Hongera rafiki yangu kwa siku ya leo. Naamini siku hii imeitumia kwa faida kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yako. Hata kama kuna changamoto kadhaa umekutana nazo husife moyo na badala yake jipe moyo mkuu kwa ajili ya kuendelea kusonga mbele.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
Karibu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha siri nyingine ambayo itakuwezesha kukuza utajiri wako.
Makala zilizopita nilikushirikisha siri ya kwanza ya kutengeneza utajiri ambapo nilikutaka kuhakikisha unatenga kati ya asilimia 10 hadi 20 ya pato lako. Kupitia siri hiyo nilikushirikisha umuhimu wa kutenga bajeti binafsi inayoendana na pato lako halisi.
Kupitia siri ya kwanza tunapata siri ya pili ambayo matajiri hutumia kukuza utajiri wao. Siyo mara kwanza kuandika kuhusu siri hii, hila kwa kuwa kipindi hiki nimedhamiria kukushirikisha siri zote za kukuza utajiri wako inabidi nirudie tena kukumbusha.
Siri hii inasema; "kabla ya kutumia unatakiwa kutenga pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba." Siri hii hujulikana pia kama "KUJILIPA KWANZA."
Nilijifunza siri hii kupitia vitabu viwili vya Robert Kiyosaki (Rich Daddy, Poor Daddy na Rich Daddy's Conspiracy of Rich).
Hata hivyo, siri hii imeandikwa kwenye vitabu vingi vya uhamasishaji wa mafanikio japo ni watu wachache sana wanaotumia siri hii.
Kutokana na hilo, haishangazi kuona idadi ya matajiri katika jamii ni ndogo ikilinganishwa na masikini au watu pato la kati. Kadri unavyoifahamu siri hii na kuitumia mapema ndivyo itatenda muujiza kiasi cha kujuta kwa nini umekuwa ukijichelewesha mwenyewe.
Kujilipa kwanza si kingine zaidi ya kuhakikisha kila shilingi inayoingia mikononi mwako unatenga asilimia maalumu kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba.
Katika siri ya kwanza tuliona kuwa inashauriwa kiasi unachojilipa kiwe kati ya asilimia 10 hadi 20.
Kwa wale ambao wameajiriwa katika sekta rasmi wanaweza kutengeneza mfumo wa moja kwa moja (automatic system) ambao unawezesha kiasi cha kujilipa kwanza kiingizwe kwenye akaunti maalumu ya Uwekezaji na Akiba bila kuingizwa kwenye akaunti ya mshahara.
Hata hivyo, haizuii kuhakikisha wanajilipa kwanza kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwao nje ya mshahara.
Pia, Wafanyabiashara nao wanaweza kujilipa kwanza kwa kuhakikisha kila mwezi wanatenga pesa ya Uwekezaji na Akiba kabla ya matumizi mengine.
Kwa nini siri hii ni mkombozi kwako?
Wakati ambao unaendelea kuhoji kuhusu umuhimu wa siri hii kwenye maisha yako, naomba uwe mkweli kujibu maswali haya;
Je, una akiba kiasi gani? Je, leo hii ukipata dharura ya kawaida unaweza kuitatua bila mkopo au bila utegemezi kutoka kwa watu wengine?
Je, ikitokea unaachishwa kazi au unashindwa kuendelea na kazi ikiwa ni miongoni mwa watu wengi ambao ili wape mkate ni lazima watoke na kufanya kazi utaweza kumudu gharama za kuishi?
Kama majibu ya maswali hayo ni HAPANA au una WALAKINI, Siri ya JILIPE KWANZA imefika tena mezani mwako!
Mtu yeyote ambaye hana utaratibu wa kutenga akiba, ni dhahiri kuwa hana pesa za kutosha kwa matumizi ya siku zijazo.
Siri ya kujilipa kwanza inataka ikuondoe kwenye kundi la watu wa aina hiyo. Ukiachana na dharura, kuna fursa ambazo utazikosa kwa kuwa huna Akiba ya kutosha.
KUJILIPA KWANZA ni kanuni ya dhahabu itakayowezesha kuwa na akiba yenye kuongezeka kulingana na ongezeko la pato lako.
Ili uweze kutumia Kanuni hii kwa faida, unachotakiwa kufanya ni kujitoa kila mara kutenga akiba kabla ya kutumia.
Kabla ya kulipa bili zako, kununua chakula, kulipa ada ya watoto wako, au kulipia king'amuzi cha TV unapaswa KUJILIPA KWANZA.
Kiwango unachojilipa inabidi iwe ni bili ya kwanza ambayo lazima uilipe na kisha ndiyo upange matumizi mengine.
Kufanikisha hilo, unapaswa kuongozwa na nidhamu binafsi.
Siri hii inaweza kuonekana rahisi lakini kama hauna nidhamu binafsi hutofanikiwa kujilipa kwanza.
Nidhamu binafsi ndiyo nyenzo ambayo itakuwezesha kuona kiasi unachojilipa kama deni tena ambalo husipolipa madhara yake ni makubwa.
Nihitimishe kwa kusema; nje ya siri hii kukuwezesha kukuza utajiri wako, kuna faida nyingi unapoamua siri hii iwe sehemu ya maisha yako.
Moja, kupitia kujilipa kwanza utakuwa na uhakika na mwendelezo wa kutenga akiba.
Pili, kujilipa kwanza ni njia bora ya kutenga akiba kwa ajili ya kuwezesha manunuzi makubwa kwa kadri ya mpango wako, ujenzi au kutenga akiba ya kusomesha watoto wako.
Tatu, kwa kujilipa kwanza unaweza kukusanya mtaji wa biashara.
Nne, kwa kujilipa kwanza unaweza kutenga fedha kwa ajili ya kipindi chenye mahitaji makubwa ya pesa kama vile nyakati za likizo au kutembelea sehemu kufurahi maisha na familia.
NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.
WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.