[USHAURI] TENGENEZA SABABU ZA ZINAZOKUSUMA

NENO LA LEO (JANUARI 11, 2021): [USHAURI] TENGENEZA SABABU ZINAZOKUSUMA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine katika juma jipya ambapo tumepewa tena kibali cha kuendelea kuwa hai. Kama ilivyo kawaida yetu, siku hii ni miongoni mwa siku za ushindi ambazo tumejaliwa katika kipindi cha maisha yetu. Nasema siku ya ushindi  kuwa kila mara nakukumbusha umuhimu wa kutengeneza ushindi mdogo mdogo katika kila siku ya maisha yako. Ushindi huo mdogo unapounganishwa katika kipindi chote cha maisha yako unatengeneza mafanikio makubwa ambayo kila mmoja anabakia kujiuliza uliweza vipi kufanikisha mambo yote hayo.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Katika neno la tafakari ya leo tutaona kwa nini unatakiwa kuwa na sababu za msingi ambazo zinakusukuma katika kila lengo. Mara nyingi watu wengi huwa wanaishia kwenye hatua ya matokeo wanayotamani kupata katika kila lengo. Wengi wetu tukiulizwa kwa nini tunataka matokeo katika kila lengo tulilojiwekea ni wachache ambao wana sababu zinazowasukuma kutafuta matokeo hayo.

Sababu ni muhimu kuliko matokeo kwa kuwa sababu ndizo zinakupa msukumo wa kutafuta matokeo. Mfano, kila mtu anatamani kuwa na uhuru wa kifedha. Kwenye hilo wengi huwa wanaweka lengo kama vile: Nataka kuongeza pato langu kutoka....hadi..... Ni jambo zuri lakini mhusika ukimuuliza kwa nini anahitaji kuongeza pato lake leo atakupa majibu haya na kesho atakupa majibu mengine. Hali hii inatokea kwa kuwa hana sababu maalumu zinazomsukuma kuongeza pato lake.

Kutokana na kutokuwa na sababu zinazotusukuma, wengi wetu huwa tunakimbilia kwenye matokeo na mwisho wake tunasahau hatua za kuchukua ili kufikia matokeo husika. Kila lengo huwa linaambatana na shughuli ambazo mara nyingi huwa zinajikita kwenye kutatua changamoto za jamii. Mfano, lengo la kuhitaji kukuza pato linatakiwa liambatane na changamoto za jamii ambazo kwa kuzitatua zitasaidia kukuza pato lako. 

Unaweza kutatua changamoto za jamii kupitia mahusiano yako ya kifamilia. Unaweza kutatua changamoto za kijamii kupitia kutoa elimu kwa jamii. Unaweza kutatua changamoto za jamii kupitia fani yako. Unaweza kutatua changamoto za jamii kupitia kipaji chako na unaweza kutatua changamoto za jamii kupitia biashara yako. Kupitia sehemu zote hizo unapata sababu zinazokusukuma kufikia matokeo unayotamani kwa kila lengo.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa sababu za kutaka matokeo kwa kila lengo ni za muhimu kuliko kuishia kwenye kutamani matokeo husika. Kupitia malengo tunaweza kutatua changamoto za jamii na katika kufanya hivyo tukafikia ukuaji (development) tunaotamani kwenye kila sekta ya maisha yetu. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.


PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKA HII

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com 

onclick='window.open(