NENO LA LEO (FEBRUARI 29, 2020): TANGULIZA THAMANI NA PESA ZITAKUFUATA

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hakika Mwenyezi Mungu amekuwa mwema kwetu kiasi ambacho muda kama huu tunaweza kuandika na kusoma neno la tafakari ya leo. Leo hii tunasema kwa kheri Fubruari, 2020 tukiwa na hamu ya kuikaribisha Machi, 2020 ili tuendeleze moto ya kufanikisha malengo makuu tuliyojiwekea katika maisha yetu kwa kipindi hiki cha mwaka 2020.
.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha siri muhimu unayotakiwa kuitumia kwa ajili ya kutengeneza pesa na hivyo kukuza uchumi wako. Pesa imekuwepo tangu ilipozinduliwa na ikawezesha kuwa msingi wa kufanikiza mauzo na manunuzi katika Jamii. Kumbuka kuwa, kabla ya ugunduzi wa pesa mauzo na manunuzi (biashara) yalikuwa yakifanyika kwa kubadilishana bidhaa na bidhaa au bidhaa kwa huduma au huduma kwa huduma.
.
✍🏾Baada ya pesa kugunduliwa, msingi wa biashara (mauzo/kununua) ulibadilika kabisa kiasi ambacho hauwezi kununua kama hauna pesa. Pesa ilibadilisha mtazamo wa Jamii kiasi ambacho mwenye pesa nyingi akawa na nguvu ya kuliteka soko kutokana na bidhaa anazozalisha au huduma anazotoa. Toka enzi hizo hadi sasa hapajatokea uvumbuzi wa kubadilisha thamani ya pesa kama msingi mkuu wa kuwezesha biashara katika Jamii.
.
✍🏾Hauwezi kununua kama hauna pesa na hauwezi kupata huduma unayotaka kama hauna pesa. Pesa imekuwa kipimo cha utajiri na imekuwa chanzo cha kulazimisha watu kufanya kazi. Utapata pesa kutokana na bidii na weledi wako katika kazi. Utajiri wako utapimwa kutokana na mali unazomiliki na mali hizo ni lazima zithaminishwe katika kipimo cha pesa. Hakuna namna kila mtu kwenye jamii nahitaji kuwa na pesa japo pesa imekuwa adimu kiasi ambacho haipo tayari kupatikana kama hujui njia zake!
.
✍🏾 Je ni fanye nini ili nipate pesa nyingi? Hili ni swali la msingi ambalo kila mtu kwenye Jamii anahitaji majibu yake na kupitia tafakari ya leo nakushirikisha jibu sahihi la kupata pesa. Jibu la kupata pesa si jingine bali ni “Hakuna muujiza wowote wa kupata pesa zaidi ya kuwa mtu wa thamani kwa Jamii”. Jamii inasubiria tunu ya thamani iliyopo ndani mwako itumike kwa ajili ya kuifaidisha na kutokana thamani hiyo Jamii ipo tayari kukuzawadia mapesa.
.
✍🏾 Je nawezaje kuwa mtu wa thamani kwa Jamii? Ni ukweli mtupu kuwa “Pesa zipo kwa watu ndani ya Jamii hii tunayoishi” na ili upate pesa hiyo ni lazima ujue jamii inataka thamani ya aina gani kutoka kwako. Jibu lipo wazi kuwa katika mfumo wa biashara ambao ndiyo msingi mkuu wa upatikanaji wa pesa ni lazima pawepo bidhaa/huduma ambayo inathaminishwa kwa thamani ya kiasi cha pesa. Tafsiri yake ni kwamba kama unahitaji kuwa mtu wa thamani kwa jamii inayokuzunguka ni lazima utambue jamii hiyo inakabiliwa na changamoto zipi.
.
✍🏾Baada ya kutambua changamoto zinazoikabili jamii, kazi iliyopo mbele yako ni kuhakikisha unatatua changamoto za jamii kupitia kazi au biashara yako. Kumbe, badala ya kulenga kupata fedha unatakiwa kulenga kutatua changamoto zilizopo katika jamii na kupitia utatuzi wa changamoto pesa zitakufuata kwa kasi. Hata hivyo, kiwango cha pesa ambacho utapata kitategemeana na nguvu, ubunifu na weledi unaowekeza katika kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.
.
✍🏾Sijui kama naeleweka hapa. Ngoja nitumie mfano huu kuelezea ili wote tuwe kwenye uelewa mmoja. Bwana Doni (sio jina halisi) anatoa huduma ya kutibu magonjwa ya ngozi katika jamii. Hivyo, thamani ya bwana Doni katika jamii ni kutibu magonjwa ya ngozi kwa watu wenye matatizo hayo. Je Bw. Doni ili apate pesa nyingi anatakiwa kujitangaza vipi katika jamii? Ili Bw. Doni apate pesa nyingi anatakiwa kujitangaza kuwa: Mimi flani nawasaidia watu kuepukana na matatizo ya magonjwa ya ngozi.
.
✍🏾Hapa ndipo watu wengi wanakosea katika kutangaza thamani wanazotoa kwa jamii. Badala ya kutangaza thamani wanazotoa wanatangaza bidhaa huduma wanazouza. Hii ni sawa na kukutana na msichana kwa mara kwanza kabla hamjatongozana ukamtaka muoane. Jibu liko wazi kuwa hautaweza kufanikiwa kuoana nae kama kweli ni mtu anayejitambua. Ndivyo, ilivyo kwenye ulimwengu wa biashara badala ya kutangaza bidhaa unatakiwa kutangaza thamani unayotoa.
.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha kuwa ili upate pesa nyingi unatakiwa kujiuliza thamani yako ni ipi katika jamii inayokuzunguka. Hii ni pamoja na kufahamu pesa zako zipo sehemu gani katika jamii. Pesa zipo katika changamoto zinazoikabili jamii. Chagua changamoto ambayo unataka kuitatua na anza kutoa thamani kwanza kabla ya kutanguliza uhitaji wa pesa.
.
✍🏾Kupata mada hii kwa undani nunua uchambuzi wa vitabu 2 vinavyotoa elimu juu ya jinsi gani unaweza kufanya biashara yenye kutengeneza faida katika karne hii ya 21. Kitabu cha kwanza ni kutoka kwa Sabri Suby ambaye amekuwa ni Muuzaji mwenye njaa ya mauzo kuliko kijana yeyote katika karne ya sasa. Kitabu cha pili ni kutoka kwa Nil Eyal ambae pia anashirikisha namna kila mmoja wetu anatakiwa kuzalisha bidhaa ambazo zinamfanya mteja awe na ushirika na bidhaa/huduma zako. Uchambuzi wa vitabu vyote hivi unapatikana kwa Tshs. 20,000/= kila kimoja na ukinunua vyote utapata kwa bei ya Ofa ya Tshs. 15,000/=.
.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
.
 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 
.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(