FAHAMU VITU 10 AMBAVYO HAVIFUNDISHWI SHULENI

NENO LA LEO (JANUARI 10, 2021): FAHAMU VITU 10 AMBAYO HAVIFUNDISHWI SHULENI

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambapo tumejaliwa uhai katika siku za maisha yetu hapa Duniani. Ni katika siku hii nikupa mwanga juu vitu ambavyo pengine pamoja na kusoma hadi elimu ya juu lakini hukufundishwa vitu hivyo katika masomo uliyofundishwa. Wakati mwingine huwa kuna msemo kuwa mfumo wa elimu unawaangusha Wajasiliamali. Msemo huu unaweza kuwa na ukweli ndani yake kwa kuzingatia kuwa asilimia kubwa ya matajiri ni wale walioachana na shule na kujitosa kwenye ujasiliamali.  

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Kuhusiana na mfumo na ujasiliamali Tajiri namba moja kwa sasa Elon Musk baada ya kumpita Jeff Bezos hapo juzi aliwahi kuorodhosha vitu 10 ambavyo vifundishwi shuleni. Karibu tupitie orodha ya vitu hivyo:-

Jinsi ya kuuza: Shuleni utafundishwa maana ya mauzo na wakati mwingine nadharia mbalimbali kuhusu mauzo lakini hautofundishwa jinsi ya kuuza. Wapo wengi wanamaliza kozi mbalimbali zinazohusiana na masoko lakini wakiingia mtaani mbinu hizo hazifanyi kazi.

Jinsi ya kufikiri: Hili ni tatizo jingine kwa mfumo wa elimu. Kufikiri ni mtihani mgumu kwa watu wengi na wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha kutoka na kutokujua namna ya kufikiri. Fikra ni chanzo cha kila aina ya mafanikio na fikra hizo ni chanzo cha kila aina ya maangamizo.

Jinsi ya kufanikisha makubaliano ya kibiashara: Wengi wanajifunza njia za makubaliano ya kifedha au biashara kupitia uzoefu. Hata wale wanaosoma kozi za biashara wengi wanafundishwa nadharia ambazo hazifanyi kazi katika mazingira ya sasa.

Jinsi ya kukabiliana na changamoto au anguko: Mfumo wa elimu unafundisha wanafunzi kuogopa changamoto na kubwa zaidi kuogopa kuanguka au kufeli. Wale wanaofanya vibaya darasani wanaonekana hawawezi kufanikisha lolote katika maisha wakati wale wanaofanya vizuri ndiyo wanaonekana watafanikiwa kimaisha. Hata hivyo, uhalisia katika ni tofauti.

Jinsi ya kutunza muda: Muda ni pesa kwa kuwa ni msingi wa kufanikisha kila aina ya mafanikio kwenye maisha ya mhusika. Pamoja na ukweli huu, mfumo wa elimu haujaweka kipaumbele katika kuandaa wanafunzi kwenye mbinu za kutunza muda pindi wakiwa masomoni au baada ya kuhitimu masomo yao.

Jinsi ya kuwekeza pesa: Kwenye suala la uwekezaji, asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu wanaingia mtaani wakiwa hawana mbinu za uwekezaji. Ndiyo maana matajiri wengi pamoja na kwamba wengi hawajasoma lakini wana macho ya kuona fursa za uwekeazaji kuliko wasomi. Na mara nyingi wasomi hawa huwa ndiyo wanapeleka taarifa za fursa muhimu kwa Matajiri huku wakiishia kupokea vipesa kidogo kutoka kwa wawekezaji hao. Wasomi wengi hawana msingi na taarifa sahihi za sehemu zipi wanaweza kuwekeza pesa zao.

IKIWA UNAHITAJI MWAKA 2021 KUJENGA TABIA YA KUJILIPA KWANZA: SOMA MAKA HII

Kanuni za mafanikio: Mfumo wa elimu haufundishi mbinu za mafanikio na ndio maana wahitimu wengi ambao hawajibidishi kutafuta maarifa mapya nje yale waliyofundishwa darasani wanateseka kimaisha. Wapo wasomi wanapokea mishahara mikubwa lakini kwa kuwa hawana kanuni za mafanikio wanaendelea kuishi maisha kwenye mzunguko wa umasikini.

Jinsi ya kugundua dhamira/shauku: Wahitimu wengi wanaangaika kimaisha kwa kuwa toka wakiwa wadogo hawakuandaliwa kugundua nini hasa wanataka kupata katika maisha yao. Wengi wanashindwa kujua kusudi la maisha yao na matokeo yake wanazunguka huku na huko pasipo kuridhisha hitaji la nafsi zao.

Jinsi ya kuanzisha biashara: Asilimia kubwa ya biashara zinazoanzishwa na Wasomi zinakufa kutokana na kuanzishwa pasipo kuzingatia mahitaji muhimu ya biashara husika. Wasomi hao wanapoteza pesa nyingi kwa vile wanaanzisha biashara ambazo hawana uelewa wa kutosha na zaidi ya yote hawana muda wa kusimamia biashara hizo.

Msingi wa mafanikio: Msingi wa mafanikio ya aina yoyote ile upo ndani ya mhusika na mafanikio yanapatikana pale mhusika anapotoa thamani kwa wengine. Chochote utakachofanya chenye thamani kwa wengine kwa maana kinakidhi mahitaji yao kina nafasi ya kukupa mafanikio. Hivyo, mafanikio yanapatikana kwa kutoa thamani kwa wengine. Iwe kwenye biashara au kazi msingi namba moja ambao unatakiwa kutanguliza ni kutoa thamani kwa walengwa wako.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza vitu 10 kutoka Elon Musk ambavyo hatukufundishwa kwenye mfumo wa elimu. Hata hivyo, elimu haina mwisho hivyo kila mmoja wetu ana nafasi ya kuendelea kujifunza kuhusiana na mambo kadhaa ambayo hukufundishwa shuleni. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(