👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na umeiona Machi mosi ukiwa na hamasa na nguvu ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza moto wa kufanikisha malengo uliyojiwekea. Hongera sana kwa kupata nafasi hii ya kipekee katika maisha kwani wapo wengi walitamani lakini hatuko nao tena. Hata hivyo, pamoja na kupata zawadi hii unatakiwa kutambua kuwa una deni la kuhakikisha unafanya kitu maalumu na kipekee katika kipindi cha maisha yako.
.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nalenga kukumbusha kuwa siku hazigandi zinakimbia kweli kweli. Ni juzi tu tulikota kusherekea mwaka mpya wa 2020 lakini leo hii tunaingia mwezi Machi ambapo tunaelekea kuhitimisha robo ya kwanza ya mwaka. Sina hakika kama wote tunaona jinsi siku sinavyokimbia ikilinganishwa na utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea.
.
✍🏾Ni juzi tu kauli za mwaka mpya kama vile: “mwaka mpya na mambo mapya”, “mwaka huu sitakubali ni lazima niwe wa tofauti”, “huu ni mwaka wa mabadiliko”, “huu ni mwaka wa kuepukana na matumizi yasiyo ya lazima” na kauli nyinginezo nyingi ambazo zilitawala katika mitandao ya kijamii na katika nafsi za walio wengi. Swali la kujiuliza ni je umeuanza mwaka 2020 kwa kasi uliyokusudia au unaendelea na maisha ya mazoea.
.
✍🏾Kauli zote hizo ni matamanio ya nafsi yako katika kuelekea kwenye maisha ya mabadiliko ambayo umekuwa ukiyatamani kila ifikapo mwaka mpya. Nafsi yako imejaa matamanio kwa ajili ya kuboresha kila sekta ya maisha yako kuanzia kwenye afya (yawezekana unatamani kupungua uzito), uchumi (kila mtu anatamani kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha); mahusiano (kila mtu anatamani kuwa na familia yenye maisha ya upendo hai); na kiroho (kila mtu anatamani kuwa na ushirika bora wa kiroho kulingana na Imani yake).
.
✍🏾Hata hivyo, matamanio huwa yana sifa ya kuikumbusha nafsi ya mhusika kila mara ndani mwake ikiwa ni kumtaka achukue hatua zinazolenga kubadilisha matamanio hayo kuwa vitendo. Kupitia vitendo matamanio (wishes) yanabadilishwa kuwa uhalisia (reality). Hata hivyo, matamanio huwa yana tabia ya kudumu kwa kipindi cha muda maalum ndani ya fikra za mhusika na pale inapotokea hayakufanyiwa kazi ndani ya muda husika huwa yanapotea moja kwa moja.
.
✍🏾Hali hii ndio huwa inapelekea watu wengi mwishoni mwa mwaka katika kuelekea katika kipindi cha mwaka mpya wanakuwa na matamanio mengi yanayolenga kubadilisha maisha yao. Baada ya kuuanza mwaka mpya moto wa matamanio waliyokuwa nayo huwa unapoa taratibu na hatimaye wanajikuta wamerudi kwenye maisha waliyozoea.
.
✍🏾 Je ni kwa nini watu wengi wanashindwa kubadilisha matamanio kuwa uhalisia? Majibu yapo mengi lakini hayo mengi yatakayotajwa ni lazima ukutane na haya: watu ni wavivu – wanatamani mabadiliko lakini hawapo tayari kubadilika; watu wanaishi kana kwamba wana mkataba wa uhakika kuwa wataendelea kuwepo kesho – wanaishi kwa kuairisha mambo (jambo ambalo linawezekana leo linasogozwa kesho kesho kesho na hatimaye linasahaurika); watu wanaishi kwa visingizio – hakuna ambaye yupo tayari kuwajibika kwa uzembe wake na badala yake anatafuta sehemu ya kusukumia mzigo; watu hawana msingi wa elimu sahihi ya kubadilisha matamanio kuwa uhalisia; watu hawana mpango wa malengo unaowaongoza katika kila matamanio waliyonayo; watu wanahitaji mabadiliko ya haraka – wanaweka bidii siku za mwanzoni na wasipopata matokeo wanarudi kwenye maisha waliyozoea; na watu ni wepesi wa kukata tamaa – wanashindwa kukabiliana na mawimbi/changamoto katika safari yao ya mafanikio.
.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kujifanyia tathimini inayolenga kugundua kama kweli tupo kwenye dira ya kuyabadilisha matamanio tuliyokuwa nayo kipindi tunauanza mwaka huu. Pia, tunakumbushwa tabia ambazo zimepelekea tuendelee kuishi maisha ya kawaida ikilinganishwa na matamanio tuliyonayo. Wajibu wetu kupitia neno la tafakari ya leo ni kuishi kwa vitendo zaidi kuliko matamanio na maneno yasiyo na mpango wa utekelezaji.
.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw