Habari
ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambapo
tumejaliwa kuwa na uhai. Wajibu wetu katika siku ya leo ni kuhakikisha
tunaendelea kuwa bora katika yale tunayofanya. Yawezekana kuna mambo mengi ambayo
tungependa kufanya siku ya leo lakini katika yote nakushauri uchague mambo
kadhaa ambayo yanakupa muendelezo kwa pale ulipoishi jana. Kwa kufanya hivyo
kila siku, baada ya muda wa miaka kadhaa kila mtu atakushangaa uliwezaje
kufanikiwa katika yale utakayokuwa umefanikisha.
Ni ukweli ambao unakubalika kwetu sote kuwa kila mtu anatamani kuona anakuwa wa kipekee kwenye kila sekta ya maisha yake. Kila mtu anatamani kuwa na afya bora – hakuna anayebisha kwenye hilo. Kila mtu anatamani kuwa na umbo zuri iwe kwa jinsia ya kike au jinsia ya kiume – hakuna anayebisha juu ya hilo kwa kuwa kila mara tunaona watu wanakesha kwenye mazoezi kwa ajili ya kujenga miili. Hakuna anayebisha kuwa kila mtu anatamani kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha. Hakuna anayebisha kuwa kila mtu anatamani kufanikiwa kuwa na kazi au biashara nzuri na yenye mafanikio. Kwa ujumla tunakubaliana kuwa kila mtu anahitaji kuwa wa kipekee katika kila sekta ya maisha yake.
Jambo moja ambalo litakuwezesha uwe wa kipekee ni VITENDO (ACTIONS) vikiambatana na MAONO (VISION). Huo ndiyo ufunguo wa kufanikisha kila aina ya upekee unahitaji katika maisha yao. Kila siku tunaamka na kuzama kwenye majukumu (vitendo) kwa ajili ya kujipatia mkate wa siku. Hata hivyo, ikiwa kazi tunazofanya haziongozwi na maono tunajikuta tunazunguka huku na kule bila mafanikio. Maana yake ni kwamba vitendo bila maono ni sawa na bure.
Je unahitaji kuwa na mwili wenye afya bora na uliojengeka vizuri? Kuanzia sasa jipatie muda wa miezi sita ya kufanikisha hitaji lako. Katika kipindi hicho cha miezi sita hakikisha unafanya kile ambacho unatakiwa kufanya kwa ajili ya kuwa na aina ya mwili unaotamani. Hakika baada ya kipindi cha miezi sita utakuwa na mwili uliojengeka kiumbo na afya bora kuliko asilimia 90 ya watu katika eneo lako. Hakuna muujiza bali kinachokubadilisha na kufanya kile ambacho wengine wanafanya kwa ajili ya kujiimairisha kiafya na kimwili.
Je unahitaji kufanikiwa kwenye biashara yako? Hakuna muujiza ambao utakufanya ufanikiwe kibiashara au kwenye kazi yako zaidi ya kujitofautisha na wengine. Kuanzia sasa jipatie muda wa miezi sita na kuendelea kwa ajili ya kufikia kile unachotamani kwenye biashara au fani yako ya kazi. Ikiwa muda mrefu umekuwa unatamani kuanzisha biashara hakikisha katika kipindi hicho cha miezi sita unaanzisha bila kujali ukubwa wa mtaji utakaoanza nao. Unapoanzisha hatua ya kwanza kuna nguvu kubwa ya kubadilisha yasiyowezekana yakawezekana. Hakika katika kipindi cha miezi sita ukiwa na nidhamu ya kufanya kile kinachotakiwa kufanywa katika biashara au kazi yako utakuwa wa kipekee kwa asilimia 90 zaidi ya watu wengi katika kile unachofanya.
Je umekosa mtaji wa kuanzisha biashara kwa muda mrefu? Watu wengi wanatamani kuanzisha biashara lakini wengi wanashindwa kutokana na kutokuwa na mtaji. Hata hivyo, ukiuuliza mtu unahitaji mtaji kiasi gani na mchanganuo wa kiasi anachotaka utashangaa kuona kuwa wengi hawajui kiwango cha mtaji wanachotaka. Pia, matumizi ya kiwango hicho ni kitendawili kwa wale ambao wanajua kiwango cha mtaji wanachohitaji. Kumbe, hali hii inadhihirisha kuwa mtaji upo ndani ya uwezo wetu kutoka kwenye pesa tunazopata kila siku. Ndiyo inawezekana kupata mtaji katika kipindi cha miezi 6. Mbona kila siku unatapa hela ya kifurushi, mbona kila siku unapata hela ya kula, mbona kila siku unapata hela kinywaji na mengine mengi. Yote hayo unayapata kwa kuwa umeyapa kipaumbele. Kuanzia sasa weka mkakati wa kufanikisha mtaji unaohitaji katika kipindi cha kuanzia miezi sita na kuendelea. Hakika baada ya miezi sita utashangaa una asilimia 90 ya mtaji ukilinganisha na watu wengine wanaokuzunguka.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa vitendo na maono katika kufikia hitaji la maisha yetu. Tunashindwa kufanikiwa siyo kwamba hatuna uwezo wa kufanikiwa bali tunashindwa kuwa tunakosa vitendo ambavyo vinaongozwa na maono. Kwa kutokuwa na maono tunafanya mambo mengi ambayo hayana muunganiko au uhusiano na mwisho wake kila mara tunaangaika kimaisha kwa kuwa vitendo tunavyofanya havitufikishi popote. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya
pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka
kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu
inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine MathiasMawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com