Habari ya leo rafiki yangu na mfuatuliaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri. Hongera kwa kuendeleza jitihada zinazokusogeza kwenye ukamilisho wa vipaumbele vya maisha yako.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
Karibu katika makala ya leo ambayo ni mwendelezo wa makala iliyohusu kujilipa kwanza.
Makala iliyopita tuliona jinsi unavyoweza kutumia mbinu ya kujilipa kwanza kujenga tabia ya kuweka Akiba na Uwekezaji.
Tuliona unaweza kutumia mbinu hii kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili malengo tofauti.
Katika makala hii tutajifunza mbinu tano ambazo unatakiwa kuzingatia wakati unapoendelea kujilipa kwanza.
Naamini mpaka sasa umedhamiria kujilipa kwanza na tayari umeshaamua kiwango ambacho utakuwa unajilipa kwa siku, wiki au mwisho wa mwezi.
Pia, umeshaainisha malengo ambayo unahitaji kufanikisha kupitia tabia hii mpya ya kujilipa kwanza.
Kama majibu yako ni ndiyo karibu ujifunze mambo matano ya kuzingatia katika safari yako mpya:-
Chagua kiwango rafiki kulingana na uwezo wako. Makala iliyopita nilieleza kuwa inashauriwa kutenga kati ya asilimia 10 hadi 20 ya kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba, yaani kwa ajili kiwango unachojilipa.
Hata hivyo, wakati unaanza asilimia 10 inaweza ionekane kuwa kwako!
Hali hii huwatokea watu wengi kutokana na ukweli kwamba kujenga tabia mpya ni zoezi gumu ikilinganishwa na kuendeleza tabia ambayo imezoeleka kwako.
Kujilipa Kwanza ni tabia sawa na zilivyo tabia nyingine, unahitaji kujifunza taratibu hadi iwe sehemu ya mazoea yako.
Wakati unaanza unaweza kujilipa hata asilimia 5 ya pato lako na hakikisha unafanya hivyo bila kuacha angalau kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Baada ya kipindi hicho, angalia kiasi ulichofanikiwa kukusanya na jiulize kama ni utaratibu mzuri wa kuendelea nao kabla ya kuamua kuongeza au kupunguza kiwango cha kujilipa.
Chagua sehemu salama ya kuwekeza kiasi unachojilipa. Kuna watu wengi ambao hufanikiwa kujilipa kwanza lakini hujikuta katika mtego wa kutumia kiwango wanachojilipa kinyume na malengo yao ya awali.
Asilimia kubwa ya watu hawana uwezo wa kujizuia kutotumia pesa ambayo ipo sehemu ambako inafikiwa kirahisi.
Kuna watu wanakusanya pesa kwa malengo maalumu kwa kuidumbukiza kwenye kibubu lakini ghafla kibubu huvunjwa kabla ya muda uliokusudiwa awali.
Wapo watu ambao hufungua akaunti ya benki na kukusanyia pesa huko lakini kwa kuwa kadi ya benki inakuwa mikononi mwao hujikuta wametoa hela yote na kuidumbukiza kwenye matumizi mengine nje ya malengo ya awali.
Kumbe, ili ufanikiwe kujilipa kwanza na kutimiza malengo yako ni vyema pesa unayojipa iwekwe kwenye akaunti maalumu yenye masharti yanayokubana.
Mfano, benki nyingi zina akaunti maalumu ambazo unaruhusiwa kukusanyia pesa yako na huruhusiwi kuchukua pesa hiyo mpaka kipindi cha mwaka au zaidi.
Sehemu nyingine ambapo unaweza kuwekeza pesa unayojilipa ni Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Kwa hapa kwetu UTT AMIS).
Muhimu! Iwe benki katika akaunti maalumu au sehemu yoyote ile, unashauriwa kuwekeza pesa yako sehemu ambako kuna ongezeko la riba (interest).
Ainisha kipindi cha Uwekezaji au Akiba unayokusudia kujilipa kwanza. Hapa unatakiwa kujua ni kiasi gani unahitaji kukusanya kadri unavyojilipa na kwa muda gani.
Yawezekana unakusanya hela kwa ajili ya mpango wako wa kustaafu!
Yawezekana unakusanya hela kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu kwa mwanao ambaye yupo shule ya msingi kwa sasa!
Yawezekana unakusanya kusanya mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara!
Yawezekana unakusanya pesa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa nyumba au kununua gari!
Kwa ujumla, lengo la kiasi cha pesa unachohitaji kukusanya hupelekea kuamua kipindi maalumu ambacho unatakiwa kujilipa hadi kufanikisha lengo husika.
Mshirikishe Mwenza Wako Kama Yupo. Kama tayari umefanikiwa kumpata mwenza wako hakikisha anakuwa Mshirika wa karibu katika malengo yako ya kujilipa.
Mshirikishe unakusudia kujilipa kiasi gani na kwa muda gani bila kusahau chanzo cha pesa.
Mshirikishe malengo ya muda mfupi na muda mrefu katika kukuza pato na miradi ya familia kupitia utaratibu wa kujilipa kwanza.
Mhamasishe umuhimu wa yeye kuwa upande wako ili kwa pamoja mfanikishe malengo unayokusudia.
Tunza rekodi. Kumbukumbu ni muhimu kwenye kila shilingi unayojilipa.
Ikiwa hauna kumbukumbu hauwezi kujua umejilipa kiasi gani na kiasi gani kimezalishwa kupitia ongezeko la riba.
Pia, kumbukumbu ni njia ya kudumumisha shauku na hamasa ya kuendelea kujilipa kwanza kadri unavyoendelea kujenga tabia mpya.
Kufanikisha hilo, unashauriwa uwe na utaratibu wa kupitia kumbukumbu zako mara kuwa mara.
NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.
WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.