NENO LA LEO (FEBRUARI 25, 2020): ANZA KWA KUBADILISHA IMANI ULIZONAZO KUHUSU PESA NA UTAJIRI

👉🏿Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa kwa ajili ya kukoleza moto ushindi mdogo mdogo wenye mwelekeo wa kutimiza malengo yako. Ni siku muhimu ambayo unatakiwa kuitumia vyema kupiga hatua za kukusogeza mbele katika mstari wako wa mafanikio bila kujali ulefu wa hatua hizo.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirisha namna ambavyo umekuwa ukishindwa kupiga hatua za kufikia uhuru wa kifedha kutoka na imani ulizonazo kuhusu pesa na utajiri kwa ujumla. Katika jamii tunayoishi kila mmoja ana mtazamo wake inapotajwa pesa au utajiri.

✍🏾Tafakari juu ya mitazamo na Imani kama hizi kuhusu pesa na utajiri: Pesa ni chanzo cha maovu katika jamii; Huwezi kuwa na pesa ukawa mtu mwema kwa jamii; Pesa zipo chache sana na kwa watu wachache wenye bahati; Ili uwe na pesa ni lazima kuwa na ushirika wa kishetani (kujiunga Freemasonry); Matajiri ni watu wachoyo; Ni heri ya kuwa masikini ili kuwa na amani moyoni kwa maana matajiri hawana amani; Familia yetu hatuna bahati ya kuwa matajiri; Ili na pesa natakiwa kuwa kupanda cheo au kiwango flani cha na elimu; na huwezi kuwa tajiri kama umezaliwa kwenye familia masikini.

✍🏾Hizi ni kauli kandamizi ambazo tunaendelea kuzisikia katika jamii inayotuzunguka. Kauli hizi zimekuwa sehemu ya maisha ya watu wengi na zinaendelea kudumuza maisha yao kutokana na kuamini katika Imani hizo. Ikumbukwe kuwa Imani ni kuwa na uhakika juu ya vitu vinavyosadikika. Tafsiri yake ni kwamba watu wengi kwa kuendelea kuamini katika kauli hizo wamejiwekea vikwazo vya kufikia uhuru wa kifedha au utajiri ambao wanautamani katika maisha yao.

✍🏾Pesa ni alama tu ambayo imewekwa kwa ajili ya kufanikisha kubadilishana bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kulingana na thamani ya bidhaa au huduma husika. Kila mmoja wetu katika jamii anakubali kuwa endapo mhusika atakosa pesa ya kukidhi mahitaji muhimu ya maisha yake ni dhairi kuwa maisha yake yatataliwa na huzuni kubwa inayoambatana na hofu ya maisha ya baadae. Ni kutokana na ukweli huu kila mmoja katika jamii anajibidisha kutafuta pesa hata kama ana Imani hovu kuhusu pesa.

✍🏾Vivyo hivyo, utajiri kwa tafsiri rahisi ni kuwa na hali ya kiuchumi ambayo inakuwezesha kupata mahitaji yako yote muhimu pamoja na wategemezi wako na kuwa na ziada kwa ajili ya dharura na vizazi vyako. Hakuna ubaya wowote katika utajiri kama utajiri huo umetafutwa kwa kufuata misingi na kanuni za kutengeneza utajiri. Unaweza kuwa tajiri na kuwa na Amani ya maisha (ukawa na usingizi), unaweza kuwa tajiri ukawa na furaha ya maisha au unaweza kuwa tajiri na kuwa mtu mwema katika jamii.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kujifanyia tathimini juu ya Imani na kauli tunazoamini kuhusiana na pesa na utajiri. Ili uwe na maisha bora unatakiwa kujifunza kila kuhusiana na pesa na utajiri ili uvunje kauli kandamizi ambazo zimekuwa zikukuzuia kusonga mbele katika kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kipesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 *Mwalimu Augustine Mathias*
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

FIKRAZAKITAJIRI.BLOGSPOT.COM
onclick='window.open(