NENO LA LEO (FEBRUARI 29, 2020): TANGULIZA THAMANI NA PESA ZITAKUFUATA

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hakika Mwenyezi Mungu amekuwa mwema kwetu kiasi ambacho muda kama huu tunaweza kuandika na kusoma neno la tafakari ya leo. Leo hii tunasema kwa kheri Fubruari, 2020 tukiwa na hamu ya kuikaribisha Machi, 2020 ili tuendeleze moto ya kufanikisha malengo makuu tuliyojiwekea katika maisha yetu kwa kipindi hiki cha mwaka 2020.
.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha siri muhimu unayotakiwa kuitumia kwa ajili ya kutengeneza pesa na hivyo kukuza uchumi wako. Pesa imekuwepo tangu ilipozinduliwa na ikawezesha kuwa msingi wa kufanikiza mauzo na manunuzi katika Jamii. Kumbuka kuwa, kabla ya ugunduzi wa pesa mauzo na manunuzi (biashara) yalikuwa yakifanyika kwa kubadilishana bidhaa na bidhaa au bidhaa kwa huduma au huduma kwa huduma.
.
✍🏾Baada ya pesa kugunduliwa, msingi wa biashara (mauzo/kununua) ulibadilika kabisa kiasi ambacho hauwezi kununua kama hauna pesa. Pesa ilibadilisha mtazamo wa Jamii kiasi ambacho mwenye pesa nyingi akawa na nguvu ya kuliteka soko kutokana na bidhaa anazozalisha au huduma anazotoa. Toka enzi hizo hadi sasa hapajatokea uvumbuzi wa kubadilisha thamani ya pesa kama msingi mkuu wa kuwezesha biashara katika Jamii.
.
✍🏾Hauwezi kununua kama hauna pesa na hauwezi kupata huduma unayotaka kama hauna pesa. Pesa imekuwa kipimo cha utajiri na imekuwa chanzo cha kulazimisha watu kufanya kazi. Utapata pesa kutokana na bidii na weledi wako katika kazi. Utajiri wako utapimwa kutokana na mali unazomiliki na mali hizo ni lazima zithaminishwe katika kipimo cha pesa. Hakuna namna kila mtu kwenye jamii nahitaji kuwa na pesa japo pesa imekuwa adimu kiasi ambacho haipo tayari kupatikana kama hujui njia zake!
.
✍🏾 Je ni fanye nini ili nipate pesa nyingi? Hili ni swali la msingi ambalo kila mtu kwenye Jamii anahitaji majibu yake na kupitia tafakari ya leo nakushirikisha jibu sahihi la kupata pesa. Jibu la kupata pesa si jingine bali ni “Hakuna muujiza wowote wa kupata pesa zaidi ya kuwa mtu wa thamani kwa Jamii”. Jamii inasubiria tunu ya thamani iliyopo ndani mwako itumike kwa ajili ya kuifaidisha na kutokana thamani hiyo Jamii ipo tayari kukuzawadia mapesa.
.
✍🏾 Je nawezaje kuwa mtu wa thamani kwa Jamii? Ni ukweli mtupu kuwa “Pesa zipo kwa watu ndani ya Jamii hii tunayoishi” na ili upate pesa hiyo ni lazima ujue jamii inataka thamani ya aina gani kutoka kwako. Jibu lipo wazi kuwa katika mfumo wa biashara ambao ndiyo msingi mkuu wa upatikanaji wa pesa ni lazima pawepo bidhaa/huduma ambayo inathaminishwa kwa thamani ya kiasi cha pesa. Tafsiri yake ni kwamba kama unahitaji kuwa mtu wa thamani kwa jamii inayokuzunguka ni lazima utambue jamii hiyo inakabiliwa na changamoto zipi.
.
✍🏾Baada ya kutambua changamoto zinazoikabili jamii, kazi iliyopo mbele yako ni kuhakikisha unatatua changamoto za jamii kupitia kazi au biashara yako. Kumbe, badala ya kulenga kupata fedha unatakiwa kulenga kutatua changamoto zilizopo katika jamii na kupitia utatuzi wa changamoto pesa zitakufuata kwa kasi. Hata hivyo, kiwango cha pesa ambacho utapata kitategemeana na nguvu, ubunifu na weledi unaowekeza katika kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.
.
✍🏾Sijui kama naeleweka hapa. Ngoja nitumie mfano huu kuelezea ili wote tuwe kwenye uelewa mmoja. Bwana Doni (sio jina halisi) anatoa huduma ya kutibu magonjwa ya ngozi katika jamii. Hivyo, thamani ya bwana Doni katika jamii ni kutibu magonjwa ya ngozi kwa watu wenye matatizo hayo. Je Bw. Doni ili apate pesa nyingi anatakiwa kujitangaza vipi katika jamii? Ili Bw. Doni apate pesa nyingi anatakiwa kujitangaza kuwa: Mimi flani nawasaidia watu kuepukana na matatizo ya magonjwa ya ngozi.
.
✍🏾Hapa ndipo watu wengi wanakosea katika kutangaza thamani wanazotoa kwa jamii. Badala ya kutangaza thamani wanazotoa wanatangaza bidhaa huduma wanazouza. Hii ni sawa na kukutana na msichana kwa mara kwanza kabla hamjatongozana ukamtaka muoane. Jibu liko wazi kuwa hautaweza kufanikiwa kuoana nae kama kweli ni mtu anayejitambua. Ndivyo, ilivyo kwenye ulimwengu wa biashara badala ya kutangaza bidhaa unatakiwa kutangaza thamani unayotoa.
.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha kuwa ili upate pesa nyingi unatakiwa kujiuliza thamani yako ni ipi katika jamii inayokuzunguka. Hii ni pamoja na kufahamu pesa zako zipo sehemu gani katika jamii. Pesa zipo katika changamoto zinazoikabili jamii. Chagua changamoto ambayo unataka kuitatua na anza kutoa thamani kwanza kabla ya kutanguliza uhitaji wa pesa.
.
✍🏾Kupata mada hii kwa undani nunua uchambuzi wa vitabu 2 vinavyotoa elimu juu ya jinsi gani unaweza kufanya biashara yenye kutengeneza faida katika karne hii ya 21. Kitabu cha kwanza ni kutoka kwa Sabri Suby ambaye amekuwa ni Muuzaji mwenye njaa ya mauzo kuliko kijana yeyote katika karne ya sasa. Kitabu cha pili ni kutoka kwa Nil Eyal ambae pia anashirikisha namna kila mmoja wetu anatakiwa kuzalisha bidhaa ambazo zinamfanya mteja awe na ushirika na bidhaa/huduma zako. Uchambuzi wa vitabu vyote hivi unapatikana kwa Tshs. 20,000/= kila kimoja na ukinunua vyote utapata kwa bei ya Ofa ya Tshs. 15,000/=.
.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
.
 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 
.
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (FEBRUARI 28, 2020): HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUWA JINIASI (GENIUS) KATIKA KILA UNALOFANYA.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umezawadiwa siku hii mpya katika maisha yako ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kupiga hatua kuelekea ushindi unaoutamani katika maisha yako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha siri itakayokuwezesha kupata mafanikio makubwa katika kila unachofanya. Siri hii nyingine bali ni nguvu ya utatu unaohusisha UTULIVU (FOCUS), MABORESHO YA KILA SIKU (DAILY IMPROVEMENT) na MUDA (TIME).

✍🏾Kanuni hii inatuambia kuwa unatakiwa na UTULIVU kwenye kila unalofanya ukiongozwa na picha kubwa uliuonayo kichwani. Utulivu huo unakuwa silaha ya kukufanya uwe mvumilivu katika unachokifanya na hivyo kuepuka kukata tamaa kabla ya muda kuvuna matunda.

✍🏾Katika kanuni hii pia tunajifunza kuwa ili tupate matokeo au matunda kwenye kila ninachofanya ni lazima tufanye maboresho ya kila siku. Hapa ndipo nimekuwa nikikusisitiza kuwa kila siku unatakiwa kusherekea ushindi mdogo mdogo ambao unachangia katika kupiga hatua kwenye ushindi wa picha kubwa uliyonayo kichwani. Bila kujali hatua zako ni fupi kiasi gani, kila siku unatakiwa kupiga hatua ambazo zinakusogeza mbele kwenye safari ya kuelekea matamanio ya mafanikio ya maisha yako. Maboresho hayo ya kila siku ni sawa na kufanya palizi kwenye mazao ambayo unasubiria yakomae kwa ajili ya mavuno.

✍🏾Kupitia kanuni hii pia tunaona nguvu ya muda katika kuelekea kwenye ushindi tunaotamani. Hapa ndipo watu wengi wamekuwa wakikosea kwa vile wanapanda mti wa matunda leo na wanataka uzae matunda kesho kabla ya muda wake wa kuzaa kufikia. Na inapotokea haujazaa matunda kwa haraka kama wanavyokusudia wanakata tamaa na kuungoa mti huo. Kupitia kanuni ya leo tunajifunza kuwa chochote unachofanya kwa sasa unatakiwa kutambua kuwa ili kikomae na kuzaa matunda kusudiwa ni lazima kipitie katika kipindi cha muda maalumu.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunatakiwa kujifunza kuwa ili tufikie mafanikio makubwa katika maisha yetu kiasi cha kuitwa jiniasi katika tunayojishughulisha nayo ni lazima kuwa na utulivu kwenye jambo moja na kulifanyia maboresho kila siku na hatimaye kulipa muda ili lifikie kwenye kipindi cha ukomavu wake.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (FEBRUARI 27, 2020): KAMA HAUJUI UNAKOELEKEA NJIA ZOTE UTAONA ZINAFAA.

👉🏿Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na una nguvu za kutosha kwa ajili ya kuendeleza bidii kazi ambazo zitakuwezesha kufanikisha malengo uliyojiwekea. Hongera sana kwa siku hii muhimu ambayo umebahatika kuzawadiwa ili uitumie kuweka utofauti katika maisha yako ya sasa.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nakushirikisha umuhimu wa kuwa na vipaumbele kwa ajili ya kufanikisha malengo uliyojiwekea. Mara nyingi katika jamii tunaendelea kuona watu ambao wana dhamira ya kuanzisha mifereji mipya ya kipato kwa ajili ya kukuza uchumi wao lakini wanajikuta katika hali ya kugusa gusa kwa juu kwenye kila mfereji wanaoanzisha. Mifereji hiyo ni sawa na njia ambazo mhusika anatakiwa kuzitumia kwa ajili ya kufikia kwenye kilele malengo aliyoyaweka kwa ajili ya kukuza pato lake.

✍🏾Tabia hii ya kugusa gusa ni uthibitisho kuwa mhusika hajui yuko wapi kwa wakati huo na anahitaji kufika wapi baada ya muda flani. Kwa vile hajui anakotakiwa kufika anajikuta katika hali ya kujaribu kila njia inayojitokeza mbele yake. Matokeo yake ni kwamba atapoteza rasilimali, muda na nguvu nyingi bila kufikia kwenye kilele cha matamanio yake.

✍🏾Tafsiri yake ni kwamba kama unahitaji kufanikiwa kwenye sekta yoyote ya maisha yako ni lazima ujue upo wapi kwa wakati huo na unalenga kufika ngazi ipi baada ya kipindi flani cha muda. Baada ya kufahamu sehemu ambayo ndiyo kilele cha matamanio yako hatua inayofuata ni kuchagua njia sahihi ambayo itakufikisha huko. Unatakiwa kuwa na vipaumbele katika njia unazochagua ili kuepuka tabia ya kuchagua kila njia ambapo mwisho wake huwa hakuna njia inayotimiza malengo yako kwa ufanisi.

✍🏾Mfano, kama umeona kuwa njia sahihi ambayo itakufikisha kwenye kilele cha mafanikio yako (uhuru wa kifedha) ni kupitia ufugaji hakikisha unafuga kisasa kwa kuanza kidogo kulingana na mtaji ulionao huku ukiwa na picha pana ya kufuga kisasa. Vunja picha hiyo pana ya kufugaji kisasa kwenye awamu kadhaa za utekelezaji na hakikisha kuwa kila siku unafanya kitu ambacho kinakusogeza kuelekea ufugaji wa ndoto yako.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tambua kuwa watu wengi wamekuwa wakifanya makosa ya kugusa gusa kwenye kila mfereji unaojitokeza mbele yao na matokeo yake wanajikuta katika hali ambayo hakuna mtaji hata mmoja ambao una tija kwenye kuelekea kilele cha matamanio yao. Leo anaanzisha mradi wa ufugani kabla mradi haujakomaa kuzalisha matunda anaanzisha mradi wa kilimo au duka na mwisho wake anajikuta hana mradi hata mmoja ambao una sura ya kumfikisha kwenye kilele cha matamanio yake. 

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (FEBRUARI 26, 2020): Roho inataka lakini Mwili ni dhahifu.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Siku hii ni kati ya zawadi za kipekee ambazo unaendelea kuzawadiwa kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kuyaishi maisha ya ndoto zako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo naendelea kukushirikisha umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kufikia kilele cha malengo yako. Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia nguvu ya roho ikilinganishwa na nguvu ya mwili. Kila mwanadamu ambaye ameumbwa amepewa vitu hivi viwili (roho na mwili).

✍🏾Pamoja na kwamba kila mwanadamu amepewa roho na mwili, vitu hivi vinafanya kazi kwa kutofautiana. Mara zote roho ipo upande wa mema kwa mhusika, roho inataka ukamilifu vitu kwa asilimia zote. Roho inataka kila kinachofanyika kifanyike kwa mafanikio makubwa sana. Roho inataka uwajibikaji na utekelezaji wa shughuli kwa viwango vya hali ya juu. Roho inataka kuepuka dhambi zote na kuwa upande wa matendo mema kwa jamii.

✍🏾Hata hivyo, pamoja na kwamba roho ipo upande wa mema haiwezi kukamilisha mambo yote yaliyopo ndani ya matamanio yake bila kushirikisha mwili. Kwa ufupi ni kwamba roho inatamani lakini haiwezi kufanya kazi bila ya mwili kuhusika. Mwili ndo unatakiwa kupokea maagizo kutoka kwa roho na kuyabadilisha kutoka kwenye matamanio au ndoto kuja kwenye uhalisia wake. Kumbe, Mwili kwa mwanadamu ndio unahusika na utekelezaji wa matamanio ya roho na bila kuwa na utayari mhusika ataendelea kuwa na ndoto au matamanio ambayo hayatekelezeki.

✍🏾Tunajifunza nini katika neno hili kuhusu roho na mwili wako? Somo kubwa la kujifunza ni kwamba katika maisha ya kila siku, mwili huwa unapenda kustarehe kwa maana haupendi maumivu au mateso ya aina yoyote ile. Unapenda kupumzika na sikujihusisha na kazi; unapenda kunywa/kula vitu vizuri; unapenda kuepukana na kazi ngumu; unapenda kulala kwa ajili ya kupata joto na kuepukana na baridi ya asubuhi; unapenda kukimbilia dhambi za kuliko matendo mema na mengine mengi. Haya ndio madhaifu ya mwili ambayo yanadumuza watu wengi kuchukua hatua dhidi ya matamanio ya roho zao.

✍🏾Mwisho kupitia neno la tafakari ya leo tunajifunza kuwa kama unahitaji kupata matokeo makubwa dhidi ya matamanio au ndoto za maisha yako ni lazima roho na mwili wako vifanye kazi kama timu moja. Roho inatakiwa kutoa maagizo kwa mwili ili mwili uitikie maagizo hayo na kuyafanyia kazi. Hakuna namna nyingine au njia ya mkato zaidi ya nguvu hizi mbili kusikilizana na kuwa kitu kimoja.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (FEBRUARI 25, 2020): ANZA KWA KUBADILISHA IMANI ULIZONAZO KUHUSU PESA NA UTAJIRI

👉🏿Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa kwa ajili ya kukoleza moto ushindi mdogo mdogo wenye mwelekeo wa kutimiza malengo yako. Ni siku muhimu ambayo unatakiwa kuitumia vyema kupiga hatua za kukusogeza mbele katika mstari wako wa mafanikio bila kujali ulefu wa hatua hizo.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirisha namna ambavyo umekuwa ukishindwa kupiga hatua za kufikia uhuru wa kifedha kutoka na imani ulizonazo kuhusu pesa na utajiri kwa ujumla. Katika jamii tunayoishi kila mmoja ana mtazamo wake inapotajwa pesa au utajiri.

✍🏾Tafakari juu ya mitazamo na Imani kama hizi kuhusu pesa na utajiri: Pesa ni chanzo cha maovu katika jamii; Huwezi kuwa na pesa ukawa mtu mwema kwa jamii; Pesa zipo chache sana na kwa watu wachache wenye bahati; Ili uwe na pesa ni lazima kuwa na ushirika wa kishetani (kujiunga Freemasonry); Matajiri ni watu wachoyo; Ni heri ya kuwa masikini ili kuwa na amani moyoni kwa maana matajiri hawana amani; Familia yetu hatuna bahati ya kuwa matajiri; Ili na pesa natakiwa kuwa kupanda cheo au kiwango flani cha na elimu; na huwezi kuwa tajiri kama umezaliwa kwenye familia masikini.

✍🏾Hizi ni kauli kandamizi ambazo tunaendelea kuzisikia katika jamii inayotuzunguka. Kauli hizi zimekuwa sehemu ya maisha ya watu wengi na zinaendelea kudumuza maisha yao kutokana na kuamini katika Imani hizo. Ikumbukwe kuwa Imani ni kuwa na uhakika juu ya vitu vinavyosadikika. Tafsiri yake ni kwamba watu wengi kwa kuendelea kuamini katika kauli hizo wamejiwekea vikwazo vya kufikia uhuru wa kifedha au utajiri ambao wanautamani katika maisha yao.

✍🏾Pesa ni alama tu ambayo imewekwa kwa ajili ya kufanikisha kubadilishana bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kulingana na thamani ya bidhaa au huduma husika. Kila mmoja wetu katika jamii anakubali kuwa endapo mhusika atakosa pesa ya kukidhi mahitaji muhimu ya maisha yake ni dhairi kuwa maisha yake yatataliwa na huzuni kubwa inayoambatana na hofu ya maisha ya baadae. Ni kutokana na ukweli huu kila mmoja katika jamii anajibidisha kutafuta pesa hata kama ana Imani hovu kuhusu pesa.

✍🏾Vivyo hivyo, utajiri kwa tafsiri rahisi ni kuwa na hali ya kiuchumi ambayo inakuwezesha kupata mahitaji yako yote muhimu pamoja na wategemezi wako na kuwa na ziada kwa ajili ya dharura na vizazi vyako. Hakuna ubaya wowote katika utajiri kama utajiri huo umetafutwa kwa kufuata misingi na kanuni za kutengeneza utajiri. Unaweza kuwa tajiri na kuwa na Amani ya maisha (ukawa na usingizi), unaweza kuwa tajiri ukawa na furaha ya maisha au unaweza kuwa tajiri na kuwa mtu mwema katika jamii.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kujifanyia tathimini juu ya Imani na kauli tunazoamini kuhusiana na pesa na utajiri. Ili uwe na maisha bora unatakiwa kujifunza kila kuhusiana na pesa na utajiri ili uvunje kauli kandamizi ambazo zimekuwa zikukuzuia kusonga mbele katika kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kipesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 *Mwalimu Augustine Mathias*
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

FIKRAZAKITAJIRI.BLOGSPOT.COM

NENO LA LEO (FEBRUARI 24, 2020): KUBALI KUWA KILICHOFANYIKA KIMEFANYIKA – SONGA MBELE NA YALIYOPO

👉🏾Habari rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kwa ajili ya kuianza vyema siku ya kwanza katika wiki ya mwisho wa mwezi Februari, 2020. Ni wiki ambayo unatakiwa kufanya tathimini juu ya hatua unazopiga katika kutimiza malengo uliyojiwekea kwenye kipindi hiki cha mwaka 2020. Ni wiki ya kuweka mikakati ili unapouanza mwezi Marchi husirudie makosa ambayo umegundu umefanya katika kipindi hiki cha miezi miwili iliyoisha.


HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linaendelea kutukumbusha wajibu wa kutopoteza muda kutokana na matendo yako yaliyopita. Kuna nyakati ambazo unajikuta katika hali ya kutopendezwa na matokeo ya maamuzi ambayo yamepelekea kutenda jambo ambalo lipo kinyume na matarajio yako.

✍🏾Zipo nyakati ambazo utajikuta unasikitika kwa kupoteza fedha zako kwenye uwekezaji ambao haujazalisha faida kama ulivyotarajia. Pengine mradi uliokusudia kuwa utatengeneza faida kubwa umekuwa sehemu ya kupoteza fedha zako ambazo umekusanya kwa kipindi kirefu au umekopa sehemu.

✍🏾Zipo nyakati ambazo utajikuta upo kwenye huzuni kubwa kutokana na matukio ambayo yapo nje ya uwezo wako. Pengine umepoteza fedha zako kutokana na kuibiwa au rasilimali zako kupotea kutokana na majanga ya kimazingira kama vile mafuriko, wadudu waharibifu au ukame.

✍🏾Zipo nyakati ambazo huzuni na hofu kubwa itatawala kutokana na matukio kama vile magonjwa, vifo vya wapendwa wako au kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki kutokana na matakwa yao wenyewe kutokana na kuishi kwako misingi na kanuni za mafanikio zinazoenda kinyume na mahitaji yao.

✍🏾Neno la tafakari ya leo linakukumbusha kuwa katika nyakati kama hizo unatakiwa kusimama imara na kurudisha nguvu kubwa ambayo itakuwezesha kukusukuma kusonga mbele. Husikubali kusimama na pengine kurudi katika maisha yako ya awali ambayo ulishajiwekea mikakati ya kuachana nayo na kuishi maisha mapya yenye misingi na kanuni za mafanikio.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tunakumbushwa umuhimu wa kutopoteza muda pamoja na dira kuu ya maendeleo ya maisha yetu hata kama tutayumbishwa na mawimbi ya Dunia hii. Neno hili linatukumbusha kuwa sio kila mara tutapata matokeo yanayoendana na matarajio yetu. Kama kuna nyakati za kupanda tunatakiwa kutarajia pia kuwa nyakati za kushuka zipo.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

NENO LA LEO (FEBRUARI 23, 2020): IFANYE TABIA HII KUWA SEHEMU YA TABIA ZILIZOPENDWA KWAKO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambayo ni siku ya mwisho katika wiki hii. Siku zinasogea na wajibu wetu kila tunapoianza siku mpya ni kujiuliza kama kweli bidii tunazofanya kila siku kama zinatusogeza kwenye ukamilifu wa malengo tuliyojiwekea.


HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha wajibu wetu katika kutunza muda. Uwepo wetu hapa Duniani una muda maalum hivyo kila sekunde tunayoishi inapunguza kwenye muda tuliyoandikiwa kuishi. Swali la msingi n kujiuliza unautumia vipi muda wa thamani ambao unazawadiwa katika kila siku ya maisha yako?

✍🏾Kupitia neno la tafakari ya leo nitakushirikisha tabia moja ambayo unatakiwa kuachana nayo kwa ajili ya kuokoa muda mwingi ambao umekuwa ukipoteza kutokana na tabia hiyo. Imani yangu kwa kila mmoja ndani ya kundi hili anamiliki TV au Kompyuta mpakato au Simu janja au vyote kwa pamoja. Vifaa hivi vimekuwa sehemu ya kuendeleza tabia ya kupoteza muda wetu wa thamani kutokana na kuwa na ratiba ya kuangalia vipindi maalumu, filamu (movies) au tamthilia.

✍🏾Katika jamii inayotuzunguka naendelea kushuhudia watu ambao wanatumia muda mwingi kukaa nyumbani na kuangalia TV kiasi ambacho wana ratiba ya vipindi mbalimbali kwenye kila Chaneli. Katika jamii hii hii naendelea kushuhudia watu ambao bado wana muda kukaa chini masaa kazaa kwa ajili ya kuangalia filamu ambazo zimeigizwa kama mfuatano wa matukio (series).

✍🏾Ni katika jamii naendelea kusikitika ninapoona kuwa kuna watu ambao wanakuwa na urahibu/uteja (urahibu) na filamu zinazoendeshwa na TV mbalimbali kwa lengo la kuvuta hisia zao hasa katika matangazo ya biashara bila ya wao kujitambua. Hii ni hatari kwa maendeleo ya mtu ambaye bado anaendekeza tabia hii.

✍🏾Nasema ni hatari kutokana na ukweli kwamba muda unaopoteza kwa ajili ya kuangalia TV au filamu ungeutumia kufanya jambo la maana kama vile kusoma kitabu, kufanya mazoezi, kuanzisha majukumu ya ziada nje ya kazi za mwajiri wako au kukaa karibu na familia yako.

✍🏾Kwa nini watu wanaangalia TV au filamu/tamthilia kwenye kompyuta au simu janja? Majibu yanayopatikana kutoka kwenye jamii ni yanajumuisha; wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata habari, kujifunza au kupumzika baada ya majukumu magumu ya siku nzima. Swali la msingi ni je wanachojifunza kinaendana na uhalisia wa maisha? Kwa maana maudhui yaliyopo kwenye filamu yanaendana na ukweli wa maisha au tamaduni zetu?

✍🏾Ukisoma taarifa za watu waliofanikiwa kimaisha utakuta hawana utaratibu wa namna hii ya kujifunza au kupata habari mpya. Kama anahitaji kujifunza kitu atasoma kitabu, makala, ripoti za kitafiti au kama atahitaji kupata habari anakuwa na ratiba ya kupata habari mpya kupitia magazeti, tovuti au mitandao ya kijamii. Huu unakuwa ni utaratibu wa kila siku ndani ya ratiba yake ya siku. 

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo naomba ujifanyie tathimini ya muda ambao umekuwa ukipoteza kutokana na tabia ya kuangalia TV au filamu mbalimbali. Baada ya tathimini hiyo ujiulize kama kweli kila unachojifunza kutokana na tabia hiyo kama kina faida katika maisha yako.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (FEBRUARI 22, 2020): UNAHITAJI KUWA TAJIRI? JIFUNZE SIRI HII YA MAUZO.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa siku umeianza vyema na upo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kupiga hatua katika kufikia malengo uliyojiwekea. Ni siku ya Jumamosi ambayo ni fursa kwako kufanya kazi za ziada kwa ubunifu ili uwe tofauti na wale ambao wanaichukulia siku hii kama siku ya mapumziko.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tunaenda kujifunza siri moja muhimu ya kukuwezesha kuuza bidhaa/huduma zako kwa kiwango kikubwa sana kuliko unavyofanya kwa sasa kama una biashara. Kabla ya kuzungumzia siri hii ningependa kila mmoja wetu afahamu kuwa hakuna namna utaweza kufikia utajiri wa ndoto yako kama hauna biashara.

✍🏾Biashara ni moja ya nyenzo muhimu ambayo itakuwezesha kukuza kipato chako hadi kufikia maisha yenye uhuru wa kifedha. Tafiti zinaonesha kuwa biashara nyingi zinazoanzishwa zinakufa katika kipindi cha miaka 5 ya awali toka kuanzishwa kwake. Hata biashara zile zinazoendelea zaidi ya kipindi hicho zinakuwa zinajiendesha kwa hasara kwa maana hazizalishi faida. Kumbuka kuwa uhai wa biashara ni kutengeneza faida.

✍🏾Je unajua ni kwa nini biashara hizo zinakufa ndani ya kipindi hicho? Jibu ni rahisi biashara nyingi zinaanzishwa na watu ambao wengi wao hawana taaluma ya misingi sahihi ya kuendesha biashara. Wengi wanaanzisha biashara kutokana na uzoefu wa kuangalia kwa ndugu, rafiki au jirani. Ni wachache sana ambao wanatambua kuwa biashara zina kanuni zake na moja ya kanuni muhimu ni kuendeleza uhai wa mzunguko wa pesa. Kiwango cha pesa inayoingia inatakiwa kuwa kubwa zaidi ya kile kinachotoka.

✍🏾Tafsiri yake ni kwamba ili biashara iendelee kutengeneza faida ni lazima mauzo yaendelee na idadi ya wateja iendelee kuongezeka. Mauzo ndio injini au uhai wa biashara yoyote ile. Waanzilishi wa biashara wengi huwa hapa ndipo wanakosea kwa kuwa hawajui siri moja muhimu ya mauzo ambayo nitakushirikisha katika makala hii.

✍🏾Je ungependa kufahamu ni siri ipi hiyo? Kama jibu ni ndiyo endelea kusoma makala hii. Siri ya mauzo ni kuepuka kutangaza bidhaa au huduma unazotoa na badala yake ukaanza kutangaza bidhaa au huduma hizo zinatatua changamoto gani katika jamii.

✍🏾Sijui kama umenielewa! Tunafanya biashara ya aina yoyote ile kwa ajili ya kutatua changamoto au matatizo yaliyopo kwenye jamii. Hivyo kabla ya kuanzisha biashara yoyote au kumshawishi mteja kununua bidhaa au huduma zako unatakiwa kumuonesha namna ambavyo bidhaa/huduma zako zitamsaidia kutatua changamoto au matatizo yake.

✍🏾Tafsiri yake ni kwamba unahitaji kwanza kumuonesha mteja tarajiwa thamani iliyopo katika bidhaa au huduma zako ikilinganishwa na matatizo yanayomkabili kwani matatizo hayo ndiyo msukumo wa yeye kuhitaji kununua bidhaa/huduma husika. Kumbe, unatakiwa kufahamu kuwa wateja wananunua kwa ajili ya kutatua matatizo au changamoto zinazowakabili. Wajibu wako kama muuzaji ni kuhakikisha unamuelimisha mteja ni kwa jinsi gani bidhaa au huduma zako zitakidhi hitaji lake.

✍🏾Hivyo ili ufanikiwe kukuza mauzo ya bidhaa/huduma zako unahitaji kuwa na programu maalumu ambayo inaendesha vipindi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wateja tarajiwa. Dunia ya karne hii imekuwa ni kijiji kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano. Hivyo, unatakiwa kutumia ukuaji wa teknolojia hii ya mawasiliano kwa ajili ya kuwa karibu na wateja tarajiwa wa bidhaa au huduma zako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha umuhimu wa kufanya biashara kulingana na ukuaji wa teknolojia ya karne hii ya 21 na kuepuka kuendelea kufanya biashara kwa kutumia mbinu za kizamani. Kupata mada hii kwa undani nimekuandalia uchambuzi wa vitabu 2 vinavyotoa elimu juu ya jinsi gani unaweza kufanya biashara yenye kutengeneza faida katika karne hii ya 21.👇🏾

👉🏾Kitabu cha kwanza ni kutoka kwa Sabry Suby ambaye amekuwa ni Muuzaji mwenye njaa ya mauzo kuliko kijana yeyote katika karne ya sasa. Kitabu cha pili ni kutoka kwa Nil Eyal ambae pia anashirikisha namna kila mmoja wetu anatakiwa kuzalisha bidhaa ambazo zinamfanya mteja awe na ushirika nazo kwa kutengeneza tabia mpya katika maisha yake. Uchambuzi wa vitabu vyote hivi unapatikana kwa Tshs. 20,000/= kila kimoja na ukinunua vyote utapata kwa bei ya Ofa ya Tshs. 15,000/=.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

NENO LA LEO (FEBRUARI 21, 2020): HAUWEZI KUCHAGUA UZALIWE KATIKA HALI GANI HILA UNAWEZA KUCHAGUA UFE KATIKA HALI FLANI

👉🏾Habari ya asubuhi hii ya leo rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii katika malengo uliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yako.

HUSIPOTEZE NAFASI YA KUPATA MAFUNDISHO HAYA KILA SIKU PAMOJA NA KUJUMUIKA NA FAMILIA YA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  BONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE NA KUNDI LA WHATSAPP. Jiunge sasa nafasi ni chache.
👉🏾Kumbuka husisahau kutengeneza ushindi mdogo mdogo kila siku kwani kupitia ushindi huo unazidi kupiga hatua kuelekea kwenye kutimiza malengo makuu uliyojiwekea katika kila sekta ya maisha yako.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutukumbusha kuwa maisha ya hapa Duniani ni mafupi na hakuna anayejua mwisho wake ni lini. Kutokana na fumbo hilo lilipo katika maisha yetu ndipo tunatakiwa kuchagua hatima ya maisha yetu iwe katika hali gani pindi mauti yatakapotufikia.

✍🏾Ni moja ya sheria ya asili ya uwili kinzani (Natural law of polarity) ambayo inatukumbusha kuwa kama kuna kuzaliwa pia kuna kufa. Kila mwanadamu anayeishi katika Dunia hii siku ikifika ni lazima aonje mauti. Pamoja na kwamba kifo kinaogepesha kwa kiumbe chochote chenye uhai lakini hakuna namna maisha yana mwisho wake.

✍🏾Hauwezi kuchagua uzaliwe katika hali gani kwani kama ingekuwa hivyo kila mtu angechagua kuzaliwa kwenye familia tajiri. Jambo moja ambalo una uwezo nalo katika maisha yako ni kuchagua hatima ya maisha yako iwe katika hali ipi ili hata mauti yakapowadia kwako uacha alama kwa kipindi ambacho umezawadiwa kuishi.

✍🏾Unawezaje kuacha alama jina lako? Mwandishi Robin Shama katika kitabu chake cha “The Greatness Guide” anatufundisha kuwa tunatakiwa kufa kila siku! Ndiyo, husiogope unatakiwa kufa kila siku. Tafsiri ya fundisho hili, mwandishi anatushirikisha kuwa kila siku unatakiwa kujiuliza swali moja “kama leo ingekuwa ni mwisho wa maisha yangu ni mambo yapi ambayo jamii ninayoiacha ingejivunia kwa kipindi kifupi cha maisha yangu”?.

✍🏾Swali hili linaambatana na tafakari ya kujiuliza maswali haya kila asubuhi: “kama siku ya leo ingekuwa ndiyo mwisho wa maisha yangu ni kipi ambacho ningefanya kukamilisha kusudi la maisha yangu hapa Duniani?, Kama ningepata nafasi ya kuishi siku zaidi ni mambo yapi ambayo ningefanya kwa ajili ya kuepuka maisha niliyofanya hapo awali? Je ni watu gani ambao ningepata muda wa kuishi zaidi ningependa wawe karibu yangu? Je ni watu wapi katika jamii inayonizunguka ningependa kupata muda kidogo kwa ajili ya kuomba msamaha makosa niliyowakosea?

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa maisha yetu hapa Duniani yana mwisho. Jambo linalowezekana leo hakikisha linafanyika leo badala ya kusema nitafanya kesho. Neno hili ilikuwa niandike mwanzoni mwa mwezi huu hila kila ilipokuwa inafika muda wa kuandika nilikuwa nalisogeza mbele. Hali hii ilitokana na ukweli kwamba kila mtu anaogopa kifo. Hila jana bahati mbaya nimeondokewa na rafiki yangu ambaye nilipopata taarifa za kifo chake sikuamini kabisa. Masikitiko hayo ndo yamenisukuma niwashirikishe neno hili kwa ajili ya kila mmoja wetu kuishi akitambua kuwa maisha yana mwisho hivyo husipende kuahirisha mambo.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw