👉🏾Hongera rafiki kwa kufikia siku hii ya mwisho katika mwezi Januari 2020.
👉🏿Hakika siku zinaenda kasi maana ni juzi tulisherekea mwaka mpya 2020 lakini leo hii ni mwaka huo huo ambao umebakiza miezi 11.
👉🏿Mategemeo yangu ni kwamba umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii za kuhakikisha siku zilizobaki katika mwaka huu zinakuwa zenye faida katika kuboresha maisha yako.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutumbusha malengo ambayo tumejiwekea katika mwaka huu.
✍🏾Katika jamii tunayoishi kila inapofika mwaka mpya utasikia maneno mengi kama vile "mwaka mpya na mambo mapya". Kauli hizi zinaonesha kuwa watu wengi wanahitaji mabadiliko kila wanapoingia mwaka mpya.
✍🏾 Wengi wanaweka malengo lukuki yanayolenga kubadilisha mazoea na tabia katika kipindi cha mwaka unaoisha ili mwaka unaofuatia uwe wa tofauti katika maisha yao.
✍🏾Tafsiri yake ni kwamba kila mtu anahitaji maisha bora. Maisha yenye mafanikio kwenye kila sekta na ndio maana kila mwaka watu wanalenga wabadilike kutoka kwenye maisha ya zamani na kuingia kwenye maisha mapya.
✍🏾Hata hivyo ukweli ni kwamba wengi wanahitaji mabadiliko lakini ambao wapo tayari kubadilika ni wachache.
✍🏾Wengi wanaweka malengo kila mwaka lakini kadri siku zinavyosegea wanajikuta wamerudi kwenye maisha yale yale waliyozoea. Kumbuka kuwa kama unahitaji mabadiliko ni lazima yaanzie ndani mwako.
✍🏾Tafakari jinsi ambavyo mwaka huu umejiwekea malengo na fanya tathimini inayolenga kupima mwenendo wako kuelekea kwenye ufanisi wa malengo hayo. Jiulize maswali yafuatayo:
👉🏿Januari umeondoka lakini umeniacha je?.
👉🏿Je umechukua hatua yoyote inayolenga kufikia malengo uliyojiwekea?
👉🏿Jiulize je kuna mabadiliko yoyote ya kitabia na mazoea ikilinganishwa na mwaka jana?.
👉🏿Jiulize je umeweka jitihada zozote zinazolenga kubadilisha maisha yako?
✍🏾Mwisho kama bado upo kama ulivyokuwa mwaka jana, hakika bado hujachelewa. Chukua hatua sasa maana Dunia inasubiri kuandika mema yako ambayo uliyafanya katika kipindi cha uhai wako.
👐🏾Nakutakia kila la kheri katika siku hii leo.