[USHAURI] HUSIRUHUSU FURAHA IZIDI KIPIMO

NENO LA LEO (JANUARI 07, 2021): [USHAURI] HUSIRUHUSU FURAHA IZIDI KIPIMO

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya kipekee ambayo imejaa matumaini kwetu kwa ajili ya kufanikisha majukumu muhimu katika siku ya leo. Ni siku ya kipekee na yenye furaha kwa taifa na hasa wapenzi wa Simba SC tukiachilia mbali upinzani wa Kariakoo pacha.

Katika neno la tafakari ya jana tulijifunza kuwa furaha katika maisha hatakiwi kupimwa kwa kipimo cha mafanikio. Naamini neno hili litakuwa limetujenga zaidi kwa kuzingatia kuwa maisha yetu kila siku yanahusisha mapambano dhidi ya majukumu yaliyopo mbele yetu. Hata hivyo, katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha athari za furaha inapozidi kipimo. 

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Kwa kulitazama tukio la jana ambalo nimegusia la Simba SC kutinga hatua ya makundi kuna mengi nimejifunza kuhusu furaha inapozidi kipimo. Kila kitu fanyeni kwa kiasi, ni moja ya mafundisho katika maandiko matakatifu. Ndicho kinachodhihirisha hata kwenye hisia ya furaha kwa mwanadamu. 

Moja ya athari za furaha inapozidi ni uwezekano wa kupoteza maisha au kuishia kwenye majeraha ambayo hayakutarajiwa. Jana mitaani tumeona watu hasa boda boda jinsi walivyokuwa wanaendesha pikipiki kwa fujo bila kufikiria kuwa hivyo ni vyombo vya moto. Achilia mbali tunashuhudia au kusikia visa kadhaa vinavyohusisha watu ambayo wanapoteza maisha kutokana na kuruhusu hisia ya furaha itawale akili yao kuliko inavyotakiwa.

Athari nyingine ya furaha iliyopitiliza ni kuingia kwenye matumizi ya fedha ambayo hayakukusudiwa. Katika siku ya jana tumeshuhudia jinsi ambavyo sehemu za starehe zilijaa watu kana kwamba ilikuwa ni mwisho wa juma. Matokoe yake watu wameishia kwenye matumizi makubwa ambayo hayakuwa sehemu ya mpango wa matumizi kwa siku ya jana.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa furaha ni hisia ambayo inaweza kuathiri maisha yetu pale inapozidi kipimo. Kila mara unapokuwa kwenye hali ya furaha iliyopitiliza hakikisha haupotezi utu wako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com 

onclick='window.open(