👉🏾Habari ya asubuhi rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kuendeleza jitihada zinazolenga kupata ushindi mdogo mdogo katika siku hii ya leo. Kumbuka kila unaposherekea ushindi mdogo kila siku ndani ya muda maalum unakuwa unapiga hatua kuelekea kilele cha mafanikio yako.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha fursa moja yenye fursa nyingi ndani yake kwa ajili ya kukuza utajiri wako au kukuwezesha kufikia uhuru wa kifedha unaotamani katika maisha yako. Sifa moja ya mjasiliamali ni muda wote kuwa macho katika kusoma na kutafsri mabadiliko yanayototekea katika jamii anayoishi.
✍🏾Historia ya maendeleo ya mwanadamu inaonesha namna ambavyo mwanadamu amepitia kwenye mabadiliko mbalimbali kutoka kwenye kipindi cha zama za mawe, mapinduzi ya kilimo, mapinduzi ya viwanda na sasa mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano. Kila kipindi kati ya vipindi hivi kiliambatana na ukuaji wa idadi ya watu kutokana na mazingira ya mwanadamu kuishi hapa Duniani kuendelea kuboreka kutoka kwenye hali duni.
✍🏾Ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu ndipo fursa kibao ambazo zinaendelea kutengeneza matajiri katika kila karne. Fursa ninayokushirikisha katika neno la tafakari ya leo ni ukuaji wa idadi ya watu ikilinganishwa na mahitaji ya chakula.
✍🏾Inahitaji kutumia dakika kadhaa kutafakari juu ya takwimu na makadirio ya idadi ya watu ikilinganishwa na mahitaji ya chakula. Mwaka 1961 wakati Tanzania inapata uhuru wake, idadi ya watu ilikuwa ni milioni 10.3 ikilinganishwa na milioni 59.7 mwishoni mwa mwaka 2020. Idadi hii ya watu inakadiriwa kufikia milioni 129.3 ifikapo mwaka 2050.
✍🏾Kwa takwimu hizo hizo, idadi ya watu Duniani mwishoni mwa mwaka 2020 inakadiriwa kufikia watu bilioni 8. Ifikapo 2050, idadi ya watu Duniani inakadiriwa itaongezeka hadi kufikia bilioni 9.2 sawa na ongezeko la watu bilioni 1.2 kwenye idadi ya mwaka huu.
✍🏾Ili watu hawa kupata chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya mwili, inakadiriwa uzalishaji wa chakula unatakiwa kuongezeka kwa asilimia 60 hadi 70 ikilinganishwa na uzalishaji wa sasa.
✍🏾Takwimu hizi zinatoa kiashiria kuwa kama unahitaji kuwa tajiri kutokana na ongezeko hilo la idadi ya watu ni lazima sekta ya kilimo na ufugaji uitazame kwa jicho la kipekee. Nasema sekta ya kilimo ya ufugaji kwa kuwa ndio sekta zinazoongoza kwa kuzalisha chakula kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya mwanadamu na wanyama.
✍🏾Sekta hizi kwa pamoja zina fursa nyingi ambazo ukizichangamkia zitakufanya uwe tajiri ndani ya muda ya mfupi kutokana na ukweli kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuishi bila kula, iwe masikini au tajiri ni lazima ule ili uendelee kuishi.
✍🏾Tafsiri yake ni kwamba kuanzia sasa unatakiwa kuanza kujiuliza juu ya sehemu zipi ndani ya sekta ya kilimo na mifugo ambazo unatakiwa kuwekeza kwa ajili ya kuongeza uzalishaji au usindikaji wa chakula ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa ongezeko la idadi ya watu.
✍🏾Fursa hii inaambatana na kuhakikisha unaanza kuwekeza kwenye ardhi kwa kuwa hautaweza kufanya uwekezaji wowote kwenye kilimo na mifugo bila ya kumiliki ardhi. Iwe ufugaji, kilimo au viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na mifugo vyote hivyo vinahitaji ardhi kwanza.
✍🏾Mwisho, kupitia tafakari ya leo nakusisitiza kuwa macho kwa mabadiliko yanayotokea katika maendeleo ya historia ya mwanadamu ili kufahamu ni kwa namna gani unaweza kutumia mabadiliko hayo kwa ajili ya kukuza utajiri wako. Ili ufanikishe azma hiyo ni lazima uwe mtu wa kujibidisha katika kutafuta maarifa mapya kila siku. Kuna mambo mengi yanaendelea kutokea ambayo ni fursa ya kukuza uchumi wako.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA - KUWA NA NDOTO KUBWA (SUCCESS IS YOUR BIRTH RIGHT - DREAM BIG)
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw