NENO LA LEO (JANUARI 05, 2021): JAMBO MOJA LA KUFAHAMU KUHUSU MALENGO YAKO YA 2021.
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine tumepata kuamshwa salama tukiwa na nguvu na hali kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni katika kipindi hiki tuna kila sababu ya kutafakari matendo tunayokusudia kuchukua katika siku hii ya leo ili tupate kuwa na siku bora. Moja ya hatua ambazo unatakiwa kuchukua ni kuanza kwa kujiweka mbele za Mungu sambamba na kuainisha malengo ya siku ya leo.
Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA
Katika neno la tafakari ya leo tutajifunza kitu muhimu cha kuepuka ili upate kukamilisha malengo uliyojiwekea katika kipindi cha mwaka 2021. Najua una malengo ambayo unakusudia kuyakamilisha katika kila sekta ya maisha yako. Unaweza kuwa umedhamiria kupunguza uzito (lengo la kiafya), unaweza kuwa umepanga kujenga nyumba ya kuishi (lengo la kifamilia), unaweza kuwa umepanga kuanzisha biashara (lengo la kiuchumi) au unaweza kuwa umepanga kusoma/kuandika vitabu kadhaa (lengo la ukuaji wa kiroho na nafsi).
Malengo yote hayo si lolote ikiwa hauna mpango wa utekelezaji wake. Leo hii tupo tarehe tano ya mwezi wa kwanza kwa maana unatakiwa uwe tayari umeshaanza kutekeleza malengo uliyojiwekea katika kipindi cha mwezi wa kwanza. Jambo moja ambalo huwa linakwamisha watu kufikia malengo wanayojiwekea ni tabia ya "KUAIRISHA". Huu ni ugonjwa hatari kwa malengo uliyojiwekea katika kila sekta ya maisha yako.
Ugonjwa huu huwa unaambatana na dalili za kukufanya uone kuna nafasi iliyo bora zaidi ya hiyo uliyonayo sasa. Mara kadhaa tunashindwa kufanikisha malengo ya siku husika na kujisemea nitafanya kesho bila kujua kuwa na kesho ilitakiwa kuwa na majukumu yake. Kila siku tunasogeza mbele na ghafla tunajikuta mwezi umeisha. Majukumu ya mwezi ulioisha yanasogezwa mwezi unaofuata na hatimaye tunajikuta mwaka umeisha bila kukamilisha yale tuliyokusudia kufanya katika kila sekta ya maisha yetu.
Malengo hayana maana ikiwa tunaendekeza tabia ya kuairisha majukumu ya msingi. Hivyo, pamoja na nia ya dhati uliyonayo ikiwa hautajenga nidhamu ya kujisukuma kutekeleza majukumu ya kila siku hakika itakuwa ni ndoto kufanikisha malengo yako.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa jambo la msingi katika kukamilisha malengo yetu ni kuepuka tabia ya kuairisha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS. Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
onclick='window.open(