👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kundeleza bidii za kuboresha maisha yako katika hii ambayo wengi wamejipanga kutumia sehemu ya akiba yao kusherekea siku ya wapendanao. Hakikisha haupotezi kusudi kuu la maisha yako kutokana na mawimbi au dhoruba iliyopo njiani.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kukumbusha kuepuka kupoteza fedha zetu kutokana na mihemko ya matukio yaliyowekwa na watangulizi wetu kwa maslahi au matakwa yao. Siku ya leo maeneo mengi Duniani watu wanasherkea siku ya wapendanao (Valentine Day).
✍🏾Maazimisho haya yanaambatana na mila, jadi au imani mbalimbali. Mfano, sehemu nyingi leo tutashuhudia rangi nyekundu kama vile nguo au maua ya kila aina. Mbaya zaidi sherehe hizi zinaambatana na matumizi ya fedha yaliyopitiliza huku matendo ya kishetani nayo yakishamiri.
✍🏾Leo hii mida ya jioni mitaa na kumbi za starehe zitapambwa hamsha hamsha za hapa na pale ambazo zote kwa pamoja zinatumia sehemu ya akiba ya fedha za wahusika. Sina hakika kama waanzilishi wa siku hii walikuwa na kusudio kama hili.
✍🏾Sherehe zote zinazoadhimishwa na wanadamu zimekuwa zikiambatana na matumizi makubwa ya fedha kiasi ambacho watu wanabaki mifuko wazi. Akiba zote zinatumika kwenye matumizi yasiyo ya lazima kiasi ambacho wahusika wanaanza upya. Ndio maana kutokana na sherehe za mwezi Desemba na mwaka mpya, mwezi Januari unaonekana kuwa mwezi ambao watu wengi wanakuwa juu ya mawe.
✍🏾Hii ni tabia mbaya kwa mtu ambaye anajua kanuni na misingi ya maisha yake hasa kwenye matumizi sahihi ya pesa. Badala ya kuendeshwa na matukio ya mwanadamu unatakiwa kujiendesha mwenyewe. Mfanye kila mtu aliyepo karibu yako atambue kuwa unaendeshwa na misingi uliyojiwekea mwenyewe na sikuendeshwa na matukio ya ulimbukeni.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo unatakiwa kufahamu kuwa kila siku una nafasi kutimiza upendo wako kwa wapendwa wanaokutegemea kuwapa upendo. Nenda kinyume na matukio ya wanadamu kwa kukamilisha matukio ya upendo kila siku kwa kadri uwezavyo.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw