikilizana na kuwa kitu kimoja.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(