👉🏾Habari ya leo mwanafamilia wa FIKRA ZA KITAJIRI. Ni furaha yangu kuona umeamka salama ukiwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kufikia kwenye matamanio ya maisha yako. Hilo linatakiwa kuwa jukumu la kila siku, kwa maana ya kuhakikisha kila unachokifanya kila siku kiwe kinachangia kukusogeza hatua moja mbele katika safari ya kufikia mafanikio ya ndoto yako.
KUMBUKA UNAWEZA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA NA KUNDI LA WHATSAPP
✍🏾Siri hii si nyingine bali ni "ili uwe tajiri ni lazima uwekeze kwenye kitega uchumi na baada ya kuwekeza kwenye kitega uchumi hicho kisimamie kirudishe hela uliyowekeza". Siri haiishii hapo bali baada ya kurudisha pesa uliyowekeza unapaswa kuwekeza kwenye kitega uchumi kingine na chenyewe kisimamie kirudiashe pesa uliyowekeza. Endelea na mzunguko huo hadi pale ambapo hakutakuwa na kikwazo wala mtu wa kukusimamisha kwenye njia uliyochagua.
✍🏾Hii ni siri ambayo inaonekana ni ndogo sana kwa maneno lakini hakika ukiitumia itabadilisha maisha yako kiasi ambacho hautoamini. Niliwahi kuandika katika makala zangu kuwa kutegemea chanzo kimoja cha kipato ni utumwa. Siri hii inakukumbusha umuhimu wa kuhakikisha unaanzisha vitega uchumi vingi kwa ajili ya kukuza utajiri wako.
✍🏾Siri hii pia inatukumbusha umuhimu wa kuwa na usimamizi mzuri kwenye vitega uchumi tunavyoanzisha. Watu wengi wanaanzisha vitega uchumi ambavyo havirejeshi kiasi cha pesa iliyowekezwa. Matokeo yake ni kwamba badala ya kitega uchumi kuwa chanzo cha kuongeza kipato kinakuwa sehemu ya kuendelea kutumia kiasi kidogo cha pesa ulichonacho.
✍🏾Mwisho siri hii inatukumbusha umuhimu wa kutumia vizuri faida inayozalishwa kutoka kwenye vitega uchumi tulivyonavyo kwa ajili ya kuendelea kuanzisha vitega uchumi vipya. Hapa ndipo utaona maendeleo halisi katika maisha kwa kuwa kila mara utakuwa unakua kutokana na vyanzo vipya vya mapato.
👐🏾Nakutakia kila la kheri katika siku hii ya leo.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 763745451/0786881155
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 763745451/0786881155
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw