NENO LA LEO (FEBRUARI 17, 2020): HUYU NDIYE MTU PEKEE ANAYEKUKWAMISHA

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Mungu ni mwema kiasi ambacho ametuzawadia siku hii ya Jumatatu kwa ajili ya kuendeleza jitihada za kuisha maisha ya thamani. Hongera rafiki yangu kwa zawadi ya hii ambayo naamini utaitumia vyema kwa ajili kuwa na wiki iliyo bora.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha moja ya msingi muhimu katika kufikia mafanikio tunayotamani. Imekuwa kawaida kuwa katika maeneo tunayoishi kuona watu wanalalamikia Serikali, wazazi au mazingira yanayowazunguka kama sababu kuu inayowazuia kufanikiwa.

✍🏾Hata hivyo, katika jamii hiyo, serikali ile ile, wazazi wa sifa zile zile au mazingira yale yale utakutana na Vijana ambao wamefanikiwa kupiga hatua kimaendeleo ikilinganishwa na wanaolalamika. Kumbe kinachomzuia mtu kufikia malengo yake si mfumo wala wazazi au mazingira yanayomzunguka bali yeye mwenyewe.

✍🏾Ndiyo naamanisha wewe mwenyewe ndo mtu unayejikwamisha mwenyewe kutokana na maamuzi ambayo umekuwa ukifanya katika maisha yako ya kila siku. Hali uliyonayo kwa sasa ni matokeo ya fikra/mawazo, tabia na mazoea ambavyo vyote kwa pamoja vinapelekea maamuzi yako katika maisha ya kila siku.

✍🏾Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu na kumpa akili ambayo inamtofautisha na viumbe wengine. Kutokana na kiwango cha matumizi ya akili hiyo ndipo tunaona makundi tofauti ya wanadamu kulingana na mafanikio yao.

✍🏾Kutokana na tafakari ya leo, unatakiwa kufahamu kuwa mafanikio ya aina yoyote unayoyataka yapo ndani ya uwezo wako. Achana na fikra potofu au mawazo finyu ambayo yanapelekea ujione kuwa wewe ni fungu la kukosa na mafanikio ni kwa watu wachache.

✍🏾Mwisho, nakukumbusha kuwa mtu pekee anayeweza kukuzuia kufikia mafanikio unayotamani katika maisha yako ni wewe mwenyewe. Ishinde hiyo sauti ya ndani inayokuambia kuwa muda wa kuchukua hatua bado. Ishinde sauti hiyo ya ndani ambayo kila mara inakufanya uwe na hofu ya kuchuku hatua. Ishinde sauti hiyo ya ndani ambayo inakuambia kuwa mafanikio ni kwa wateule wachache waliobahatika.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(