HAKIKISHA MWAKA 2021 UNAJENGA TABIA YA KUJILIPA KWANZA.

NENO LA LEO (JANUARI 8, 2021): HAKIKISHA MWAKA 2021 UNAJENGA TABIA YA KUJILIPA KWANZA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tumepata kibali cha kuendelea kuwa bora katika yale tunayofanya. Wajibu uliopo mbele yetu katika siku hii nikuendelea kuishi malengo ambayo tumejiwekea katika kipindi hiki cha mwaka 2021.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Moja ya lengo ambalo nakushauri ulipe kipaumbele katika mwaka huu ni kuhakikisha unakuwa na tabia ya kujilipa kwanza. Maana ya kujilipa kwanza, ni kuhakikisha kabla ya kufanya matumizi yoyote unatenga asilimia flani kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwako na kuiwekeza sehemu ambayo hauwezi kuigusa hela hiyo. Baada ya kujilipa fedha inayobakia ndiyo fedha halali kwa ajili ya matumizi au mahitaji yako kulingana na vipaumbele katika bajeti yako. Kiasi unachojilipa kinakuwa ni maalum kwa ajili ya uwekezaji au akiba ili kukuza pato lako katika maisha yako ya baadae.

Mfano; kama wewe ni mfanyabiashara ambaye umedhamiria kujilipa asilimia kumi (10%) katika faida unayotengeneza. Hesabu ya haraka ni kwamba ukipata faida ya laki moja, 10% yake ambayo ni elfu kumi ndo fedha unayotakiwa kujilipa. Elfu tisini inayobakia ndiyo unaweza kuigawa kwenye mahitaji mengine. Pia, kama ni mwajiriwa na umeamua kujilipa asilimia kumi ya mshahara wako ambao kiwango cha mshahara ambacho mfano ni 300,000.00. Unachotakiwa kufanya ni kutenga elfu 30,000.00 (10%) kila mwezi na kuiwekeza kwenye akaunti maalumu unayojilipa. Kiwango kinachobakia ndicho stahiki yako kufanikisha mahitaji mengine.

Je niwekeze wapi fedha ninazojilipa? Nimegusia kuwa fedha unazojilipa unatakiwa kuziwekeza sehemu salama na ni vyema ikiwa inaongezeka thamani. Kwa hapa Tanzania unaweza kuwekeza kwenye akaunti maalum katika benki zilizopo karibu na eneo lako, unaweza kununua Hisa za Kampuni mbalimbali (kwenye hili unatakiwa kuwa makini), unaweza kununua Hatifungani/Dhamana za Serikali au unaweza kuwekeza kwenye kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Mutual Funds).

Nifanye nini ili mwaka 2021 uwe wa tofauti katika kutenga akiba? Katika kipindi cha mwaka 2021 nimeweka lengo la kuwasaidia watu 50 kujenga tabia ya kujilipa kwanza. Vijana hao katika nyakati za tofauti za kipindi cha mwaka huu nitawapa mafunzo (mentorship) kwenye kujilipa kwanza na mwongozo wa sehemu sahihi ya kuwekeza pesa wanayojilipa kila mmoja kulingana na kiasi ambacho atachagua kujilipa kwa kutegemea pato lake. Kila mwezi nitahakikisha kila mmoja ananipa mrejesho wa kiasi ambacho amejilipa na uthibitisho wa maandishi kama vile ujumbe wa miamala iliyofanyika wakati anajilipa au uthibitisho wa hati ya malipo (payment slip ya benki). Nami sitakuwa nyuma nitahakikisha namthibitishia kila mmoja kiasi ambacho nimejilipa katika mwezi husika kama sehemu ya kuwapa hamasa.

Je nifanye nini ili kuwa sehemu ya wanufaika? Ni rahisi sana kuwa sehemu ya wanufaika hila kwa masharti matatu tu:-

  • Utatakiwa uwe na nidhamu binafsi katika kutekeleza yale ambayo tutakuwa tunakubaliana kwa pamoja.
  • Utatakiwa kuchangia gharama ya Tshs. 50,000.00 (elfu hamsini) kwa ajili ya ada ya coaching (ufuatiliaji wangu pamoja na mafunzo) ambayo nitakuwa nakupatia katika kipindi chote cha mwaka mzima.
  • Inabidi uwe na chanzo chochote cha mapato bila kujali wingi au uchache wa kiasi cha pesa unachopata kila mwezi.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza maana ya kujilipa kwanza na kwa nini unatakiwa kujenga tabia ya kujilipa kwanza. Kwa kifupi tumeona sehemu zipi salama za kuwekeza pesa unayojilipa. Pia, nimetoa wito kwako kuwa miongoni mwa watu hamsini (50) ambao watakuwa sehemu ya mpango maalumu wa kujengewa tabia ya kujilipa kwanza katika kipindi kizima cha mwaka 2021. Hakikisha unakuwa sehemu ya Mpango huu maalum ili kuonesha tofauti kwenye hatua za ukuaji wako kwenye sekta ya fedha.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(