Je! Unaogopa Kifo? Fahamu Somo Lililojificha Katika Kifo!

NENO LA SIKU_FEBRUARI 1/2022: Je! Unaogopa Kifo? Fahamu Somo Lililojificha Katika Kifo!

📌Habari ya leo rafiki na mfuatiliaji wa masomo yangu. Ni siku bora ambayo tunaanza mwezi wa pili katika seti ya miezi 12 ya mwaka huu. Hongera kwa kuwa miongoni mwa watu ambao tumefanikiwa kuiona siku hii muhimu katika jitihada za kuboresha maisha yetu.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

📌Katika makala ya leo kwenye mfululizo wa masomo yenye mada zinazolenga kubadilisha mtazamo wetu kuhusu maisha, tutajifunza kuhusu uthamani wa kifo kwenye maisha yetu hapa duniani. Tutakubaliana kuwa kifo ni hitimisho ya safari ya maisha kwenye uso wa dunia kwa kila kiumbe chenye uhai. Pamoja na kwamba kila mwanadamu anatambua kuwa kifo ni njia ya kutenganisha maisha yake katika uso wa dunia na kuingia kwenye maisha mapya, hakuna ambaye ni jasiri dhidi ya kifo. 


📌Katika kutafuta umaana wa maisha, historia ya maendeleo ya mwanadamu inaonesha kuwa dini mbalimbali zimekuwepo kama njia ya kuwezesha wanadamu kuishi kwa kufuata misingi ya imani. Imani hizi hulenga kumuandaa mwanadamu aishi maisha ambayo yatamwezesha kuwa na uhakika wa maisha yajayo, yaani maisha baada ya kifo.  


📌Pamoja na kwamba kila mtu anaogopa kifo, ukweli unabakia kuwa kila mmoja wetu ni lazima ataonja mauti kama njia ya kuhitimisha safari yake hapa duniani. Kuhusu maisha baada ya kifo, inabakia kwenye misingi ya imani kulingana na dini yako. Kumbe! Badala ya kuogopa kifo tunatakiwa kukitazamia kama tukio muhimu kwenye safari ya maisha yetu.


📌Changamoto kubwa iliyopo katika kungojea kifo ni ile ya kutokujua ni lini na wakati gani ukurasa wa maisha yetu utafungwa hapa duniani! Hilo ni swali ambalo si mwanadamu yeyeto katika uso wa duniani hii amepata kufunuliwa majibu yake. Hata hivyo, vifo vinaendelea kutokea kwenye jamii tunayoishi, kama siyo kwenye familia yako, ni kwenye ukoo, kwa jirani au kwenye mtaa/kijiji unachoishi.


📌Kila aina ya kifo ambacho tumeshuhudia katika mazingira tunayoishi mara nyingi huambatana na maswali mengi kuhusu hatima ya maisha yetu. Kumbe, pamoja na huzuni ambayo tunapata kutoka kwa wale wanaokufa, lipo somo ambalo tunatakiwa kujifunza kuhusu kifo kwa kuwa sisi sote ni wafu watarajiwa (Mhubiri 7:2). 


📌Kumbe! Tunatakiwa kutumia hofu ya kifo kama njia ya kuishi maisha yanayozingatia kutenda mema na adili dhidi ya nafsi yetu, jamii inayotunzunguka na viumbe wote kwenye mazingira tunayoishi. Hii inajumuisha kutumia muda wetu hapa duniani kwa kuendeleza na kutumia karama na vipawa ambavyo tumejaliwa toka kuumbwa kwetu ili kuacha alama inayodumu vizazi na vizazi. Hivyo, matendo mema katika jamii yanatakiwa kuwa msingi kwa kila mmoja kujiandalia kifo chema. 


📌Nihitimishe, kwa kusema pamoja na kwamba kila mmoja wetu anaogopa kifo, ni vyema tukatambua kuwa hatuna ujanja wa kukikwepa. Njia pekee ya kungojea kifo ni kuhakikisha tunaishi kila muda tunaopata kana kwamba huo ndo muda wetu wa mwisho duniani hapa, yaani tuishi kwa ukamilifu. Tutende mema na kuishi kwa kuongozwa na busara kana kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kuishi hapa duniani. Tusameheane sisi kwa sisi kwa kuwa chuki na uhasama vina nafasi katika kungojea kifo chema. Pia, tuepuke sana kusogeza mbele mambo kwa kuwa hakuna anayejua dakika inayokuja atakuwa katika hali gani.


PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA BORA HAPA DUNIANI

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.




onclick='window.open(