NENO LA LEO (FEBRUARI 23, 2020): IFANYE TABIA HII KUWA SEHEMU YA TABIA ZILIZOPENDWA KWAKO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambayo ni siku ya mwisho katika wiki hii. Siku zinasogea na wajibu wetu kila tunapoianza siku mpya ni kujiuliza kama kweli bidii tunazofanya kila siku kama zinatusogeza kwenye ukamilifu wa malengo tuliyojiwekea.


HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha wajibu wetu katika kutunza muda. Uwepo wetu hapa Duniani una muda maalum hivyo kila sekunde tunayoishi inapunguza kwenye muda tuliyoandikiwa kuishi. Swali la msingi n kujiuliza unautumia vipi muda wa thamani ambao unazawadiwa katika kila siku ya maisha yako?

✍🏾Kupitia neno la tafakari ya leo nitakushirikisha tabia moja ambayo unatakiwa kuachana nayo kwa ajili ya kuokoa muda mwingi ambao umekuwa ukipoteza kutokana na tabia hiyo. Imani yangu kwa kila mmoja ndani ya kundi hili anamiliki TV au Kompyuta mpakato au Simu janja au vyote kwa pamoja. Vifaa hivi vimekuwa sehemu ya kuendeleza tabia ya kupoteza muda wetu wa thamani kutokana na kuwa na ratiba ya kuangalia vipindi maalumu, filamu (movies) au tamthilia.

✍🏾Katika jamii inayotuzunguka naendelea kushuhudia watu ambao wanatumia muda mwingi kukaa nyumbani na kuangalia TV kiasi ambacho wana ratiba ya vipindi mbalimbali kwenye kila Chaneli. Katika jamii hii hii naendelea kushuhudia watu ambao bado wana muda kukaa chini masaa kazaa kwa ajili ya kuangalia filamu ambazo zimeigizwa kama mfuatano wa matukio (series).

✍🏾Ni katika jamii naendelea kusikitika ninapoona kuwa kuna watu ambao wanakuwa na urahibu/uteja (urahibu) na filamu zinazoendeshwa na TV mbalimbali kwa lengo la kuvuta hisia zao hasa katika matangazo ya biashara bila ya wao kujitambua. Hii ni hatari kwa maendeleo ya mtu ambaye bado anaendekeza tabia hii.

✍🏾Nasema ni hatari kutokana na ukweli kwamba muda unaopoteza kwa ajili ya kuangalia TV au filamu ungeutumia kufanya jambo la maana kama vile kusoma kitabu, kufanya mazoezi, kuanzisha majukumu ya ziada nje ya kazi za mwajiri wako au kukaa karibu na familia yako.

✍🏾Kwa nini watu wanaangalia TV au filamu/tamthilia kwenye kompyuta au simu janja? Majibu yanayopatikana kutoka kwenye jamii ni yanajumuisha; wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata habari, kujifunza au kupumzika baada ya majukumu magumu ya siku nzima. Swali la msingi ni je wanachojifunza kinaendana na uhalisia wa maisha? Kwa maana maudhui yaliyopo kwenye filamu yanaendana na ukweli wa maisha au tamaduni zetu?

✍🏾Ukisoma taarifa za watu waliofanikiwa kimaisha utakuta hawana utaratibu wa namna hii ya kujifunza au kupata habari mpya. Kama anahitaji kujifunza kitu atasoma kitabu, makala, ripoti za kitafiti au kama atahitaji kupata habari anakuwa na ratiba ya kupata habari mpya kupitia magazeti, tovuti au mitandao ya kijamii. Huu unakuwa ni utaratibu wa kila siku ndani ya ratiba yake ya siku. 

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo naomba ujifanyie tathimini ya muda ambao umekuwa ukipoteza kutokana na tabia ya kuangalia TV au filamu mbalimbali. Baada ya tathimini hiyo ujiulize kama kweli kila unachojifunza kutokana na tabia hiyo kama kina faida katika maisha yako.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(