KWA NINI UNATENGANISHA FURAHA NA MAFANIKIO YAKO?.

NENO LA LEO (JANUARI 06, 2021): KWA NINI UNATENGANISHA FURAHA NA MAFANIKIO YAKO?.

✍🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ambayo tunapata wakati mwingine wa kuendeleza yaliyo mema katika historia ya maisha yetu. Ni leo hii tuna kila sababu ya kutambua kuwa tunaishi mara moja na kila siku ni muhimu katika kufanikisha maisha hayo mafupi. Hata hivyo, ufupi wa maisha hayo unatulazimisha kuhakikisha tunaishi kila siku kwa ukamilifu wake. Kumbe, hatupaswi kuacha deni kwa ajili ya kesho maina hatuna uhakika na kesho.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

✍🏾 Ikiwa maisha ni sasa hatuna budi ya kutenganisha furaha na mafanikio. Tutakuwa tunakosea ikiwa tunapima furaha ya maisha yetu kutokana na ngazi ya mafanikio. Maisha yamejaa kila aina ya vikwazo ambavyo ikiwa unategemea furaha yako itokane na kiwango cha mafanikio utajikuta muda mwingi umeishi kwa huzuni. 

✍🏾 Hata hivyo, furaha halisi kila siku inapatikana kutokana na upendo wa ndani katika yale tunayofanya - furaha ipo kwenye majukumu yetu ya kila siku. Ikiwa haupendi kile unachofanya hakika hautoweza kuwa na furaha kwa kuwa muda mwingi ratiba ya maisha ya kila siku ni kwa ajili ya ukamilisho wa majukumu ya msingi. Hivyo, furaha inatakiwa kuanzia tangu pale unapoianza siku kama ni kwa mazoezi unawajibika kufurahia jukumu hilo, kama ni kazini au biashara una kila sababu ya kufurahia kila unachofanya ukiwa sehemu ya kazi, vivyo hivyo, ukiwa karibu na wapendwa wako ioneshe furaha yako kutokana na uwepo wao.

✍🏾 Mwanadamu ni kiumbe chenye hisia ya tamaa na uchoyo. Hisia mbili hizo ndizo zinawafanya watu wote kila kukicha wajitose kwenye majukumu. Vile vile, kutokana na hisia hizo hakuna siku kiumbe mwanadamu anaridhika na hatua ya mafanikio aliyonayo. Ni jambo la heri kuona kuwa hatua moja ya mafanikio inafungua hatua mbili zaidi za kusonga mbele kimafanikio. Tafsiri yake nini hasa kwenye furaha ya maisha? Hapa nataka utambue kuwa ikiwa unapima furaha yako kulingana na mafanikio unayopata utajikuta muda wote hauna furaha kwa kuwa hakuna siku utaridhika na mafanikio ya maisha. Mfano, utapambana sana kutafuta pesa na kweli utafanikiwa kupata pesa za kutosha lakini baada ya mafanikio hayo utajiona una ombwe kubwa kwenye sekta nyingine ya maisha.

✍🏾 Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa ni kosa kubwa kutenganisha furaha na mafanikio. Furaha ipo kwenye majukumu yetu ya kila siku na wala siyo kwenye matokeo ya majukumu hayo. Hivyo, tuna kila sababu ya kutambua kuwa mafanikio siyo chanzo cha furaha bali mafanikio yanatokana na furaha katika yale unayofanya. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.


πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(