AMKA SASA! Hivi Unatambua Kuwa Haujaumbwa Kuwa Masikini?

ENO LA SIKU_FEBRUARI 20/2022: AMKA SASA! Hivi Unatambua Kuwa Haujaumbwa Kuwa Masikini?

📌Ni siku nyingine ambayo tumezawadiwa kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yetu. Hongera rafiki yangu kwa kuendelea kuwa miongoni mwa watu ambao wanajifunza maarifa mbalimbali kupitia mtandao wa Fikra za Kitajiri katika siku hii ya leo.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📌Karibu tena katika makala yetu ya leo ambapo tutajifunza kuwa tumeumbwa kuwa matajiri katika kila hali na kila kitu. Neno utajiri huvuta hisia za watu wengi katika jamii kutokana na mitazamo ya watu kuhusu maisha ya utajiri.


📌Jamii imeaminishwa kuwa maisha yenye utajiri ni toshelevu, kwa maana ya maisha yasiyopungukiwa kwenye mahitaji ya msingi (basic needs). Pia, mbali na mahitaji ya msingi jamii inaamini maisha ya utajiri ni toshelevu kwenye mahitaji yasiyo ya lazima yaani mahitaji ya ziada (extra wants).


📌Kutokana na imani hii, watu wengi wanataka utajiri kama njia ya kuishi maisha toshelevu. Pia, utajiri ni kiu ya wengi kwa kuwa huchukuliwa kama njia ya kulifikia kusudi kuu la maisha ambalo hujumuisha kuongeza uhakika wa kila kiumbe kuishi, kuonja uzoefu wa kila aina na katika kiwango cha juu kabisa, na kuongeza uwezo wa kufikia uzoefu mpya na wa kipekee bila ya kuwa na hofu. Ndiyo, maisha si kingine zaidi ya kuishi kwa ajili ya kufikia malengo hayo matatu.


📌Kwa undani wa malengo haya matatu tunaweza kuona kuwa maisha ni kwa ajili ya kuujaza ulimwengu na uzoefu mapya kupitia matumizi ya nguvu na ujuzi tuliopewa toka kuumbwa kwetu. Hii inajumuisha udadisi na ubunifu kwa ajili ya kutafuta uzoefu mpya katika kila sekta ya maisha.


📌Pia, tunaweza kuona kuwa hatujaumbwa kuishi maisha ya dhiki, magonjwa, njaa au kila aina ya mateso bali tumeumbwa kuupenda na kuufurahia ulimwengu. Na tunaweza kufanikisha kusudi hili ikiwa tutahusisha furaha na majukumu yetu ya kila siku, yaani tunatakiwa kutambua kuwa kazi ni njia ya ufanisi wa kila hitaji la maisha yetu hivyo hatuna budi kupenda kile tunachofanya. 


📌Turudi katika mada yetu ya msingi kuhusu maisha na utajiri, maelezo hapo juu yanalenga uone ni kwa jinsi gani utajiri ni muhimu katika kuliishi na kulifikia kusudi kuu la maisha.


📌Ukweli ni kwamba mtu masikini au taifa masikini haliwezi kutimiza malengo makuu matatu ya maisha tuliyoona hapo juu. Masikini hana uwezo kuwezesha uendelevu wa maisha yake achilia mbali kuwezesha uendelevu wa maisha ya viumbe wengine!


📌Masikini hana uwezo wa kuonja uzoefu wa kila aina na katika viwango vya juu kabisa! Lengo hili linahusisha uwezo wa kutembea sehemu mpya na zenye asili tofauti kwa ajili ya kujifunza, kufurahi na kuona uzuri wa asili au vyote vinavyoujaza ulimwengu.


📌Mwisho, masikini hana uwezo wa kuongeza uzoefu mpya na wa kipekee pasipo kuwa na hofu. Pamoja na kwamba tumeumbwa kwa ajili ya kuongeza uzoefu mpya kuhusu maisha dhidi ya nafsi zetu, watu wengine na mazingira kwa ujumla, hofu imetufanya tupoteze uwezo huo wa asili wa kuumba vitu vipya ambavyo vinaujaza ulimwengu na uzoefu mpya.


📌Uzoefu mpya unaongezwa kupitia njia tatu ambazo ni: idadi (quantity), ubora (quality), na radha au aina tofauti (variety). Yaani chochote ambacho tunadhani kinasaidia kuongeza uzoefu mpya kinatakiwa kupatikana au kuzalishwa kwa wingi (idadi), viwango vya juu (ubora) na muundo au staili za kila aina (radha).


📌Yote hayo si kingine zaidi ya kuhitimisha kwa kusema tunahitaji utoshelevu kwenye kila sekta ya maisha yetu, yaani tuna deni la kuuzaja ulimwengu na utajiri wa kila aina. Hivyo, kila moja wetu anatakiwa kuhakikisha kila anachofanya kichangie kwenye upatikanaji wa utajiri dhidi ya nafsi yake, watu wanaomzunguka na mazingira kwa ujumla.


📌Nihitimishe kwa kusema; Mungu hapendi uwe masikini kwani wavivu na masikini wa fikra hawana nafasi katika makao yake.

📌Tumeumbiwa utajiri na tukapewa mamlaka ya kuumba na kutawala vitu vinavyoujaza ulimwengu hila tunashindwa kufanya hivyo kwa wingi kutokana na kukosa maarifa. Ardhi, maji na viumbe vyote vya kila aina ni miongoni mwa mmiliki yetu kwa ajili ya kutengeneza na kuishi maisha ya utajiri.

📌Je! Upo tayari kuishi maisha ya utajiri? Anza kwa kuhakikisha unakusanya maarifa sahihi kuhusu nafsi yako, watu wanaokuzunguka na mazingira kwa ujumla.


📌Kujifunza zaidi kuhusu misingi ya maisha toshelevu jinyakulie nakala ya kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI.


📌Katika kitabu hiki utajifunza vitu vya msingi ambavyo unatakiwa kufanya ili kuishi maisha yenye kuacha alama. 


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com


Kupata Mafundisho Haya Kwa Barua Pepe, Jiunge na Mtandao wa Fikra za Kitajiri 

* indicates required 

onclick='window.open(