Fahamu Kauli Ambazo Zimekuwa Zikikuzuia Kuishi Maisha Kwa Ukamilifu

NENO LA SIKU_FEBRUARI 6/2022: Fahamu Kauli Ambazo Zimekuwa Zikikuzuia Kuishi Maisha Kwa Ukamilifu


Habari ya wakati huu rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo yanayotolewa na mtandao wa Fikra za Kitajiri. Ni muda mwingine katika siku mpya ambayo tumezawadiwa kwa ajili ya kuendeleza jitihada za kuwa bora zaidi.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


Karibu katika makala fupi ambayo inalenga kukufunulia jinsi ambavyo umekuwa ukipoteza nafasi ya kuishi maisha ya ukamilifu kwa kuendekeza kauli kandamizi. Kupitia makala zinazotolewa na mtandao huu nimekuwa nikikusisitizia umuhimu wa kuishi kana kwamba hakuna wakati ujao. Hali hii inatokana na ukweli kuwa ni Mungu pekee mwenye kujua matukio ya wakati ujao kwa kila mmoja wetu. Hata hivyo, ieleweke kuwa simaanishi maisha yako hayapaswi kuzingatia mipango ya wakati ujao. 


Kupitia makala hii naendelea kukumbusha kuwa huna budi kutambua hakuna maisha zaidi ya haya. Mara nyingi unashindwa kuishi maisha ya ukamilifu kwa kutegemea ipo kesho iliyo bora zaidi ya leo. Moja ya kauli kandamizi ambazo zinakuzuia kuishi kwa ukamilifu ni zile zinazohusisha maneno kama vile: “Nikiwa….”, “Nikifanikiwa….”, “Nikifikisha….”, “Kama ninge…..”, “Haiwezekani …..”, “Sina….”. Hizi ni baadhi tu ya kauli ambazo zinakuhamisha kutoka kwenye mazingira au hali ya wakati uliopo na kukuaminisha kuwa kuna jambo za ziada ambalo unalingojea litokee maishani mwako.


Kupitia kauli kama hizo umekuwa ukisogeza majukumu na matendo muhimu ambayo yangeweza kufanyika kulingana na hali au mazingira ya wakati husika. Mfano, fikiria jinsi ambavyo mara nyingi umekuwa ukisogeza hisia za furaha, upendo na faraja kwa kuwa unahusianisha vyote hivi na hali ya kipato, familia, mazingira au jamii kwa ujumla. Fikiria jinsi ambavyo mara kadhaa umeshindwa kuwa msaada kwa wengine kwa kudhania kuwa kwa sasa hauna kitu cha kusaidia, japo unasahau kuwa msaada si lazima uwe pesa au vitu. Fikiria jinsi ambavyo umeshindwa kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya kuwa karibu na wapendwa wako, kwa unadhania kuwa ipo siku utakuwa na muda zaidi kuliko ilivyo sasa. Fikiria jinsi ambavyo watoto wako wanakosa malezi sahihi kutokana na kudhania kuwa wakiwa wakubwa ndiyo utaweza kuwafunda zaidi.


Nihitimishe kwa kusema kuwa, hii ni baadhi ya mifano michache tu kati ya mambo mengi ambayo umekuwa ukisogeza mbele katika maisha yako ya kila siku. Jambo ambalo nataka utambue ni kwamba: “ubora wa maisha yako haupimwi kwa urefu wa muda unaoishi bali vitu unavyotenda kwa manufaa yako, jamii inayokuzunguka na mazingira katika kipindi unachoishi.” Kila unaposogeza mbele baadhi ya majukumu kwa kudhani labda bado mdogo au kipato chako bado hakiruhusu, unajinyima fursa ya kutimiza majukumu husika katika kipindi hicho. 


PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA BORA HAPA DUNIANI

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.




onclick='window.open(