Habari
ya asubuhi mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka
salama na upo tayari kuendeleza pale ulipoishia jana. Ni siku nyingine tunapata
nafasi ya kuendelea kutoa thamani kwa ajili ya kuwa bora zaidi katika majukumu
yetu.
Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA
Mabadiliko ni jambo ambalo kila mtu anatamani. Pamoja na kwamba wengi wanatamani mabadiliko ukweli unabakia kuwa wanaofikia kwenye kilele cha mabadiliko wanayotamani ni wachache. Huo ndiyo ukweli kwa kuwa mabadiliko yanamtaka mhusika kubadilisha mfumo mzima wa maisha jambo ambalo ni gumu ikiwa mhusika hajadhamiria kubadilika kweli. Katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha hatua tatu ambazo kila mtu anatakiwa kupitia katika kufikia kilele cha mabadiliko anayohitaji.
Hatua #1: Mabadiliko kwenye tabia au
changamoto husika – Katika hatua hii mhusika anatakiwa awe tayari kutafuta
mshauri ambaye atamsaidia kufikia kilele cha mabadiliko anayotamani. Kazi ya
mshauri ni kumpa mhusika mwongozo ambao utasaidia kubadilisha tabia/changamoto
ambayo imekuwa ikimkwamisha kufikia malengo yake. Mfano, mtu anaweza kutafuta
ushauri wa jinsi gani anaweza kukabiliana na changamoto za kikazi, msongo wa
mawazo, changamoto za kifedha au jinsi ya kukuza mauzo kwenye biashara. Hii ni
hatua muhimu ambayo mhusika anatakiwa kuitumia kwa ajili ya kubadilisha mtazamo,
fikra au matendo kuhusiana na changamoto iliyopo mbele yake. Mfano, katika
hatua hii mhusika anatakiwa kubadilika kutoka kwenye kuwa na hofu na kuanza kujiamini
au kutoka kwenye kutokuchukua hatua na kuanza kuchukua hatua za kivitendo.
Hatua #2: Mabadiliko katika sehemu/sekta maalum ya maisha – Katika hatua hii mhusika tayari ametambua changamoto anayotaka kubadilisha na yupo tayari kukabiliana kwa vitendo na tatizo linalomsumbua katika maisha yake ya kila siku au jamii inayomzunguka. Mfano, mtu anaweza kuwa anahitaji kuboresha maisha yake kwenye sekta ya mahusiano, mauzo, malezi, kujiamini n.k. katika hatua hii muhusika anakuwa na programu ya kubadilisha sehemu ya maisha yake ambapo anaweza kusoma vitabu au makala yanayohusiana na changamoto aliyonayo. Ili kuwa na mabadiliko ya jumla, mhusika anatakiwa kuweka ratiba ambayo anapaswa kuitekeleza katika majukumu yake ya kila siku.
Hatua #3: Mabadiliko ya jumla – Hatua hii inahitimisha mabadiliko ya jumla katika mfumo mzima wa maisha ya mhusika. Katika hatua hii muhusika anabadilika moja kwa moja kutoka kwenye hali yake ya awali na kuingia kwenye ulimwengu mpya kulingana na hitaji la mabadiliko katika maisha yake. Hivyo katika hatua hii mtu anabadilisha mazoea yake yote katika kila nyanja ya maisha. Mfano, mabadiliko ya jinsi mtu anavyojitazama mwenyewe, kujiamini na mtazamo wake kwa watu wanaomzunguka. Hata hivyo, hatua hizi zinategemeana na katika kila hatua lazima mhusika awe tayari kubadilika ndani mwake ili hatimaye mabadiliko hayo yajitokeze katika mfumo wa maisha ya nje.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza hatua tatu za kuzingatia katika kuelekea kwenye kilele cha mabadiliko unayotamani. Hata hivyo, mabadiliko yoyote kwenye maisha ya mtu ili yadumu ni lazima yajengwe kwenye mfumo wa maisha unaolenga kuwa na mafanikio ya muda wote (life time success). Ili kufanikiwa katika mabadiliko ya namna hii ni lazima mfumo mpya wa maisha uambatane na vitendo. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya
pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka
kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu
inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu
Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com