Fahamu Jinsi Unavyojikwamisha Kupitia Fikra Hasi

NENO LA SIKU_FEBRUARI 15/2022: Fahamu Jinsi Unavyojikwamisha Kupitia Fikra Hasi.

📌Habari yako rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri! Hongera kwa siku nyingine ambayo ni miongoni mwa siku za kufanikisha ushindi mkuu wa maisha yako. Njia pekee ya kukufikisha kule unakotamani katika kila sekta ya maisha yako ni kuhakikisha kila siku ya maisha yako unafanya jambo ambalo linatengeneza ngazi ya kuelekea juu zaidi.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📌Makala ya leo ni miongoni mwa makala zinazolenga kufunua akili yako ili upate kutambua kuwa kila mara umekwama kufanikisha ndoto zako kwa kuendekeza fikra hasi.


SOMA PIA: MUHIMU! Fahamu Jinsi Unavyojikwamisha Kupitia Mfumo Wako wa Fikra


📌Wakati mwingine yawezekana hata sasa unajiuliza mbona mimi siyo mtu wa kuwaza mambo mabaya lakini sifikii kilele cha mafanikio ya ndoto zangu? Iwe unakubali au unakataa, jambo la msingi ambalo unatakiwa kulitambua ni: wewe ni zao la kile unachowaza muda wote.


📌Katika hilo, Stephen Covey aliandika: "Tunauona ulimwengu, siyo jinsi ulivyo, bali jinsi tulivyo - au, kama tulivyozoeshwa kuuona. Tunapofungua midomo yetu kuelezea kile tunachokiona, ukweli ni kwamba huwa tunaelezea kupitia uzoefu wetu wenyewe, maoni yetu, na dhana au hisia zetu badala ya uhalisia au ukweli wa kitu husika."


📌Huu ndiyo ukweli ambao kila mara unakwamisha watu wengi kufikia kilele cha mafanikio katika kila hitaji la maisha.


📌Tukirudi katika mada ya leo, fikra hasi huwa zina ushawishi mkubwa katika kuamua mawazo yanayokubaliwa na kupewa kibali cha kutekelezwa katika uhalisia wake. Kupitia fikra hasi unaweza kukesha usiku kucha na asubuhi ukaendelea na mawazo hayo na hata kufikia kiwango cha kujiona hakuna unaloweza kufanikisha maishani mwako. Hali hii hupelekea kujidharau mwenyewe katika vitu vya msingi vya kuamua mafanikio yako. 


📌Swali la msingi la kujibu ni: Nitawezaje kutambua nimekuwa nikijikwamisha kimaendeleo kwa kuendekeza fikra hasi? Kadri unavyosoma makala hii nataka utafakari mfumo wako wa fikra kwenye sehemu zifuatazo pindi unapofanya maamuzi ya msingi yanayolenga kufanikisha ndoto zako.


📌Mtazamo wa kuona kila mara haiwezekani kwa kila tukio au hali. Mtu ambaye anazuiwa na fikra hasi za kundi hili mara zote huwa anaona na kuwaza upande wa kutowezekana katika kila tukio au hali. Mtu wa aina hii kila anapoletewa wazo jipya mara zote kabla ya kuangalia uwezo wake anaanza kuorodhesa mapungufu aliyonayo na kuhitimisha kuwa haiwezekani.


📌Katika hali hii mapungufu hupelekea kutochukua  hatua za ziada zinazolgenga kutafuta suluhu ya kufanikisha hali au tukio husika. Hawa ni watu ambao mara zote wanajiona dhaifu katika kufanikisha au kupata kila jambo zuri wanalotaka.


📌Mfano, jiulize ikitokea leo hii unaambiwa baada ya miezi kumi kuanzia sasa unatakiwa kumiliki milioni kumi kwenye akaunti yako! Ni lazima kuna sauti imelia ndani mwako! Kama ndivyo, sauti hiyo imekuambia nini kati ya INAWEZEKANA au HAIWEZEKANI? Kama imekuambia haiwezekani ni dhairi kuwa na wewe ni miongoni mwa watu wanaozuiwa na fikra hasi.


📌Badala ya kusema haiwezekani ulitakiwa kujiuliza jinsi gani (how)? Unapojiuliza jinsi gani unaitaka akili ianze kutafuta mikakati au mbinu ambazo zitawezesha ufanisi wa hitaji husika.


📌Kuwaza matukio hasi pekee katika kila tukio au hali. Hii ni pale ambapo akili ya mtu muda wote inawaza au kuona hali na matukio hasi pekee. Watu wa aina hii akili yao imetawaliwa na hali au matukio hasi ikilinganishwa na yale ambayo ni chanya.


📌Kuna watu ambao asubuhi hadi jiona hana jambo jema lolote ambalo anaweza kujisifia au kuliona kutoka kwa watu ambao amekutana nao katika siku husika. Kuna watu ambao wanaishi na ndani ya familia moja lakini hana hata jambo jema ambalo anaweza kuliona kwa wanafamilia wenzake.


📌Kuna watu ambao kila mara akiambiwa aelezee anachojua kuhusu jambo fulani anaanza kwa kutanguliza changamoto au mapungufu ya jambo husika. Jiulize kila mara unapoona au kuambiwa jambo jipya akili yako huwa inakuambia nini? Wapo watu ambao katika kila tukio au hali akili yao huwa inawakumbusha matukio au hali hasi zilizowahi kutokea zamani. 


📌Kutafsiri hali hasi muda wote kuhusu watu, hali, tukio au mazingira. Hawa ni watu ambao muda mwingi hutafsiri na kupata majibu hasi kuhusu watu, vitu, eneo, tukio au hali hata kabla ya kutafiti zaidi.


📌Watu katika kundi hili mara nyingi kila akikutana na watu au kuingia kwenye maeneo mapya hutafsiri upande hasi kuhusu watu au maeno hayo. Wapo watu ambao wameshindwa kufungua milango ya mafanikio ya maisha kwa kudhania wapo watu wabaya dhidi yao.


📌Fikiria ni mara ngapi umeshindwa kuchukua hatua ya mahusiano ya kikazi, kibiashara, kiroho, kiuchumi au kiungozi kwa kudhania watu wana nia mbaya dhidi yako. Fikiria ni mara ngapi umeshindwa kueleza shida zako kwa watu kwa vile unadhani hautaeleweka au hakuna watu wa kusikiliza shida zako. 


📌Kila mara kutabiri matokeo hasi. Hawa ni watu ambao muda wote wanawaza kupatwa na mabaya katika kila hali au tukio lililopo mbele yao. Wakati mwingine yale wanayowazia hutokana na historia ya matukio hasi katika maisha yao, matukio ya asili (ukame, mafuriko, mioto au vifo) au matukio ya jamii.


📌Tabia hii pia ina uhusiano huambatana na hali ya kuamua hatima ya matukio yajayo kutokana na matukio yaliyopita. Fikiria athari za usaliti wa kimahusiano kama umewahi kusalitiwa na tafakari yanakuathiri vipi katika maisha ya sasa. Wapo watu ambao baada ya kusalitiwa walifunga mioyo yao hata kama wameingia mahusiano mapya bado hawapendi kama walivyopenda zamani.


📌Fikiria athari za hasara uliyowahi kupata iwe kwenye biashara, kilimo au ufugaji kutokana na matukio ambayo yalikuwa nje ya uwezo wako.


📌Fikiria athari ya stori au taarifa mbaya ambazo umewahi kuambiwa kuhusu mtu, mradi au eneo, wapo watu wakishaambiwa habari mbaya kuhusu mradi, mtu au eneo wanaamini moja kwa moja na kufunga katika akili yao kiasi cha kutoruhusu kupokea taarifa mpya. Ili uondokane na tabia hii unatakiwa kujifunza kuwaza na kuona upande chanya katika maisha yako ya kila siku.


📌Mfano, mtu ambaye amewahi kutapeliwa pesa kila atakapoletewa wazo jipya linalohusu kutoa pesa, akili yake itamwambia hawa matapeli tu! Hana muda wa kuchunguza tofauti za wazo la sasa na lile ambalo alitapeliwa. 


📌Nihitimishe makala hii kwa nukuu kutoka kwa Viktor Frankl; "Kila kitu kinaweza kuchukuliwa kutoka kwa mwanadamu labda jambo moja: uhuru wa mwisho wa mwanadamu - kuchagua mtazamo wa mtu katika hali yoyote, kuchagua njia yake mwenyewe." Kila mara tuna uhuru wa kuchagua jinsi gani tunataka maisha yetu yawe kupitia fikra na mawazo yetu juu ya watu, vitu, matukio au hali zinazotunguka.


📌Tunaweza kufanikisha chochote au kuwa mtu yoyote ikiwa tutaruhusu akili yetu ione na kudumu katika mafanikio tunayotamani katika kila sekta ya maisha yetu.


KIJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA, JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.




onclick='window.open(