UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Zaidi Kanuni Ya 50/30/20

NENO LA SIKU_FEBRUARI 24/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Zaidi Kanuni Ya 50/30/20.  



📌Hongera rafiki kwa kufanikiwa kuendeleza jitihada za kuboresha maisha yako. Ni siku nyingine ambayo umezawadiwa kwa ajili ya kuendeleza bidii zinazolenga kupata matokeo chanya katika kila sekta ya maisha yako.


📌Ninafurahi kusikia ushuhuda wako. Nitumie ujumbe ukielezea jinsi ambayo masomo yangu yamesaidia kubadilisha maisha yako. Unaweza kutuma ujumbe wako kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au WhatsApp namba +255 786 881 155. Ujumbe wako ni muhimu sana katika kufanikisha uendelevu wa masomo haya. 

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📌Karibu katika makala ya leo ambayo ni mwendelezo wa kujifunza kuhusu jinsi gani unaweza kutenga bajeti binafsi.


📌Makala ya leo ni mwendelezo wa makala ya jana hasa kwenye jinsi gani unaweza kutumia Kanuni ya 50/30/20 kuratibu matumizi ya pato lako.


SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Kubajeti Pesa Zako.


📌Kuelewa vizuri jinsi unavyoweza kutumia Kanuni hii katika kudhibiti matumizi yako huna budi uelewe maneno haya; 'Needs'; 'Wants' na 'Savings/Investments'. 


📌NEEDS - Katika makala ya jana nilitumia maneno ya kiswahili "matumizi ya lazima" kujumuisha matumizi yote yanayoingia ndani ya kundi hili.


📌Kwa ujumla, haya ni matumizi ambayo ni ya lazima katika kufanikisha uendelevu wa maisha yako.


📌Haya ni matumizi ambayo huwezi kuyakwepa, yaani pasipo gharama hizo huwezi kuishi au utakosa haki zako za msingi.


📌Matumizi haya yanaweza kujumuisha; 

  • Kodi ya kila mwezi,

  • Bili za umeme na maji

  • Usafiri

  • Bima (afya, gari, au kipenzi)

  • Chakula na vinywaji vya lazima

  • Ada za wanafunzi

  • Kulipia madeni ya lazima kama vile mikopo ya benki au SACCOS, Loan Boards n.k


📌Ikiwa unatumia Kanuni ya 40/30/20 kupanga bajeti binafsi, kundi hili linatakiwa kutengewa 50% ya pato lako baada ya kodi.


📌WANTS - Kwenye  makala ya jana nilitumia maneno "matumizi yasiyo ya lazima, starehe au matumizi ya ziada".


📌Katika kundi hili kuna matumizi yanayokufanya ufarahie kuishi. Ni matumizi ambayo siyo lazima yapatikane ili uendelee kuishi. Unaweza kukosa matumizi haya na maisha yako yakaendelea kama kawaida.


📌Ni kundi linalojumuisha matumizi kama vile:-

  • Mtoko wa kifamilia kwa ajili ya chakula cha jioni au kuburudika zaidi

  • Manunuzi ya nguo mpya

  • Vifurushi vya kuangalia chaneli za TV au vifurushi vya simu

  • Unywaji wa vilevi katika kumbi za starehe

  • Vyakula vya bei ya gharama

  • Manunuzi kwenye maduka gharama


📌Njia rahisi ya kutofautisha 'needs' na 'wants' ni kujiuliza hivi nikikosa kulipia huduma hii nitashindwa kuendelea na maisha? Au mara zote jiulize, Je! ni upi mbadala wa huduma hii? 


📌Mfano, kama nimezoea kununua nguo kwenye duka ambalo gharama ipo juu, unaweza kununua nguo ya ubora huo huo kwenye maduka ya hadhi ya kawaida.


📌Badala ya kwenda kula chakula hoteli ya gharama, kula kwenye hoteli yenye hadhi ya kawaida. Kwa kufanya hivyo unaweza kuokoa ongezeko la zaidi ya asilimia 20 kwenye manunuzi ya mwezi.


📌KWA mujibu wa Kanuni ya 50/30/20 tuliona kuwa kundi hili linatakiwa kutengewa asilimia 30 ya pato lako. Hila katika makala ya jana tuliona kuwa unaweza kupunguza gharama katika kundi hili na kuongeza kwenye kundi la Uwekezaji na Akiba.


📌SAVINGS/INVESTMENTS - Kwenye makala ya jana nilitumia maneno "Uwekezaji na Akiba" kuelezea matumizi katika kundi hili. Ni kundi muhimu kwa ajili ya kukuza pato lako, yaani kukuza utajiri wako.


📌Katika kundi hili unatakiwa kutenga bajeti itakayokuwezesha kuwa na akiba kwa ajili ya fursa za uwekezaji zinazoweza kujitokeza. Hata hivyo, unatakiwa kuhakikisha fursa hizo ziwe zinaendana na Mpango wako wa Uwekezaji.


📌Pia, kundi hili linajumuisha akiba kwa ajili ya matukio ya dharura au siku ambazo unaweza kushindwa kuendelea kufanya kazi. Hivyo, unaweza kutumia kundi hili kufanya maandalizi siku ambazo hutashindwa kufanya kazi au pindi utakapostaafu.


📌Ni kundi ambalo unatakiwa kuwa na mpango wa Uwekezaji wa muda mfupi (mwezi, mwaka) na muda mrefu (miaka mitano na kuendelea). 


📌Zaidi ya yote, katika kundi hili takribani 10% ya pato lako (50% ya kundi hili) inatakiwa itengwe kwa ajili ya  kurudisha kwenye jamii kwa njia ya sadaka.


📌Inashauriwa pesa unayotenga kwa ajili ya Uwekezaji na Akiba iwekwe kwenye akaunti maalumu ya Akiba/Uwekezaji au iwekezwe kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja, kwa hapa kwetu unaweza kuwekeza katika Mifuko ya UTT AMIS.


📌Baada ya ufafanuzi wa kina kuhusu Kanuni ya 50/30/20 unachotakiwa kufanya hatua ya kwanza ni kujua pato lako halisi baada ya kuondoa kodi katika kipindi maalumu cha bajeti yako.


📌Kama wewe ni mfanyabiashara, hakikisha unajua faida yako kwa kipindi hicho maalumu baada ya kuondoa kodi ya Serikali, pango la framu gharama za wasaidizi. Kiasi kinachobakia ndilo pato halisi unalotakiwa kuliingiza kwenye Kanuni ya 50/30/20.


📌Kama umeajiriwa katika sekta rasmi, kwako ni rahisi maana pato lako ni pesa halisi baada ya makato inayoingizwa kwenye akaunti yako ya benki kila mwisho wa mwezi (take home).


📌Hata hivyo, kuna makato ambayo unatakiwa uyarejeshe kwenye pato lako kabla ya kuingiza kwenye Kanuni. Mfano, makato ya bima ya afya, malipo ya mikopo ya madeni makubwa ya benki au Loan Board.


📌Baada ya kupata pato lako halisi hatua inayofuata ni kuingiza kwenye Kanuni ya 50/30/20. Kumbuka, malipo ya madeni makubwa au bima ambayo umeyarejesha kwenye pato lako yanatakiwa yaingizwe katika kundi la kwanza, yaani kundi la matumizi ya lazima (50%).


📌Hatua ya pili baada ya kutambua pato lako halisi katika kipindi maalumu cha bajeti ni kugawanya matumizi yako kulingana na makundi matatu tuliyojifunza hapo juu, yaani needs, wants na Savings/investments.


📌Kufanikisha zoezi hili, unaweza kupitia matumizi yako kwa miezi ya iliyopita. Angalia ni matumizi yapi huwa yanajirudia katika miezi kadhaa na tambua kila tumizi linaangukia kwenye kundi lipi kati ya makundi matatu.


📌Baada ya zoezi hili unatakiwa kufahamu kiasi cha pesa kinachotumika kugharamia Chakula, Afya, Kodi, Ada, Ankara za maji na umeme, usafiri, mawasiliano, malipo ya ving'amuzi au starehe.


📌Kisha tenga matumizi yote uliyoainisha katika makundi matatu; mahitaji ya lazima, mahitaji ya ziada au Uwekezaji na Akiba. 


📌Hatua ya mwisho, tathimini ni sehemu zipi unapaswa kurekebisha ili upate kukidhi matakwa ya Kanuni ya 50/30/20 kwa ufasaha.


📌Njia bora ya kufanya hivyo ni kutathmini ni kiasi gani unatumia kwa kila kundi kutoka kwenye tathimini ya matumizi uliyofanya kwa miezi iliyopita.


📌Hakikisha 50% ya pato lako inatengwa kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya lazima, 30% au pungufu itengwe kwa ajili ya mahitaji ya ziada, na 20% ielekezwe kwenye akaunti maalumu ya Uwekezaji na Akiba.


📌Nihitimishe kwa kukumbusha kuwa, Kanuni ya 50/30/20 hurahisisha upangaji bajeti kwa kugawa mapato yako ya baada ya kodi katika makundi matatu ya matumizi: mahitaji ya lazima, mahitaji yasiyo ya lazima na Uwekezaji au Akiba.


📌Kujua ni kiasi gani cha kutumia kwa kila kundi kutarahisisha kudhibiti matumizi yako na kuwezesha kuondoa matumizi ya hovyo. 


📌NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 


Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(