UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Zingatia Haya Unapochagua Pakuweza Pesa Unazojilipa

NENO LA SIKU_MACHI 01/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Zingatia Haya Unapochagua Pakuweza Pesa Unazojilipa.
Wekeza pesa: kwanini ufanye
Hongera rafiki yangu kwa siku hii ya leo ambayo naamini imekuwa miongoni mwa siku za kukusogeza kwenye ushindi mkubwa katika maisha yako. 

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha dondoo muhimu za kuzingatia unapochagua sehemu salama ya kuwekeza pesa unazojilipa. Kama ndio mara ya kwanza unaanza kusoma makala hizi, nashauri upitie makala zilizotangulia ili tuwe na uelewa sawa. 

Katika makala ya jana nilieleza kuwa inashauriwa kiasi cha pesa unachojilipa kiwekezwe kwenye akaunti maalumu tena ambayo angalau kwa mwaka inaongezeka kulingana na utaratibu wa riba ya benki au sehemu yoyote unakowekeza pesa hiyo. 


Unapochagua sehemu ya kuwekeza pesa zako hebu fikiria dondoo zifuatazo:-

Husitarajie kupata pesa ya haraka. Watu wengi wanapoambiwa huduma mbalimbali za akaunti maalumu kwenye benki za biashara au Uwekezaji kwenye masoko ya mitaji hudhania kuwa watapata pesa nyingi tena kwa haraka sana. 

Kuanzia leo, fahamu kuwa siyo kweli kuwa kuna benki au uwekezaji wa masoko ya mitaji (capital markets) ambao utakupatia pesa ya haraka. Unapowekeza ni vyema utambue kuwa ili uvune matokeo makubwa, Uwekezaji wako unaweza kuchukua mwaka au miaka kadhaa na faida unayopata ni ndogo, wala siyo kubwa. 

Kumbe, faida ipo kwenye ukamilifu wa malengo yako ya kujilipa kwanza kuliko faida inayopatikana katika benki au masoko ya mitaji uliyochagua. 

Hakuna sehemu salama ya kuwekeza hila kuna sehemu zenye hatari kidogo. Pamoja na usalama katika akaunti maalumu za benki au kwenye masoko ya mitaji, ni lazima ieleweke kuwa uwekezaji wowote, unahusisha hatari (risk), tena ambazo zinaweza kupelekea hupoteze pesa zote ulizowekeza. 

Hivyo, unapochagua sehemu ya kuwekeza pesa unayojilipa inashauriwa utafute sehemu ambapo hatari za uwekezaji zimepunguzwa. Husikimbilie kushawishiwa na watoa huduma kwenye benki za biashara au masoko ya mitaji, hakikisha una uelewa na taarifa za kutosha kabla kuwekeza huko. 

Fahamu gharama za uendeshaji na taratibu za kujiondoa kwenye Uwekezaji husika. Kuna akaunti za benki ambazo huwa zina makato ya kila mwezi au pale unapotaka kujiondoa unakatwa asilimia fulani ya kiasi ulichowekeza. 

Pia, wakati mwingine huwa kuna makato ya kodi wakati unapoamua kuchukua pesa ulizowekeza. Mfano, kwenye baadhi ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja ya UTT AMIS huwa kuna gharama za kujiondoa (exit load) lakini kuna baadhi ya Mifuko ndani ya UTT AMIS hiyo hiyo ambayo aina gharama za kujitoa. 

Hivyo, ikiwa umechagua Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (UTT AMIS) huna budi kuchagua mfuko ambao hauna gharama za kujiondoa.

Fikiria ongezeko la riba litakalopatikana kutokana na Uwekezaji wako. Katika kuchagua sehemu yenye riba nzuri, unashauriwa kutumia Kanuni ya 72 (the Rule of 72). Kanuni hii inatumika kugundua kipindi ambacho pesa uliyowekeza itaongezeka mara mbili yake kutokana na ongezeko la riba. 

Kwa maneno mepesi, Kanuni ya 72 ni dhana inayotumia namba kutabiri muda ambao uwekezaji wako utahitaji kuongezeka mara mbili ya kiasi kilichowekezwa. 

Ni kanuni rahisi ambayo kila mtu anaweza kutumia kwa kuzidisha 72 dhidi ya riba ya kila mwaka inayotokana na mtoa huduma wako (akaunti maalumu uliyochagua kuwekeza pesa zako). 

Lengo ni kubainisha muda ambao utahitajika ili uwekezaji wako uongezeke kwa 100%, yaani uongezeke mara mbili.

 T = 72/r, 
Ambapo (T) ni muda ambao Uwekezaji wako utaongezeka kwa asilimia 💯 na (r) ni riba inayotolewa na mtoa huduma wako. 

Mfano, itachukua muda gani Tshs. 5M kuongezeka mara mbili kwa riba ya asilimia 10 inayotolewa na benki X? 

Chukua 72/10 au 72*0.1 (10/100) na utapata 7.2. 

Hivyo, ikiwa sitaongeza uwekezaji wowote kwenye akaunti yangu katika benki X, milioni tano ninayowekeza leo itahitaji miaka saba na miezi miwili kuongezeka kwa asilimia 💯 endapo riba hiyo itaendelea kutolewa na benki X katika kipindi chote cha miaka 7 na miezi miwili. 

Hivyo, ikiwa kuna benki nyingine labda yenye riba chini ya asilimia 10, nitachagua benki X ili kupunguza muda ambao pesa yangu itaongezeka mara mbili. 

Naamini umenielewa kwenye jinsi ya kuchagua sehemu ya kuwekeza pesa zako kwa kutumia kigezo cha ongezeko la riba.  

Kwa ujumla, jiulize maswali yafuatayo unapochagua sehemu ya kuwekeza pesa unayojilipa; 

Je, ni uwekezaji gani ulio salama na wenye faida zaidi? Swali hili linalenga kukuwezesha kuchagua akaunti ya akiba yenye mavuno mengi na salama. 

Ni uwekezaji gani ambao utanibana nisishawishike kutumia kiasi ninachowekeza kabla ya kutimiza malengo? Swali hili linalenga kukujengea nidhamu binafsi kwenye kiasi cha pesa unachojilipa. 

Je, ni njia zipi rahisi za mimi kuwekeza pesa ninazojilipa? Swali hili linakutaka kutambua njia zitakazotumika kuwekeza pesa unayojilipa kwa muda muhafaka. Mfano, kutambua kama unaweza kuwekeza kiasi unachojilipa kupitia simu (mobile transactions) na kupunguza muda wa kwenda benki. 

Hitimisho
Leo ndiyo wakati sahihi wa kuamua kujilipa kwanza. Amua utakuwa unajilipa asilimia ngapi ya pato lako! 

Fikiria juu ya muda gani unadhamiria kusubiria kiasi unachowekeza. Tafuta uelewa zaidi kuhusu sehemu zipi uwekeze kiasi unachojilipa.

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.

Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(