NENO LA LEO (JANUARI 16, 2021): SOMO MUHIMU KUHUSU KIPATO NA UHURU WA KIFEDHA
Habari
ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine
ambapo tumebahatika kupata kibali cha kuendelea kuwa hai. Ni katika siku hii
nakukumbusha kuwa safari bado ni ndefu katika kufikia kilele mafanikio katika
maisha. Safari hii imejaa milima na mabonde na vyote hivyo ni kwa ajili ya
kutupa changamoto ili tufike salama. Huu siyo wakati wa kukata tamaa kutokana
na changamoto zilizopo mbele yako bali wakati huu ni wakati bora kwako
kunyanyuka, kuweka mikakati upya na kuanza kutekeleza malengo uliyojiwekea
katika sekta ya maisha yako.
Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA
Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo ongezeko la kipato limekuwa upanga wa kuangamiza watu wengi katika jamii. Watu wengi katika jamii yetu huwa wanaamini kuwa ongezeko la kipato ni njia halisi ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha. Ukifanya mahojiano na waajiriwa wengi utagundua kuwa asilimia kubwa kati yao wanaamini kuwa maisha yao yapo jinsi yalivyo kwa kuwa wanapokea mishahara kiduchu. Wengi wanaamini kuwa ongezeko la mshahara litabadilisha maisha yao. Vivyo hivyo, wafanyabiashara nao wanaamini kuwa kuongezeka kwa faida katika biashara zao ni hatua muhimu ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha.
Ni kweli kuwa ongezeko la mshahara au faida ni muhimu katika kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kifedha. Hata hivyo, kiuhalisia watu wengi katika jamii wameangamizwa na ukuaji wa kipato. Baada ya kuongezeka kwa mshahara au faida, wengi wanajikuta kwenye mfumo ule ule wa upungufu wa fedha katika maisha ya kila siku. Wapo watu wengi katika jamii ambao wanalipwa mishahara mikubwa lakini tunashuhudia wakiangaika kipesa. Vivyo hivyo, wapo wafanyabiashara ambao pamoja na kutengeneza faida kubwa katika biashara lakini bado biashara wanazofanya zimedumaa. Pia katika jamii zetu mifano mingi ambayo inahusisha watu ambao wamepoteza mwelekeo kutokana na ongezeko la kipato cha ghafla katika maisha yao.
Wote ni mashahidi kuwa katika jamii ni kawaida kukuta Mhudumu wa Ofisi ana maisha mazuri kuliko Maafisa wenye mishahara mikubwa. Hali iko hivyo pia, husishangae kukuta Wafanyabiashara za kawaida (biashara ndogo) kuwa na maisha mazuri ikilinganishwa na baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa. Kumbe, somo la kujifunza hapa ni kwamba “uhuru wa kifedha unategemeana na jinsi unavyotumia pesa unazopata”.
Ufunguo wa kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha unahusisha vitu vitatu: Moja, ni lazima uwe tayari kutengeneza pesa – katika kila hali unazimika kufanya kazi kwa bidii na weledi ili upate kuingiza pesa. Mbili, ni lazima utumie pesa zako kutengeneza pesa zaidi – katika hili huwa napenda kutumia msemo kuwa “pesa zinaenda sehemu zinakopendwa zaidi na kuthaminiwa”. Haijalishi ni pesa kiasi gani unaingiza kwa siku au mwezi ikiwa hauthamini pesa hiyo kamwe haiwezi kuongezeka zaidi. Tatu, ni lazima matumizi yako mara zote yasizidi pato lako – ikiwa unaishi maisha ya gharama zaidi ya kipato unachoingiza hakika kipindi cha maisha yako chote utaendelea kuangaika kipesa.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa uhuru wa kifedha unapatikana kwa kuthamini pesa unayopata. Pesa inatengeneza pesa, kwa maana kila pesa unayopata hakikisha kuna kiasi kinachotumika kuzalisha pesa zaidi katika siku za baadae. Hiyo ndiyo siri ambayo watu wote wanaitafuta kwa ajili ya kubadilisha maisha yao. Hata hivyo, wanaofanikiwa kuiishi ni wale wenye maono makubwa na nidhamu katika maisha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya
pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka
kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu
inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN
TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com