👉🏾Habari ya asubuhi ya leo rafiki na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii ya kuboresha maisha yako katika siku hii ya leo ambapo tunaianza wiki ya pili ya mwezi Februari, 2020.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linaendelea kutuhamasisha juu ya kuongeza kasi katika safari yako ya kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kifedha.
HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Neno la tafakari ya leo linatufunulia tofauti iliyopo kati ya masikini na tajiri katika vitu wanavyonunua kwenye maisha yao ya kila siku. Tajiri ananunua vitu vinavyoongezeka thamani wakati masikini ananunua vitu vinavyopungua thamani. Hebu tuangalie mifano kadhaa ya vitu hivyo:-
✍🏾Masikini ananunua vitu kama nguo na kujaza kabati kwa pato dogo alilonalo wakati tajiri ananunua nguo kutoka kwenye sehemu ya faida. Pato lake analielekeza kwenye kukuza utajiri wake ili ukue zaidi.
✍🏾Tajiri ananunua rasilimali kama vile ardhi (viwanja & mashamba) wakati masikini ananunua vikololo ambayo vinajaza nyumba na havina athari chanya kwenye maisha yake.
✍🏾Masikini anakopa na kununua gari ili aonekane mtaa kuwa ana maisha mazuri wakati tajiri anakopa ananunua gari ya biashara au mashine za kuanzisha kiwanda ilihali yeye anaendelea kutembelea baiskeli au pikipiki mitaana. Gari analonunua masikini linaendelea kumtafutana wakati gari au mitambo anayonunua tajiri inaendelea kukuza utajiri wake. Na hatimaye tajiri atanunua gari la kutembelea kutoka kwenye faida ya biashara zake.
✍🏾Mwisho, hizi ni sehemu chache ambazo nimekuainishia kwa ajili kutafakari upya juu ya vitu unavyonunua katika maisha yako ya kila siku. Lenga kununua vitu vinavyoongezeka thamani na achana kabisa kununua makolokolo.
👐🏾Nakutakia kila la kheri katika siku hii ya leo.
🗣🗣 *Mwalimu Augustine Mathias*
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Kupata mafundisho haya kila siku jiunge kwenye kundi langu la Wahtsapp kupitia link hapa chini
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw