UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 23/2022: Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.  
📌Habari rafiki yangu na hongera kwa kuendelea kufuatilia masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini masomo haya yamesaidia kukubadilisha kifikra na kivitendo.

📌Siku ya leo nahitaji kusikia ushuhuda wako. Nitumie ujumbe ukielezea jinsi ambayo masomo yangu yamesaidia kubadilisha maisha yako. Unaweza kutuma ujumbe wako kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au WhatsApp namba +255 786 881 155. Ujumbe wako ni muhimu sana katika kufanikisha uendelevu wa masomo haya. 

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

📌Katika makala ya jana tulijifunza siri ya kwanza ya kutengeneza utajiri wa ndoto yako. Tuliona kuwa siri hiyo inahusisha kutenga kati ya asilimia 10 hadi 20 kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba.


📌Hata hivyo, niligusia kuwa hauwezi kufanikisha kutenga pesa kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba ikiwa hauna utaratibu maalumu wa kudhibiti mapato yako. Katika hilo, niligusia kuwa njia pekee itakayokuwezesha kudhibiti matumizi yako ni kuhakikisha unakuwa na bajeti ya matumizi inayoandaliwa kulingana na uhalisia wa pato lako.

📌Makala ya leo inalenga kukufungua kuhusu bajeti na gani vitu vya msingi vya kuzingatia wakati unaandaa bajeti yako.

📌Je! Bajeti ni nini? Bajeti ni mpango wa matumizi unaoandaliwa kwa ajili ya kutoa dira ya matumizi ya kila shilingi kwenye pato lako. Bajeti uandaliwa kwa kipindi maalumu kama vile siku, wiki, mwezi au mwaka.

📌Mfano, ikiwa pato langu kwa mwezi baada ya kutoa kodi ya pato (pay as you earn) ni Tshs. 500,000.00; bajeti binafsi inatakiwa inipatie mwongozo wa jinsi gani natakiwa kusambaza kiasi hiki katika matumizi mbalimbali kama vile; mahitaji ya chakula, kodi ya nyumba, ada ya wanafunzi, bima ya afya au bima ya kinga ya mali dhidi ya ajali, kulipa madeni kama yapo, na matumizi ya starehe au tunaweza kutumia jina la matumizi yasiyo ya lazima.

📌Je! Ni mbinu ipi niitumie kurahisisha upangaji wa bajeti binafsi? Kabla ya kuandaa bajeti binafsi unatakiwa kufanya jambo hili la msingi.

📌Hakikisha unakokotoa pato lako halisi kwenye kila mfereji wako wa mapato katika kipindi maalumu cha bajeti yako. Yaani, hakikisha unafahamu pato lako kwa mwezi au wiki kulingana na urefu wa kipindi unachobajetia. Kama ni kwa mwaka hakikisha unatambua makadirio ya mapato yako kwa mwaka.

📌Baada ya kuwa na makadirio halisi ya pato lako kwa kipindi maalumu cha bajeti unaweza kutumia kanuni iliyopendekezwa na aliyekuwa Senator wa US Elizabeth Warren na binti yake Amelia Warren Tyagi katika kitabu cha kijulikanacho kama "All Your Worth: The Ultimate Lifetime Money Plan.” 

📌Kanuni hii inajulikana kama 50/30/20, ikamaanisha kuwa; 50% ya pato pako lako inatakiwa kutengwa kwa ajili mahitaji ya lazima (basic needs).

📌Tenga 30% ya pato lako kwa ajili ya mahitaji ya ziada au starehe au mahitaji yasiyo ya lazima. Haya ni mahitaji yote ambayo pindi unapoyakosa hauwezi kushindwa kuendelea kuishi.

📌Kisha tenga 20% ya pato lako kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba. Pia, kundi hili la 20% sehemu inaweza kuelekezwa kwenye kulipa madeni ikiwa una madeni na sehemu nyingine itengwe kwa ajili ya kurudisha kwenye jamii (sadaka kwa wahitaji). Mara nyingi inashauriwa 10% ya pato lako (kundi la kumi) ndo itengwe kwa ajili ya kurejesha kwenye jamii.

📌Unaweza kuwa mjanja kwa kuongeza bajeti katika kundi hili kwa kupunguza bajeti katika kundi la pili (punguza kwenye 30%). Yaani unaweza punguza matumizi yasiyo ya lazima na kuongezea kwenye kundi la Uwekezaji na Akiba.

📌Nihitimishe kwa kusema; utaratibu wa bajeti binafsi ni njia pekee ambayo itakuwezesha kujua sehemu ambazo zinakwamisha pato lako kuongezeka.

📌Kufanikisha hilo ni lazima ujenge tabia ya kudhibiti na kuepuka matumizi ya hovyo. Husinunue vitu ambayo havina tija kwako na epuka kununua kwa hisia.

📌Kununua kwa hisia mara nyingi hujumuisha kununua wakati ambao umefurahi, kukasirika au kushawishiwa kupitia mbinu za wauzaji. Anza sasa na kumbuka kunishukuru kwa maarifa haya.

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(