NENO LA SIKU_FEBRUARI 12/2022: MUHIMU! Fahamu Jinsi Unavyojikwamisha Kupitia Mfumo Wako wa Fikra
๐Rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao ya Fikra za Kitajiri, naamini unaendelea vyema na majukumu yako ya siku ya leo. Ni siku muhimu ambayo naamini ukiitumia vyema itachangia kwenye ukamilisho wa mahitaji muhimu ya maisha yako. Hakuna muujiza mwingine wa kufanikisha ndoto za maisha yako zaidi ya kutumia kila muda wa maisha yako kutekeleza matendo yanayochangia kwenye ukamilisho wa mahitaji ya msingi kwenye kila sekta ya maisha yako.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
๐Karibu tena katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha dondoo muhimu kuhusu jinsi unavyoweza kuharibu au kuboresha maisha yako kupitia mfumo wako wa fikra. Moja ya tofauti kuu kati ya mwanadamu na viumbe wengine ni mfumo wake wa fikra. Wakati mwingine mfumo huu hutafsiriwa kama akili kwa kuwa unahusika na matukio yote ya akili ya mwanadamu. Mfumo wa akili ya mwanadamu unaundwa na sehemu zinazohusika na fikra, mawazo, kumbukumbu, utashi na hisia. Vyote hivi, humwezesha mwanadamu kuamua hali ya maisha ya mwanadamu kupitia mtazamo, uzoefu wa furaha na maumivu, imani, hamu, nia na hisia.
๐Tunaweza kuona kuwa mfumo wa fikra ni chombo muhimu cha kuamua aina ya maisha kwa kila mwanadamu. Kupitia mfumo wa fikra unaweza kufanikisha kila hitaji la maisha kama vile mafanikio ya kibiashara, mahusiano, kazi au kiroho. Yote hayo yanawezekana kutokana na ukweli kuwa chochote unachotaka kufanikisha maishani mwako ni lazima kianzie kwenye mfumo wako wa fikra. Hata hivyo, kiwango cha mafanikio ya hitaji husika hutegemea ni kwa jinsi gani utaweza kukubali au kukataa hitaji hilo kwenye akili yako. Hivyo, fikra zinaumba mwonekano wako wa nje kupitia tabia, imani na matendo katika maisha yako ya kila siku.
๐Chochote ambacho hupewa kibali na mfumo wa fikra, ni dhahiri kitajidhihirisha katika maisha yako. Kile unachowaza muda mwingi katika akili yako kuna uwezekano mkubwa wa kujidhihirisha katika uhalisia wake na kinyume chake ni sahihi. Kupitia ukweli huu, mfumo wako wa fikra unaweza kuvuta watu, fursa au kufanikisha kila hitaji lako ikiwa upo tayari kufundisha akili ikubali kuona ukifanikisha hitaji husika.
๐Hata hivyo, ili ufanikishe kila hitaji la maisha yako kupitia mfumo wa akili ni lazima akili yako ijikite kwenye mtazamo chanya, yaani hali ya kuamini kuwa kila kitu kinawezekana. Yale yote ambayo umefanikiwa maishani mwako ni kwa kuwa mfumo wako wa akili uliona na kukubali kuwa jambo husika lipo ndani ya uwezo wako. Na yale ambayo hadi sasa unaangaika kufanikisha ni kwa vile akili yako bado ina wasiwasi juu ya uwezo ulionao kwenye kukamilisha hitaji husika. Ikiwa bado huamini kuwa unaweza kuvuta au kufanikisha hali fulani maishani mwako ni ngumu akili yako kufungua milango ya ukamilisho wa hitaji hilo.
๐Kila siku unajiumba kupitia yale unayoyawaza kwa muda mrefu. Ikiwa mfumo wako wa fikra unatawaliwa na huzuni, hofu, kutokujikubali, kuamini haiwezekani, hasira au wivu; ni dhahiri kuwa hayo ndiyo yanatawala maisha yako. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, fikra huleta hisia, ambazo huzaa tabia na tabia huzaa vitendo na kupitia vitendo tunapata mwonekano wako halisi. Hivyo ikiwa unahitaji kuacha tabia fulani au kujifunza tabia mpya huna budi kwenda kwenye chanzo, yaani kwenye fikra. Unaweza kutumia mbinu hiii kupambana na hisia za hofu, chuki, wivu, wasiwasi au kutojiamini.
๐Nihitimishe kwa kusema; ubora wa maisha yako unategemea ubora wa fikra zako. Ikiwa mfumo wako wa fikra umejazwa na maovu, wasiwasi na kila aina ya matukio au hali hasi ni dhahiri kuwa unaendelea kujirudisha nyuma kimaisha. Hivyo, nakushauri uifundishe akili yako kutafuta upande chanya katika kila hali unayopitia. Pia, ni muhimu kutambua kuwa kadri unavyoanza kuishi maisha yenye fikra chanya kuna upande mmoja wa fikra zako ambao hautakuruhusu kirahisi kuachana na mazoea ya awali. Utafanikiwa kuachana na fikra hasi ikiwa upo tayari kujenga utaratibu wa kudumu katika fikra chanya kwa kipindi cha muda mrefu.
KIJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA, JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
onclick='window.open(