NENO LA LEO (FEBRUARI 11, 2020): UNAPOIANZA SAFARI YA KUELEKEA KWENYE UTAJIRI ANZA KWA KUJIULIZA UNAMILIKI NINI KWA SASA?

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa siku hii ya leo umeianza vyema na upo tayari kukabiliana na majukumu ya kila siku yanayolenga kukufikisha kwenye mafanikio ya ndoto ulizonazo kwenye kila sekta ya maisha yako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kuendelea kutufunulia mwanga kwa ajili ya kuongeza kasi ya kufikia matamanio ya uhuru wa kifedha katika maisha yetu. Neno la leo linatukumbusha umuhimu wa kujifanyia tathimini ya rasilimali ambazo kila mmoja anamiliki kwa sasa kabla ya kuanza kujiuliza unahitaji kuwa na nini ili ufikie uhuru wa kifedha unaotamani.

✍🏾Hapa ndipo watu wengi katika jamii yetu wanashindwa kuendeleza maisha yao kwa kuwa mara zote wanajiona hawana kitu ambacho ni rasilimali muhimu inayoweza kutumika kufanikisha lengo la kuwa na uhuru wa kifedha. Mfano, kila mtu anatamani kuanzisha biashara lakini ni wachache wanaofanikiwa kufanya hivyo na kundi kubwa la watu linaendelea kusubiria wapate mtaji kutoka nje ya uwezo walionao na kwa sasa. Hata hivyo, nimekuwa nikisisitiza kutumia mbinu ya kujilipa kwanza kama mbinu unayoweza kutumia kukusanya kiasi chochote cha pesa kama mtaji kulingana na aina ya biashara unayotaka kuanzisha.

✍🏾Kupitia neno la tafakari ya leo unatakiwa kutambua kuwa hakuna wakati ulio sahihi zaidi ya sasa. Hivyo, katika kuianza safari yako ya utajiri hatua ya kwanza unatakiwa kujiuliza una uwezo gani kwa wakati huu kabla ya kuanza kuorodhesha mapungufu uliyonayo. Katika zoezi hili hakikisha unaorodhesha rasilimali unazomiliki na thamani yake bila kuacha hata moja kuanzia rasilimali fedha, ardhi (kiwanja/shamba), vitu vya ndani, simu, nguvu kazi, chombo cha usafiri (gari, pikipiki), nyumba au ujuzi ulionao katika fani yoyote ile.

✍🏾Baada ya kupata orodha ya vitu unavyomiliki na thamani yake, tafsiri yake ni kwamba utakuwa umepata thamani ya utajiri unaomiliki kwa wakati huo. Hatua inayofuata ni kujiuliza unahitaji kukuza utajiri wako kwa kiasi gani na katika kipindi cha muda gani.

✍🏾Baada ya kujibu swali hilo, hatua inayofuata unatakiwa kujiuliza kila kitu ulichonacho kwa sasa kinaweza kutumika vipi ili kufikia utajiri unaotaka. Mfano, kama namiliki simu janja (smart phone) naweza kusema simu hii nitaitumia kwa ajili ya kukuza maarifa yangu kupitia kusoma makala, vitabu au kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa kwa njia ya mtandao.

✍🏾Mwisho, hatua inayofuata ni kuorodhesha mahitaji kwa maana ya mapungufu yaliyopo katika kufanikisha safari yako ya utajiri na kuweka mkakati wa kupunguza au kutatua mapungufu hayo kupitia rasilimali unazomiliki kwa wakati huu. Tafsiri yake ni kwamba mafanikio ya kila lengo yanaanzia ndani ya uwezo wako na baada ya hapo ndipo unaweza kuongeza mahitaji nje ya uwezo wako. Kumbuka ni sheria ya asili kuwa mwenye nacho ataongezewa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoka mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com



Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw
onclick='window.open(