Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na hupo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kuboresha maisha yako. Kumbuka kuwa lengo letu ni kuhifanya Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi kupitia kazi zetu na lengo hilo ni lazima lianzie katika kuishi maisha yenye kusudi maalum.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha umuhimu wa kuishi kama wewe na siyo kuishi kulingana na mahitaji ya jamii inayokuzunguka. Jamii tunayoishi kwa sasa inamejaa watu wengi wanaoishi kwa kuigiza maisha ya wengine katika jamii. Tunaigiza tabia, tunaigiza mwonekano wetu katika jamii, tunaigiza umiliki wa rasilimali za kila aina n.k.
Kwa ujumla maisha ya sasa hasa katika ulimwengu ambao tumeunganishwa Dunia imekuwa ni kijiji, maisha ya maigizo yanazidi kushika kasi. Katika hali kama hii tunatengeneza familia ambazo zimejaa maigizo na matokeo yake tutakuwa na taifa ambalo limejaa maigizo. Maisha haya ya maigizo mwisho wake hauwezi kuwa mzuri kutokana na ukweli kwamba maigizo na uhalisia wa mhusika katika mazingira yake na ndani ya nafsi yake ni vitu viwili tofauti.
Kama unahitaji kuishi maisha yenye furaha na mafanikio makubwa ni lazima ujitambue kwanza wewe ni nani, umeumbwa kwa ajili ya kufanikisha kusudi lipi katika maisha yako (tambua kusudi la maisha yako) na unatakiwa kufanya nini ili ukamilishe kusudi hilo katika kipindi chote cha maisha yako.
Mwisho, kupitia neno la tafakari leo tunafundishwa kuachana na tabia ya kuigiza maisha ya Jamii inayotuzunguka na kujenga misingi imara ya maisha yenye furaha. Na misingi hiyo ni lazima izingatie vitu vitatu ambavyo ni: (a) kuwa na kitu unachokiishi (something to live on) (b) kitu kinachokufanya uishi (something to live for) na (c) kitu ambacho upo tayari kufa kwa ajili yake (something to die for).
Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw