USHAURI! Tumia Neno ASANTE Kufukuza Fikra Hasi

NENO LA SIKU_FEBRUARI 17/2022: USHAURI! Tumia Neno ASANTE Kufukuza Fikra Hasi


📌Ni wakati wa kipekee kuona tumepata nafasi ya kuendelea kuvuta pumzi hii ya uhai. Hongera rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa kupata nafasi ya kuendelea kutekeleza majukumu muhimu ya siku ya leo.


📌Karibu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha mbinu moja itakayokuwezesha kuwa na fikra chanya katika maisha yako.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📌Katika moja ya makala za wiki hii nilieleza jinsi ambavyo unaweza kujikwamisha kimafanikio kutokana na kuendekeza fikra hasi. Nilieleza moja ya kundi la watu ambao muda wote uona na kutafsiri mambo hasi kutoka kwa watu, vitu, mazingira, hali au matukio wanayokutana nayo katika maisha yao ya kila siku. 


📌Swali la msingi katika makala ya leo ni: Kwa nini watu wengi hutafsiri zaidi upande hasi katika maisha yao? Zipo sababu nyingi ambazo hupelekea watu kuona na kutafsiri upande hasi wa maisha yao ya kila siku.


📌Katika makala hii tutaangalia tabia ya kutokuwa na shukrani inavyoweza kupelekea mara zote utafisri na kuona ubaya badala ya wema. Wapo watu ambao asubuhi hadi jioni wanashindwa kupata hata jambo moja la kutolea shukrani kwa Muumba wao, sehemu ya kazi au kwa wanafamilia wenzao.


📌Unaposhindwa kupata jambo la kushukuru ni dhahiri kuwa utaona mambo mengi ya kutolea kasoro na madhaifu ikilinganishwa na sifa njema zilizopo katika mambo hayo. Hebu fikiria ni jinsi gani unaweza kubadili fikra zako kutoka kwenye kutawaliwa na fikra hasi kwa kuruhusu angalau kila siku uone au kutafsiri jambo moja jema kutoka kwa mwenza, watoto, mwajiri, mzazi, wafanyakazi wenzio au watu wapya unaokutana nao. 


📌Ni kweli yawezekana unapitia nyakati ngumu katika maisha yako, lakini jiulize katika nyakati hizo ni jambo gani jema unaweza kusema asante na kupelekea kubadilisha mtazamo wako kuhusu maisha unayopitia. Yawezekana unateseka kiuchumi lakini lakini ni kweli hakuna hata jambo moja la kujivunia?


📌Ni kweli yawezekana umatendwa au kufanyiwa mambo ya hovyo na watu wanaokuzunguka, hebu sasa jaribu kujiuliza mambo mangapi mema ambayo umetendewa na watu hao hao na kati hayo ni lipi jambo moja ambalo linatosha kukusukuma kusema asante ili maisha yaendelee. 


📌Ni kweli yawezekana umejaribu mara kadhaa kusimama kiuchumi lakini kila mara unaishia kupata hasara! Hebu jaribu kujiuliza ni jambo gani la msingi ambalo umejifunza kutokana na kujaribu huko na linatosha kukusukuma kusema asante.


📌Toka kuumbwa kwetu tumeumbiwa kusema asante japo ni nadra sana kutambua kuwa tunazungukwa na mambo mengi ambayo tunatakiwa kuyatolea shukrani ikilinganishwa na yale mabaya.


📌Ikiwa tutaruhusu akili yetu kutambua jambo jema kila mara kutoka kwa wanaotuzunguka au nyakati ngumu tunazopitia ni dhahiri tutafanikiwa kuruhusu akili yetu itafsiri mema zaidi ikilinganishwa na mabaya.


📌Kadri utakavyoruhusu akili yako kuona na kutafsiri matukio au hali ambazo unatakiwa kusema kutoa shukrani, utaona kwamba kuna matukio mengi katika maisha yako ambayo umeyachukulia poa.


📌Hebu unapoanza kukata tamaa kuhusu nafsi yako, watu wanaokuzunguka au mazingira yako; jiulize vipi kuhusu afya, marafiki, familia, nyakati za furaha, na nyakati ngumu ambazo umewahi kupitia katika vipindi tofauti vya maisha yako. 


📌Nihitimishe kwa kusema; unaposema asante kuna maana kubwa katika maisha yako. Kadri tunavyoshukuru zaidi ndivyo tunafungua baraka zaidi kujaza ghara la maisha yetu. Hebu kuanzia sasa, kila ukiamka asubuhi anza kwa kusema asante Mungu kwa kuniwezesha kuamka salama, na inapofika jioni tafakari kwa mapana matukio muhimu katika siku husika ambayo una deni la kusema asante.


📌Hebu anza sasa kwa kusema asante kwa mtandao wa Fikra za Kitajiri ambao umeendelea kukulisha chakula cha ubongo pasipo kulipia chochote. Nitafurahi zaidi kusikia ushuhuda wako wa jinsi gani masomo haya yamebadilisha maisha yako.


KIJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA, JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.



onclick='window.open(