👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa siku umeianza vyema na upo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kupiga hatua katika kufikia malengo uliyojiwekea. Ni siku ya Jumamosi ambayo ni fursa kwako kufanya kazi za ziada kwa ubunifu ili uwe tofauti na wale ambao wanaichukulia siku hii kama siku ya mapumziko.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tunaenda kujifunza siri moja muhimu ya kukuwezesha kuuza bidhaa/huduma zako kwa kiwango kikubwa sana kuliko unavyofanya kwa sasa kama una biashara. Kabla ya kuzungumzia siri hii ningependa kila mmoja wetu afahamu kuwa hakuna namna utaweza kufikia utajiri wa ndoto yako kama hauna biashara.
✍🏾Biashara ni moja ya nyenzo muhimu ambayo itakuwezesha kukuza kipato chako hadi kufikia maisha yenye uhuru wa kifedha. Tafiti zinaonesha kuwa biashara nyingi zinazoanzishwa zinakufa katika kipindi cha miaka 5 ya awali toka kuanzishwa kwake. Hata biashara zile zinazoendelea zaidi ya kipindi hicho zinakuwa zinajiendesha kwa hasara kwa maana hazizalishi faida. Kumbuka kuwa uhai wa biashara ni kutengeneza faida.
✍🏾Je unajua ni kwa nini biashara hizo zinakufa ndani ya kipindi hicho? Jibu ni rahisi biashara nyingi zinaanzishwa na watu ambao wengi wao hawana taaluma ya misingi sahihi ya kuendesha biashara. Wengi wanaanzisha biashara kutokana na uzoefu wa kuangalia kwa ndugu, rafiki au jirani. Ni wachache sana ambao wanatambua kuwa biashara zina kanuni zake na moja ya kanuni muhimu ni kuendeleza uhai wa mzunguko wa pesa. Kiwango cha pesa inayoingia inatakiwa kuwa kubwa zaidi ya kile kinachotoka.
✍🏾Tafsiri yake ni kwamba ili biashara iendelee kutengeneza faida ni lazima mauzo yaendelee na idadi ya wateja iendelee kuongezeka. Mauzo ndio injini au uhai wa biashara yoyote ile. Waanzilishi wa biashara wengi huwa hapa ndipo wanakosea kwa kuwa hawajui siri moja muhimu ya mauzo ambayo nitakushirikisha katika makala hii.
✍🏾Je ungependa kufahamu ni siri ipi hiyo? Kama jibu ni ndiyo endelea kusoma makala hii. Siri ya mauzo ni kuepuka kutangaza bidhaa au huduma unazotoa na badala yake ukaanza kutangaza bidhaa au huduma hizo zinatatua changamoto gani katika jamii.
✍🏾Sijui kama umenielewa! Tunafanya biashara ya aina yoyote ile kwa ajili ya kutatua changamoto au matatizo yaliyopo kwenye jamii. Hivyo kabla ya kuanzisha biashara yoyote au kumshawishi mteja kununua bidhaa au huduma zako unatakiwa kumuonesha namna ambavyo bidhaa/huduma zako zitamsaidia kutatua changamoto au matatizo yake.
✍🏾Tafsiri yake ni kwamba unahitaji kwanza kumuonesha mteja tarajiwa thamani iliyopo katika bidhaa au huduma zako ikilinganishwa na matatizo yanayomkabili kwani matatizo hayo ndiyo msukumo wa yeye kuhitaji kununua bidhaa/huduma husika. Kumbe, unatakiwa kufahamu kuwa wateja wananunua kwa ajili ya kutatua matatizo au changamoto zinazowakabili. Wajibu wako kama muuzaji ni kuhakikisha unamuelimisha mteja ni kwa jinsi gani bidhaa au huduma zako zitakidhi hitaji lake.
✍🏾Hivyo ili ufanikiwe kukuza mauzo ya bidhaa/huduma zako unahitaji kuwa na programu maalumu ambayo inaendesha vipindi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wateja tarajiwa. Dunia ya karne hii imekuwa ni kijiji kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano. Hivyo, unatakiwa kutumia ukuaji wa teknolojia hii ya mawasiliano kwa ajili ya kuwa karibu na wateja tarajiwa wa bidhaa au huduma zako.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha umuhimu wa kufanya biashara kulingana na ukuaji wa teknolojia ya karne hii ya 21 na kuepuka kuendelea kufanya biashara kwa kutumia mbinu za kizamani. Kupata mada hii kwa undani nimekuandalia uchambuzi wa vitabu 2 vinavyotoa elimu juu ya jinsi gani unaweza kufanya biashara yenye kutengeneza faida katika karne hii ya 21.👇🏾
👉🏾Kitabu cha kwanza ni kutoka kwa Sabry Suby ambaye amekuwa ni Muuzaji mwenye njaa ya mauzo kuliko kijana yeyote katika karne ya sasa. Kitabu cha pili ni kutoka kwa Nil Eyal ambae pia anashirikisha namna kila mmoja wetu anatakiwa kuzalisha bidhaa ambazo zinamfanya mteja awe na ushirika nazo kwa kutengeneza tabia mpya katika maisha yake. Uchambuzi wa vitabu vyote hivi unapatikana kwa Tshs. 20,000/= kila kimoja na ukinunua vyote utapata kwa bei ya Ofa ya Tshs. 15,000/=.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw