Amka Rafiki! Acha Kuchukulia Poa Maisha Yako.

NENO LA SIKU_FEBRUARI 7/2022: Amka Rafiki! Acha Kuchukulia Poa Maisha Yako.


📌Habari rafiki yangu mpendwa ambaye umeendelea kuwa mfuatiliaji wa makala za mtandao wa Fikra za Kitajiri. Ni matarajio yangu kuwa upo vizuri na unaendeleza mapambano kwa ajili ya kuishi maisha yenye kujikita kwenye kusudi halisi la Muumba wako.


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

📌Karibu tena katika makala ya leo ambao nitakushirikisha umuhimu wa kutochukulia poa maisha yako. Unapoanza kusoma makala hii natamani uanze kwa kutambua kuwa uhai ulionao ni wa thamani kuliko kitu chochote ambacho umewahi kufikiria ni cha thamani maishanu mwako.


📌Ni bahati mbaya sana kuona maisha ya mwanadamu hapa duniani kwa wastani yameshindwa kufikia kilele cha kuchanua na kuzaa matunda hai. Jamii inakosa vitu vya thamani ambavyo ni matunda ya kukomaa na kuchanua kwa kilele cha uwezo halisi wa mwanadamu kupitia maisha yake hapa duniani. Hali hii ni zao la Jamii zetu kuwa na idadi kubwa ya watu ambao kila kukicha wanachukulia poa maisha yao.


📌Ni kwa bahati mbaya sana kuona Jamii zetu kwa karne hii ya 21 zina idadi kubwa ya watu ambao wanaishi bila kutambua kwa nini wanaishi na wanaishi kwa ajili ya kukamilisha nini hapa duniani. Kwa nini unaishi na unaishi kwa ajili ya kukamilisha nini hapa duniani ni maswali mawili ambayo yanakutaka kutathimini kwa nini hadi sasa upo hai na uhai wako ni kwa ajili ya ukamilisho wa kitu gani. 


📌Ni kwa bahati mbaya sana kuona mpaka sasa Jamii zetu zina idadi kubwa ya watu ambao wanaishi pasipo kutambua kusudi halisi la maisha yao. Ikiwa hadi sasa unaishi bila kutambua umeumbwa kwa ajili ya kukamilisha nini hapa duniani ni wazi kuwa bado unachukulia poa maisha yako. Kuendelea kuishi pasipo kutambua kusudi la maisha yako ni kuendelea kujaribisha maisha yako kwenye makucha ya ulimwengu huu.


📌Kuishi bila kutambua umeumbwa kufanikisha nini hapa duniani ni sawa na kuifanya nafsi yako iendelee kuwajibika kwa mambo mengi ambayo si miongoni mwa vipaumbele vya maisha yako. Hatari iliyopo mbele yako kutokana na maisha ya staili hiyo ni kupoteza rasilimali muhimu za maisha yako kama vile muda, nguvu na pesa. Rasilimali hizi ni nyenzo muhimu za kukuwezesha uishi maisha halisi ya kusudi la kuumbwa kwako katika kila hatua ya ukuaji unayopitia.


📌Kuendelea kuchukulia poa maisha ni kujipoteza katika makucha ya ulimwengu huu pasipo kujua kuwa unapotea. Ndiyo! Ni ukweli kuwa yawezekana umepotea lakini hutambui kuwa unapotea kwa kuwa hauna dira halisi ya maisha yako. Unapotambua kusudi la maisha yako unakuwa umepata dira ya kuongoza matendo yako hapa duniani. Kazi ya dira ni kuhakikisha inaongoza mienendo na matendo yako katika maisha ya kila siku. 


📌Hatari kubwa kwa mwanadamu wa sasa aliye hai wala siyo kifo kama inavyosadikika katika maisha yetu ya kila siku. Hatari kubwa kwa mwanadamu aliye hai kimwili ni kuishi maisha yasiyo kuwa sababu za kwa nini anaishi. Kwa mwanadamu wa aina hii, maisha yanapoteza maana kwa kuwa hana tofauti na wanyama wengine.


📌Kupitia makala hii natamani ufunguke kiakili na kiroho na kuanza kuchukulia maisha katika mtazamo wa kuwa; maisha yana maana ikiwa watu watakuwa tayari kujirudisha kwenye misingi ya kuishi kulingana na matakwa halisi ya kuumbwa kwao. Unapoishi kwa kufuata misingi ya kuumbwa kwako unaongozwa na dira maalumu na dira hiyo inakupa sababu za kuendelea kuishi. Kupitia dira hiyo, unaisha maisha yenye muunganiko wa asili na au nguvu za Kimungu kulingana na imani yako. Haya ndiyo maisha ambayo yatakuwezesha kushiriki katika tafakari kupitia misingi ya falsafa au dini, kushiriki katika uvumbuzi wa kisayansi, sanaa au teknolojia, au kushiriki shughuli nyingine za kijamii zinazowezesha kupunguza mateso kwa wanadamu. 


📌Nihitimishe kwa kusema kuwa; sababu za kwa nini unaishi zina uhusiano wa wazi na maisha yako dhidi ya jamii inayokuzunguka sambamba na asili. Asili kwa maana ya mazingira ni mhimili halisi unaowezesha uendelevu wa maisha. Anza kutafuta maana ya maisha yako kupitia uhusiano wako dhidi ya watu wengine pamoja na mazingira yako. Haya ndiyo maisha ambayo yatakutofautisha na wanyama wengine, maana sisi wanadamu tunaishi kwenye makundi ya kijamii yenye kutegemeana sisi kwa sisi na uhusiano huu uendelevu wake una uhusiano wa moja kwa moja na asili kwa maana ya mazingira. 


PATA NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU MISINGI YA MAISHA BORA HAPA DUNIANI

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.




onclick='window.open(