JE UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Kama Jibu Ni Ndiyo Anza Kuiishi Siri Hii.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 22/2022: JE UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Kama Jibu Ni Ndiyo Anza Kuiishi Siri Hii.



πŸ“ŒNi siku nyingine tumejaliwa pumzi ya uhai. Ni siku ya kutekeleza majukumu ya msingi hasa yale yanayochangia kwenye ukamilisho wa maisha yenye thamani. Naamini unaendelea vyema na majukumu hayo ili siku yako ipate kutumika kwa manufaa.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


πŸ“ŒKaribu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha siri ya kwanza ambayo matajiri wanaitumia kukuza utajiri wao. Jambo la msingi katika mfululizo wa makala hizi ni kutambua kuwa utajiri unatangenezwa kupitia kanuni maalumu ambazo zimeendelea kuwa siri zinazobadilisha maisha ya watu.


πŸ“ŒLeo siri ya kwanza naifikisha kwenye upeo wako wa fikra, wajibu wako ni kuitafakari na kufanya maamuzi mara moja ili upate kuianza safari yako ya utajiri.  


πŸ“ŒKatika makala ya jana nilikushirikisha mbinu ya awali ya kuishi maisha ya kitajiri. Tuliona kuwa utajiri unaanza kwa kuhakikisha matumizi hayazidi kipato chako.


SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Itakayofungua Milango Ya Utajiri


πŸ“ŒNi matarajio yangu kuwa kupitia makala hiyo uliweka mikakati ya kukuwezesha kupunguza matumizi sambamba na kuwa na bajeti inayoendana na pato lako halisi. 


πŸ“Œ Baada ya kudhibiti matumizi yako, Siri ya kwanza itakayobadilisha maisha yako ni "kuhakikisha unatenga angalau kati ya asilimia 10 hadi 20 ya pato lako kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba." 


πŸ“ŒNi kama vile naona jinsi unavyofikiria kichwani kwa kujiuliza nitaweza vipi kutenga asilimia 10 au 20 kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba wakati pato langu lenyewe halitoshi kukidhi mahitaji yangu.


πŸ“ŒNi kuondoe wasiwasi huo kwa kukutaka kwanza ukubaliane na siri hii kuwa inaweza kufanya kazi katika maisha yako kupitia pato lako hilo hilo.


πŸ“ŒKukubaliana na siri hii ni hatua moja muhimu ambayo itakufungua akili na kuweza kuona sehemu zipi katika matumizi yako ambako unaweza kupata asilimia kiasi cha fedha ambayo utaanza kuitenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba. 


πŸ“ŒPia, jambo la msingi ambalo unatakiwa kufahamu kuhusu siri hii ni; matajiri kwanza huwa wanatenga kiasi cha pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba kabla ya kufanya matumizi mengine."


πŸ“ŒUnapoanza safari ya kuishi kwa kuitekeleza siri hii unatakiwa kutambua kuwa kiasi cha pesa unachotenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ni deni kwako ambalo linatakiwa kulipwa kabla ya matumizi mengine yote yanayofanikisha mahitaji yako ya lazima.


πŸ“ŒHebu fikiria jinsi ambavyo hujawahi kukosa hela ya kula, kodi ya nyumba, matibabu au ada ya wanafunzi. Vyote hivyo vimepewa nafasi katika akili yako na ndiyo sababu unatumia kila mbinu kuhakikisha vinatekelezwa kwa ufasaha na kwa wakati.


πŸ“ŒKwa nidhamu na mbinu hizo hizo ndivyo unatakiwa kuhakikisha kila mara kiwango ulichopanga kutenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba kinapatikana na kutengwa tena kabla ya kuanza matumizi mengine.


πŸ“ŒUnaweza kuanza kwa kutenga hata asilimia 5 ya pato lako kwa siku za mwanzoni ili kujenga tabia ya hiyo na kisha ukaendelea kupandisha kiwango hicho kwa kadri uwezavyo.


πŸ“ŒNihitimishe kwa kusema, kutenga bajeti kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ni siri ambayo itabadilisha maisha yako ikiwa utachukua hatua sasa. Hakuna siku ambayo utapata pesa ya ziada kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba zaidi hizi unazopata kwa wakati huu.


πŸ“ŒKadri utavyojenga tabia ya kutenga kiasi kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ndivyo utagundua ulichelewa kuanza kutumia siri hii ambayo itatenda muujiza katika maisha yako.


πŸ“ŒNB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.



KUJIFUNZA MISINGI YA MAISHA YENYE KUACHA ALAMA; PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(