UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Itakayofungua Milango Ya Utajiri

NENO LA SIKU_FEBRUARI 21/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Mbinu Ya Itakayofungua Milango Ya Utajiri


📌 Habari ya asubuhi rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Hongera kwa siku hii muhimu katika maisha yako, naamini hii ni siku ya kipekee kwako kuendelea kutekeleza mikakati ya kufikia mafanikio ya ndoto zako katika kila sekta ya maisha. 


Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA


📌Katika makala ya leo nitakushirikisha njia moja ya uhakika ambayo imeshikilia utajiri unaotamani maishani mwako.


📌Katika makala ya jana tuliona kuwa hatujazaliwa kuishi maisha ya umasikini. Mungu hapendi umasikini maana umasikini hupelekea watu kushindwa kutumia uwezo wao halisi katika kuibadili dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. 


SOMA: AMKA SASA! Hivi Unatambua Kuwa Haujaumbwa Kuwa Masikini?


📌Ikiwa hatujazaliwa kuishi maisha ya umasikini ni kwa nini watu wengi wanakufa masikini? Umasikini unaendelea kutesa maelfu ya watu duniani kote kutokana na watu hawa kushindwa kuishi kanuni zinazowezesha kutengeneza utajiri.


📌Zipo njia ambazo zinawezesha watu kupata utajiri na miongoni mwa njia hizo ni: unaweza kuwa tajiri kupitia Urithi, Kushinda michezo ya bahati na sibu (Betting), Kuajiriwa, Kucheza Kamari, Kutumia ujuzi au Taaluma yako Kujiajiri au Kuanzisha Biashara yako (Ujasiliamali).


📌Miongoni mwa njia hizi zipo wazi kwa kila mtu kupata utajiri anaotamani na kufanikiwa kukimbia maisha ya umasikini.


📌Baadhi ya njia haziko wazi kwa kila mtu kwa kuwa hutegemea na asili yake na imani yake kuhusu njia husika. Mfano, si watu wote wanaweza kucheza michezo ya bahati na sibu au kamari sawa na ilivyo kwenye njia ya urithi.


📌Hata hivyo, njia zote ambazo tunasema zipo wazi kwa kila mtu kufikia utajiri wa ndoto yake zinafanya kazi ikiwa utazingatia matakwa na masharti ya njia hizo. 


📌Je! Unatamani kujua mbinu ya awali itakayokuwezesha kuwa tajiri? Bila shaka naamini unataka kufahamu mbinu hii kwa kuzingatia kuwa hakuna mtu ambaye anatamani au kuridhika kuishi maisha ya umasikini.


📌Kama hauwezi kurithi mali, kushinda michezo ya bahati na sibu au kucheza kamari unatakiwa kutafuta utajiri kwa kuhakikisha MATUMIZI YAKO HAYAZIDI PATA LAKO. Mbinu hii ni kwa watu wote wenye kuutafuta utajiri iwe kwa njia ya kuanzisha na kumiliki biashara (ujasiliamali) au  kutumia ujuzi kujiajiri/kuajiriwa.


📌Maelfu ya watu wameendelea kuzungukwa na umasikini kwa kuwa hawana bajeti inayoongoza matumizi ya pato lao. Inashangaza kuona mtu haujui kwa mwezi anatumia bajeti ya shilingi ngapi katika matumizi ya lazima (basic needs), matumizi yasiyo ya lazima (wants) achilia mbali akiba na uwekezaji.


📌Ikiwa haujui bajeti yako ni dhahiri mara nyingi utaangukia kwenye matumizi ambayo hayana tija kwenye maisha yako. Matumizi hayo yataendelea kukudhoofisha katika safari ya ukuaji wa utajiri wako. Wapo watu wanaingiza hela nyingi lakini mara zote wanateseka kipesa kwa kuwa wameshindwa kudhibiti matumizi yao.


📌Pia, ikiwa hauwezi kudhibiti matumizi yako ni rahisi kuangukia kwenye mtego wa kila mara kuongeza matumizi kadri pato linavyoongezeka. Ipo mifano mingi ya watu wa aina hii katika mazingira tunayoishi, ya watu ambao awali walizoea kuishi maisha kawaida hila ghafla wanaanza kuishi maisha ghali kutokana na ongezeko kwenye pato lao. Yawezekana na wewe miongoni mwa watu wa aina hii, kama ndivyo gutuka mapema na chukua hatua stahiki.


📌Nihitimishe kwa kusema, kudhibiti matumizi dhidi ya mapato ni hatua ya awali ya kuutafuta utajiri ambayo inaendelea kutofautisha kati ya watu masikini, watu wa pato la kati na matajiri. Mbinu hii inakutaka kutawala matumizi yako dhidi ya pato lako halisi bila kujali wingi au uchache wa kiasi cha pesa unachoingiza.


📌Haijalishi pato lako ni dogo au kubwa kiasi gani, ikiwa hauwezi kudhibiti matumizi yako utaendelea kuona pesa haitoshi kukidhi mahitaji yako katika maisha ya kila siku. 


📌NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kudhibiti matumizi yako ikilinganishwa na pato lako halisi. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.






BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com


Kupata Mafundisho Haya Kwa Barua Pepe, Jiunge na Mtandao wa Fikra za Kitajiri 

* indicates required 

onclick='window.open(