VITU 3 AMBAVYO UNATAKIWA KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 40

NENO LA LEO (JANUARI 29, 2021): VITU 3 AMBAVYO UNATAKIWA KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 40

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo tunaendelea kupewa kibali cha kuwa hai. Ni katika siku hii tunakopeshwa masaa 24 ili ndani ya masaa hayo tupate kufanya kitu cha thamani kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi la maisha yetu. Wote tunaalikwa kuitumia siku siku hii kwa faida ili mwisho wa siku tupate furaha ya moyo inayotokana na yale tuliyokamilisha.

 Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha vitu vitatu ambavyo unatakiwa kufanya kabla ya kufikia umri wa miaka 40. Tunafahamu kuwa mwanadamu ambaye amezaliwa na mwanamke siku za uhai wake hapa Duniani ni fupi sana. Kutokana na hilo, maisha ya mwanadamu yamegawanywa katika hatua tatu za ukuaji. Kuna kipindi cha utoto ambacho ni kipindi cha kujifunza na kuweka msingi wa maisha yanayofuata; kipindi cha ujana ambacho ni kipindi cha kuishi kwa vitendo yale uliyojifunza na unayoendelea kujifunza; na kipindi cha uzee ambacho ni maalumu kwa ajili ya kupunguza maangaiko na kubakia na kazi nyepesi. Mara nyingi katika jamii nyingi huwa kipindi cha ujana ni kuanzia miaka 18 hadi 45, na baada ya hapo kipindi cha uzee huwa kinafuatia. Kabla ya kuhitimisha miaka 40 kwa maana miaka 5 kuelekea kwenye kipindi cha uzee inashauriwa uwe umefanya mambo haya matatu ambayo ni msingi wa maisha yako yote:-

Msingi #1: Tafuta fursa ambayo kila mtu ameikosa katika eneo lako. Dunia haijawahi kupungukiwa kwa watu ambao wanajua nini wanataka kufanikisha. Vizazi vinakuwepo na kuondoka lakini kila kizazi hakitakosa fursa kwa ajili ya mwendelezo wa historia ya maendeleo ya mwanadamu. Kipindi cha ujana ni kipindi kwa ajili ya kutafuta fursa kwenye kila sekta au fani. Iwe umesoma na kufikia chuo kikuu au hujasoma ikiwa utashindwa kutumia kipindi cha ujana kupata fursa ya kubadilisha historia ya maisha yako hakika husitegemee miujiza katika kipindi cha uzee. Hivyo, katika kipindi cha ujana hakikisha unatafuta fursa iwe kwenye eneo lako la kazi, eneo unaloishi, chuoni na kuhakikisha unakuwa makini kutambua fursa zinazojitokeza kupitia ukuaji wa teknolojia.

Msingi #2: Jifunze jinsi ya kutengeneza pesa. Unaweza kuwa na fursa nyingi lakini zisikusaidie kuwa na uhuru wa kifedha. Ukuaji wa umri unaambatana na ongezeko la mahitaji ya kipesa. Ikiwa unahitaji kufurahia maisha yako iwe kwenye kipindi cha ujana na hata uzee ni lazima ujifunze namna ya kukuza kipato chako. Kama umeajiriwa unatakiwa kutambua kuwa mshahara unaopata katika kipindi cha ujana ni lazima utumike kukuza kipato chako kwa ajili ya kuwa salama katika kipindi cha uzee. Ikiwa umejiajiri kila shilingi unayoipata unatakiwa kuhakikisha sehemu yake inatumika kuzalisha shilingi zaidi. Kwa ujumla, kabla ya kufikia miaka 40 unatakiwa kuwa umeweka mifereji ya uhakika kwa ajili ya kukuwezesha kuishi maisha yenye uhuru wa kifedha kipindi cha maisha yako yote.

Msingi#3: Jifunze jinsi ya kuongoza watu. Mafanikio ya kila aina yanahusisha watu. Hakuna namna utaweza kufanikiwa bila kuhusisha watu kwa maana iwe ni mafanikio kwenye fani yako au biashara ni lazima uhusishe watu. Kwenye tasinia biashara, ukuaji wa biashara unategemea uwepo wa timu imara yenye mchanganyiko wa taaluma mbalimbali. Kabla ya kufikia umri wa miaka 40 unatakiwa kujifunza misingi ya uongozi kwa maana unatakiwa ujue namna ya kuongoza watu. Hakuna mtu ambaye amezaliwa na kujikuta ni kiongozi kwa kuwa uongozi bora unapatikana kwa kujifunza misingi ya uongozi. Unaweza kuwa kiongozi kupitia kuongoza (unajifunza uongozi kutokana na nafasi uliyonayo); unaweza kuwa kiongozi kwa kusaidia watu (hapa unakuwa na mbinu za uongozi japo wewe siyo kiongozi – a leader with no title); uongozi unahusisha kujifunza mbinu za kuongea (kujua nini uongee, jinsi gani uongee na muda upi wa kuongea); na hakikisha unakuwa wa mfano au kioo kuanzia ndani ya familia yako.   

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha misingi mitatu ambayo unatakiwa kuwa nayo kabla ya kufikia umri wa miaka 40. Hata hivyo, hakuna wakati ambao umechelewa kujifunza maarifa ambayo unaona ni ya muhimu katika maisha yako. Ikiwa tayari umevuka umri wa miaka 40 makala hii hailengi kukukatisha tamaa bali iwe chachu kwako kuchangamkia fursa zilizopo kulingana na umri wako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(