NENO LA LEO (JANUARI 26, 2021): FAHAMU CHANZO HALISI CHA MSONGO WA MAWAZO
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tunaalikwa kuendelea kufanya yale yanayoboresha maisha yetu. Kila siku asubuhi tunaalikwa kujiuliza swali hili: ni ipi ajenda yangu ya msingi katika siku hii leo? Majibu ya swali hili yanakupatia majukumu ya kukamilishwa katika siku husika. Hata hivyo, unayofanya kila siku yanatakiwa kuwa na mwendelezo siku hadi siku.
Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA
Katika neno la tafakari ya leo tutaangalia chanzo halisi cha msongo wa mawazo katika maisha ya watu wengi. Katika Ulimwengu wa sasa tunashuhudia ongezeko kubwa la watu katika jamii ambao wanaishi kwa msongo mkubwa wa mawazo. Hali hii inaweza kuthibitishwa kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya wanaojiua kwa sumu, kujinyonga au kwa jinginezo.
Sababu zipo nyingi ambazo zinapelekea msongo wa mawazo kwa idadi kubwa ya watu katika jamii. Moja ya sababu ni kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ambayo imepelekea mmonyoko wa maadili katika jamii. Pia, sababu nyingine ni kupanda kwa gharama za maisha katika ulimwengu wa sasa ikilinganishwa siku za nyuma. Vyote hivi kwa pamoja vimepelekea mafarakano ndani ya familia hali inayopelekea ongezeko la msongo wa mawazo kwa wahusika. Je pamoja na hayo ni kipi ambacho unahisi kimekuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwako?
Je msongo wa mawazo unatokana na Mkuu wako wa kazi?, Je msongo wa mawazo umekuwa ukisababishiwa na mwenza wako? Je msongo wa mawazo unatokana watoto wako? He msongo wa mawazo unatokana na changamoto za kiafya? Je msongo wa mawazo umetokana na msongamano wa magari barabarani? Je msongo wa mawazo unatokana na watu wanaokuzunguka? Je msongo wa mawazo unatokana na mahitaji makubwa ya kipesa? Je msongo wa mawazo unatokana na mwenye nyumba yako?
Tunaweza kuorodhesha sababu nyingi kama chanzo cha msongo wa mawazo lakini ukweli utabakia kuwa chanzo halisi cha msongo wa mawazo kipo ndani mwako. Chanzo halisi cha msongo wa mawazo ni fikra. Jinsi unavyoitikia sababu zote hizo zilizoorodheshwa katika mfumo wako wa fikra ndicho kinapelekea uwe na msongo wa mawazo. Unaweza kuamua kuwa na mtazamo chanya au hasi katika kila hali inayokuzunguka. Unavyokuwa na mtazamo hasi kwenye changamoto iliyopo mbele yako inapelekea kuwa na msongo na hatima yake ni kuharibu mfumo mzima wa maisha yako.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumeona kuwa chanzo halisi cha msongo wa mawazo ni fikra. Fikra hasi hupelekea mtazamo hasi na hatima yake ni msongo wa mawazo. Anza sasa kuwa na fikra chanya kwenye kila hali inayokukabili. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
onclick='window.open(