NENO LA SIKU_FEBRUARI 18/2022: MALIPO NI HAPA HAPA! Ijue Sheria Ya Asili Itakayokufungua Kifikra Kuhusu Matendo Dhidi Ya Nafsi Yako Na Wengine
📌Hakika ni jambo la kumshukuru Mungu kuona tumeamka salama na tumeweza kuendelea na majukumu yetu ya siku ya leo. Hongera rafiki yangu kwa siku hii ya leo ambayo naamini umeitumia kama njia ya kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio ya maisha yako.
📌Katika makala ya leo tutaangalia moja ya sheria ya asili ambayo inaendelea kudhibiti matokeo au mafanikio ya mwanadamu kulingana na matendo yake.
📌Ukweli ni kwamba maisha ya mwanadamu katika ulimwengu huu yanaendeshwa na sheria za asili (Universal laws). Sheria hizi zimekuwepo toka enzi za kuumbwa kwa ulimwengu na zinaendelea kuamua mafanikio ya maisha ya kila mmoja wetu.
📌Ni sheria ambazo huwezesha uwepo wa msawazo katika upatikanaji wa haki kwa kila mmoja wetu bila kujali iwapo una ufahamu au hauna ufahamu juu ya sheria hizi. Na ili haki itendeke kwa kila mmoja wetu, asili hutoa adhabu na kuzawadia kila mtu kulingana na matendo yake.
📌Moja ya sheria ya asili muhimu unayotakiwa kuifahamu kadri unavyoishi na watu wengine ni Sheria ya Sababu na Athari (The Law of Cause and Effect). Sheria hii pia hujulikana kama Karma ambalo ni neno ambalo hutumika kwenye mafundisho ya dini za bara la Asia.
📌Ni sheria inayowezesha mwanadamu azawadiwe au kuadhibiwa kulingana na matendo yake. Kupitia sheria hii tunaambiwa kuwa, “kwa kila hatua au tendo tunalofanya huzalisha nishati yenye athari ambayo huzunguka katika ulimwengu, kama vile nuru ya mwanga unavyosafiri kuelekea upande mmoja.”
📌Hivyo, kila hatua au tendo la mwanadamu katika ulimwengu huchangia kwenye kuubadilisha ulimwengu kwa njia hasi au chanya. Kadri matendo hasi yanavyoongezeka ndivyo na wanadamu wanazidi kuadhibiwa kutokana na matendo yao.
📌Jambo la msingi ambalo unatakiwa kulifahamu kuhusu sheria hii ya asili ni kwamba, toka siku mwanadamu anapoumbwa akaunti ya matendo yake hufunguliwa na chochote anachofanya huingia kwenye akaunti hiyo, na kuna uwezekano wa matendo hayo kumrudia katika maisha ya sasa (maisha ya hapa duniani) au maisha ya baadae (maisha baada ya kifo).
📌Katika hilo, ni vyema pia kutambua kuwa matendo yako yanaathiri kila kitu na kila mtu ambaye yupo karibu nawe na nishati hiyo inaendelea kuwaathiri wengine zaidi ya hapo.
📌Hivyo, kadri unavyotoa nishati chanya kwa ajili ya kuubadilisha ulimwengu ndivyo utapokea sawa, na ikiwa utaujaza ulimwengu na nishati hasi ndivyo utaadhibiwa kwa kipimo kile kile. Ukitenda jema ulimwengu utakulipa jema, vivyo hivyo ukitenda baya ulimwengu utakuwajibisha kwa ubaya ikitengemea jinsi ulivyotafsiri tendo lako.
Ili uelewe zaidi kuhusu sheria hii jinsi inavyofanya kazi katika maisha yetu ya kila siku nitatumia mifano ifuatayo;
📌Fikiria umeenda kununua bidhaa dukani vyenye thamani ya Tshs. 5,000/=, umefika kwa muuza duka na kumpatia noti ya shilingi elfu kumi. Muuza duka badala ya kukurudishia elfu tano kama chenji amekuzidishia zaidi na haraka haraka unagundua na kuondoka.
📌Kwa kipindi hicho utajiona mjanja, hila Ulimwengu kupitia asili unarekodi tendo hilo. Maisha yanaendelea kama kawaida, baada ya siku unashangaa umepoteza hela au kitu cha thamani au kupatwa na tatizo ambalo linapelekea hutumie fedha pengine zaidi ya kiasi ulichodhurumu kwa muuza duka.
📌Katika hali ya kawaida utaishia kumlilia Mungu au kulalamika kwa kadri uwezavyo hila hutakumbuka kuwa umelipwa kwa vile ulishindwa kumtendea wema muuza duka.
📌Mfano, mwingine fikiria wewe ni muuza duka ambaye unapenda kudhurumu wateja wako labda kupitia vipimo visivyo sahihi (utaratibu wa kutumia kwa makusudi mizani inayopunja), unaweza kutumia utaratibu huu kwa muda mrefu na ukajiona mjanja sana na maisha yakaendelea!
📌Siku moja bila kutarajia anafika mteja ambaye ni miongoni mwa wadhibiti vipimo (Wakala wa Vipimo) anakuwekea mtego na unanasa, ili kukidhi matakwa ya sheria unatakiwa kulipa faini na kubadilisha mzani wako hali ambayo inapekelea kutumia kiasi kikubwa cha pesa pasipo kutarajia!
📌Hivyo ndivyo sheria ya asili ya Chanzo na Kisababishi inavyofanya kazi katika maisha yetu.
📌Kumbe, sisi ni waumbaji wa mbingu au kuzimu hapa duniani. Tunaweza kuzalisha laana au baraka kwa maisha yetu na kizazi chetu kupitia matendo yetu ya kila siku.
📌Kadri unavyoujaza ulimwengu na matendo mema dhidi ya nafsi yako, watu wanaokuzunguka na mazingira kwa ujumla ndivyo asili inakuzawadia zaidi na zaidi.
📌Hata hivyo, hauwezi kuujaza ulimwengu na nishati yenye athari chanya ikiwa akili yako inatawaliwa na nishati hasi kuhusu ulimwengu na vyote vilivyomo.
📌Ni hitimishe kwa kusisitiza kuwa; malipo ni hapa hapa, kama siyo kwako wewe mwenyewe itakuwa kwa wapendwa wako. Ili kuendana na matakwa ya asili hatuna budi kuwatendea wengine kama ambavyo tungetamani kutendewa.
📌Baada ya kufahamu kuhusu sheria hii ni vyema, kila unapowaza kutenda jambo lolote dhidi ya nafsi yako, watu wengine au mazingira kwa ujuma tumia dakika kadhaa kujiuliza kuhusu athari ya hatua zako.
📌Ikiwa kupitia tafakari hiyo ukajiridhisha kuwa jambo husika lina athari hasi nyingi ikilinganishwa na athari chanya huna budi kuliweka pembeni na kutafuta mbadala.
📌Kujifunza zaidi kuhusu sheria nyingine za asili na jinsi zinavyodhibiti mafanikio ya maisha yetu jinyakulie nakala ya kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI.
📌Katika kitabu hiki utajifunza sheria za asili saba na jinsi kila sheria inavyoshikilia mafanikio ya maisha yako.
WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
onclick='window.open(