[Zinduka] Kwa Nini Uendelee Kuwa Mtumwa wa Msongo wa Mawazo?

NENO LA SIKU_FEBRUARI 3/2022: [Zinduka] Kwa Nini Uendelee Kuwa Mtumwa wa Msongo wa Mawazo?


📌Habari ya asubuhi rafiki na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa fikra za kitajiri. Hongera kwa kufanikiwa kupata kibali cha kuendelea kuvunja vunja malengo muhimu ya maisha yako. Ikiwa bado tupo mwanzoni mwaka, naamini unaendelea kutumia muda, nguvu, akili na rasilimali pesa kwa ajili ya kufanikisha malengo uliyoyaainisha katika kipindi chote cha mwaka huu. 


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA 


📌Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitaangazia jinsi ambavyo asilimia kubwa ya watu katika jamii wanaendelea kuharibu maisha yao kutokana na kuruhusu utumwa wa msongo wa mawazo. Kwanza tufahamu kuwa, msongo wa mawazo hutokana na mfadhaiko wa akili ambao kimsingi siyo ugonjwa ingawa unaweza kupelekea uwepo wa athari za kudumu kea kusababisha magonjwa sugu kwa mhusika.


📌Kwa asili chanzo cha mfadhaiko wa akili hutokana na mabadiliko kwa mhusika kama vile mafanikio ya ghafla, kuanzisha mradi mpya au kupata kazi mpya, hulka ya bosi au wafanyakazi wenzake, matukio ya kijamii, mahusiano au majukumu ya kifamilia. Kulingana na chanzo chake, mfadhaiko unaweza kuwa stahimilivu au wenye hatari kwa mhusika.


📌Jamii ya sasa inakabiriwa na mfadhaiko wa akili ambao chanzo chake ni taarifa za uongo, ahadi za uongo, kutingwa kwa mahitaji ya kifedha, changamoto za kiafya na kukua kwa uhasama kwenye mahusiano ya familia na jamii. Hali hii inasababishwa na watu kuendelea kujazwa taarifa za uongo kuhusiana na ukombozi wa kiroho, kiuchumi, kiafya, kisiasa, kimahusiano na hata kijamii. 


📌Kulingana na takwimu za mtandao wa www.singlecare.com,  takribani watu milioni 284 kwa mwaka 2017 waliripoti kuwa na msongo wa mawazo duniani kote, Tanzania ikiwa ni nchi ya tatu yenye idadi ya watu wengi wenye msongo wa mawazo (57%). 


📌Madhara ya msongo wa mawazo ni kuchangia kuongezeka kwa matatizo kama vile maumivu ya kichwa, vidonda vya tumbo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo, kisukari, pumu, kupanda kwa hasira, na wasiwasi. Hali hii inafifisha furaha, upendo, amani na utulivu katika familia na jamii kwa ujumla.


📌Ni dhahiri kuwa chanzo halisi cha idadi kubwa ya watu wenye msongo wa mawazo ni uwepo wa watu wengi wanaoishi bila kuwa na mwongozo maalumu wa maisha. Watu wa aina hii kila kukicha wanasukumwa na mawimbi kutoka upande mmoja wa bahari hadi upande mwingine pasipo kufanikisha hitaji halisi la maisha yao. Hali hii ni sawa na kusafiri katika njia ambayo hujui inakupeleka wapi. Yaani, unasafiri bila kuwa na dira maalumu wala kufahamu kilele cha safari yako. Ikiwa hujui uendako ni dhahiri kuwa utandanganywa kila mara.


📌Nihitimishe kwa kukuuliza maswali haya: Je! Upo salama kiasi gani? Je? Unaijua njia sahihi ya safari ya maisha yako? Je! Njia unayosafiria katika maisha yako ya kila siku imekusababishia au kukuepusha na msongo wa mawazo kwa kiasi gani? Haya ni maswali ambayo yanakutaka kufanya tathimini binafsi ya nafsi yako kwa kuzingatia matakwa ya ndoto za maisha yako. Nakutakia kila heri katika tafakari halisi ya maisha yako.


PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA BORA HAPA DUNIANI

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.




onclick='window.open(